Featured Post

MAOMBI YA VIONGOZI WA DINI YALISAIDIA NCHI KUPATA RAIS MWENYE HOFU YA MUNGU

Askofu Mkuu wa Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre, Flaston Ndabila ambaye ndiye Mratibu wa maombi hayo akizungumza kwenye ibada ya maombi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Askofu Mkuu wa Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre, Flaston Ndabila, akimkaribisha Waziri wa HabariUtamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwenye ibada hiyo mara baada ya kuwasili.

 Waziri wa HabariUtamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati), akishiriki katika maombi ya shukurani na kuikabidhi Nchi kwa Mungu yaliyofanyika leo Nyumba ya Huduma Abundant Blessing Centre  (ABC) Tabata  jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa ABC,  na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama.
 Kwaya ya Haleluya Selebration wakitoa burudani ya nyimbo za kusifu katika ibada hiyo.
 Maombi yakifanyika.
 Mtumishi wa mungu, John Kanafunzi kutoka Kanisa la KLPT Mbezi Mwisho akiongoza kuimba nyimbo za kusifu.
 Watumishi wa Mungu  wakiwa kwenye maombi hayo. Kutoka kushoto ni Nabii Elijah Krasian Mollel kutoka Kanisa la Jehova Shammah na Askofu Mhina.
 Wachungaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Wanamaombi kutoka Kibaha mkoani Pwani wakiwa kwenye maombi hayo.
 Maombi yakiendelea.

Mmoja wa waombaji  Baba Askofu, David Mwasota akiongoza maombi ya shukurani.
 Taswira ndani wakati wa maombi hayo.
 Nabii Elijah Krasian Mollel kutoka Kanisa la Jehova Shammah, akifanya maombi.



Askofu Emanuel Mhina akiongoza maombi hayo.
Mtumishi wa Mungu akiomba katika ibada hiyo.
 Viongozi wa dini na waumini wakiwa kwenye maombi hayo.
 Utulivu wa viongozi wakati wimbo wa taifa ulipokuwa ukiimbwa.
Waziri Mwakyembe akizungumza na waumini wakati wa maombi hayo

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Habari Utamaduni, Sanaa  na Michezo,  Dk.Harrison Mwakyembe amesema maombi yaliyofanywa na viongozi wa dini wakati wa uchaguzi mkuu kuomba nchi ipate rais mwenye hofu ya Mungu ndiyo yaliyo mleta Rais Dk, John Magufuli.

Mwakyembe ameyasema hayo wakati wa maombi maalumu ya shukurani na kuikabidhi nchi kwa Mungu yaliyofanywa na maaskofu na viongozi wa dini kutoka makanisa mbalimbali katika Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre Tabata jijini Dar es Salaam leo.

"Maombi yenu ya kumuomba Mungu atupe rais mwenye hofu ya Mungu ndiyo yalisababisha kumpata Rais John Magufuli wakati wa uchaguzi mkuu ambaye anapigania maslahi ya wanyonge hasa maskini kwa kupambana na watu waliokuwa wakijineemesha wenyewe kwa kutumia fedha za umma vibaya" alisema Mwakyembe.

Alisema katika hatua nyingine Rais Magufuli ni rais pekee ambaye amekuwa akiwaomba viongozi wa dini wamuombee kwa kuwa anafahamu bila ya maombi hawezi kufanya chochote na maamuzi yake yote yanatokana na maombi ambayo anafanyiwa na viongozi wa dini.

"Serikali ina utambua mchango mkubwa mnaoufanya wa kumuombea Rais na nchi kwa ujumla hivyo mnapokuwa na malalamiko yenu msiyazungumzie chini chini tuelezeni tutayafanyia kazi kwa kushirikiana na viongozi wengine" alisema Mwakyembe.

Akizungumza katika ibada hiyo ya maombi ya kuliombea taifa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alisema serikali haitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayemsema rais vibaya wakati sasa anafanya mambo makubwa ya kuijenga nchi.

"Kuna baadhi ya watu wanamnenea vibaya rais wetu kutokana na kazi nzuri anayoifanya nasema hatutakubali kuona rais akifanyiwa hivyo mtu yeyote atakayebainika tutamkamata bila ya kumuonea huruma" alisema Mshama.

Askofu Mkuu wa Nyumba ya Huduma ya Abundant Blessing Centre, Flaston Ndabila ambaye ndiye mratibu wa maombi hayo alisema maombi hayo ya shukurani na kuikabidhi nchi kwa Mungu yameshirikisha viongozi wa makanisa mbalimbali na huduma za Kikristo na kuandaliwa na I GO Africa for Jesus Prayer Movement na kuwa maombi ya namna hiyo yamekuwa yakifanyika mara kwa mara.

Alisema maombi yaliyofanyika ni kumshukuru Mungu kwa ajili ya Uhuru wa Taifa letu ulipatikana pasipo kumwaga damu pamoja na ulinzi na neema na rehema katika nchi yetu.

Alitaja eneo lingine la maombi ni kumshukuru Mungu kwa ajili ya nchi yetu kuwa na utajiri na rasilimali nyingi kama dhahabu, almasi, uranium, mafuta ya petroli, ardhi nzuri, mbuga za wanyama, gesi, mito na milima.

Alisema maombi mengine yaliyofanyika ni kumshukuru Mungu kwa viongozi ambao wameliwezesha taifa kupiga hatua mbalimbali za maendeleo licha ya kuwepo changamoto kama za umaskini, maradhi na ujinga.

Askofu Ndabila alisema maombi mengine yalikuwa ni kuliombea Taifa, Kanisa na Afrika kwa ujumla.

Alisema anashangaa kuwasikia watu wakilalamika kuwa eti vyuma vimekaza wakati nchi ina kila rasilimali.

Maombi hayo yalihudhuriwa na maaskofu takriban tisa kutoka makanisa mbalimbali.



Comments