Featured Post

RC MASENZA AZIPIGA JEKI SHULE TANO MKOANI IRINGA


 Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari ambayo inajengwa kwa nguvu za wananchi na serikali kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu mkoani Iringa.

 Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari na akiuliza kitu kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyanzwa
 Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari akielekea kukagua vyoo vya shule ya sekondari ya Nyanzwa
 Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo vya shule ya Nyanzwa
 Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo katika sekondari ya Ibumu
 Na hili ni moja ya jengo ambalo linajengwa kwa ajili ya maabara za shule ya sekondari ya Ibumu

Na Fredy Mgunda, Kilolo

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametoa jumla ya shilingi milioni nne (4,000,000) kwa ajili ya kuchochea manendeleo ya ujenzi  majengo kwenye shule nne za sekondari  ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi wa shule hizo wanasoma bila kuwa na usumbufu wowote ule.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa shule mpya za sekondari zilizopo tarafa ya Mazombe mkuu wa mkoa Amina Masenza alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kulipia kitu mchango wowote ule utakaochangishwa na walimu.

“Mimi nimetumwa na Rais kusisimamia ila ya chama cha mapinduzi kuhakikisha inatendewa haki katika kuleta maendeleo hivyo ni lazima nihakikishe wanafunzi wanakwenda shule na sio vinginevyo maana bila wanafunzi kwenda shule Rais hawezi kunielewa nitakuwa sijatimiza malengo ya kutoa elimu bila malipo” alisema Masenza

Masenza alisema kuwa atachangia shilingi milioni moja kwa kila shule za sekondari za tarafa hiyo ambazo zipo kwenye ujenzi na shule hizo ni Ibumu na Nyanzwa ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma na kuwapunguzia umbali wa kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kuifuata shule.

“Naombeni tuzikamilishe shule hizi kwa wakati ili kuwapunguzia umbali wa kusoma watoto wetu haiwezekani wanafunzi hadi kuikuta shule moja ni umbali wa zaidi ya kilometa kumi na tatu ,jamani hawa ni watoto zetu na maisha yao yanategemea elimu hivyo ni lazima tuwekeze kwenye elimu” alisema Masenza

Masenza aliwataka viongozi wa vijiji kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofulu na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza wapelekwe shule kwa wakati na wazazi wote ambao hawajawapeleke shule watoto wao wachukuliwe hatua kwa kuwa Rais hataki kuskia kuwa mtoto hajaenda shule.

“Jamani Rais ameagiza kuwa wanafunzi wote wanatakiwa kuwa shule hata kama hawana sare za shule sasa huyo mzazi gani ambaye hatakiwa kuwa peleka shule naombeni kabla sijawakulia hatua nyinyi viongozi basi hakikisheni wanafunzi wote waliofaulu wanakwenda shule” alisema Masenza

Lakini mkuu wa mkoa alifanya ziara kwenye shule ya sekondari Kihesa manispaa ya Iringa na akatoa kiasi cha shilingi laki tano (500,000),shule ya sekondari  Ilambilole shilingi milioni moja(1,000,000) na shule ya msingi Matembo nako alitoa kiasi cha shilingi laki tano (500,000) pesa zote hizo ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya shule.

Aidha Masenza alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa mkoa wa Iringa kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.

“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Masenza

Sipia Kinyowa ni kaimu mtendaji wa kata ya Nyanzwa, Amidu Kilamba diwani wa kata ya Nyanzwa,Hemerd Wiliamu diwani wa kata ya Ibumu na Justine Mgina mtendaji wa kata ya Ibumu ni baadhi ya viongozi waliompungeza mkuu wa mkoa kwa ziara aliyoifanya ya kimaendeleo na kimkatikati kuhakikisha wanafunzi wote wanatakiwa kufika shule na kusoma bila kubuguziwa na mtu yeyeto.

“Leo tumefarijiaka sana kuona mkuu wetu kaja na mikakati hasa ya kusaidia kukuza maendeleo kwenye sekta ya elimu hivyo hatuna budi kumuunda mkono kuhakikisha kuwa mambo aliyoyaongea tunayafanyia kzi ili kuhikisha wanafunzi wanasoma” walisema vingozi

Comments