Featured Post

RAHMA, MASALU KUWAKILISHA VIJANA WA KITANZANIA ECOSOC 2018



Umoja wa Mataifa Tanzania wachagua vijana watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) 2018 jijini New York
Rahma Mwita Abdallah na Paschal Masalu wamechaguliwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) jijini New York. Wawili hao walichaguliwa kupitia shindano lililoendeshwa na Umoja wa Mataifa kupitia mitandao ya kijamii ambapo walitakiwa kupakia video ya dakika moja wakieleza kwanini wachaguliwe kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la ECOSOC.
Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) akiongea na vijana Rahma Mwita Abdallah na Paschal Masalu waliochaguliwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) jijini New York kabla ya kuwakabidhi bendera ya Tanzania na Umoja wa Mataifa.
Baraza hilo linakutanisha vijana viongozi kutoka ulimwenguni kwote kujiunga na waunda sera kujadili changamoto mbalimbali zinazowakumba vijana katika nchi wanazotoka na jinsi ya kuzitatua. Pia Mkutano huo unatoa fursa kwa vijana kutoka nchi balimbali kubadilishana ujuzi wa namna ya kutatua changamoto za vijana katika nchi zao.
Mkutano huo utafanyika kuanzia Jumatatu ya Januari 30 hadi 31 na unaweza kupata tarifa za safari ya Rahman na Paschal kwa kufuatilia akaunti za Umoja wa Mataifa katika Twitter @UnitedNationsTZ na Instagram @unitednationstz
Bw. Rodrguez akiwakabidhi vijana mfano wa hundi kama mchango wa Umoja wa Mataifa Tanzania ili kuwawezesha vijana hao kuhudhiria Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC).
Bw. Rodrigues akiwakabidhi Rahma na Paschal bendera za Tanzania na Umoja wa Mataifa kama utambulisho wao kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC).
Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez katika picha na Rahma pamoja na Paschal wakiwa wameshika bendera ya Umoja wa Mataifa Tayari kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC).

Comments