- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
ESRF IKISHIRIKIANA NA PROFESA JIN SANG LEE (KOREA KUSINI) IMEANDAA MHADHARA WA KUBADILISHANA UZOEFU KATIKA NYANZA ZA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU.
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Profesa Jin Sang LEE kutoka Chuo Kikuu cha New York – Korea (SUNY Korea) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) waliandaa mhadhara wa kubadilisha uzoefu ili kuweza kufikia malengo ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Mhadhara huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF na kufunguliwa na Mheshimiwa Anthony Mtaka – Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Akizungumza katika mhadhara huo, Mheshimiwa Mtaka alisema, nchi yetu imejipanga kufikia uchumi wa kati kwa kuwa na sera na mikakati mbalimbali. Aliongeza kwa kusema kilichobakia ni kuendelea kuitekeleza sera na mikakati hiyo ili kutimiza ndoto ya kuwa na uchumi wa kati.
Kwa upande wake, Dkt. Tausi Kida- Mkurugenzi Mtendaji ESRF alisema, mhadhara huo umekuja wakati muafaka kwa kuwa nchi yetu imedhamiria kufikia Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, ambapo sekta binafsi itakuwa injini ya ukuwaji wa uchumi.
Profesa Jin Sang LEE katika Mhadhara wake alianza kubadilishana uzoefu kwa kuelezea mapinduzi ya uchumi katika Korea ya kusini kuanzia miaka ya 1960. Alisema katika miaka hiyo Serikali ya Korea ya Kusini iliweka vipaumbele kadhaa ikiwamo kuondoa umaskini na kukuza viwanda. Katika miaka hiyo serikali ilijikita katika uchumi wa viwanda vidogo vidogo na wakijitahidi kuuza ndani na nje bidhaa ndogondogo. Katika miaka ya sabini Korea ilipiga hatua nyingine kwa kupanua techonoljia ili kuongeza tija katika viwanda vyake, Hayo yalikuwa yakifanywa kwa ushirikiano wa serikali na sekta binafsi.
Katika miaka ya themanini, nchi ilizidi kujikita katika sayansi, teknolojia na ubunifu, waliweza kuwafundisha watu wake ili kuwa na wataalamu wengi ambao watasaidia katika kubuni mambo muhimu ya maendeleo. Katika miaka ya tisini, Korea Kusini ilinza kujikita katika kujiimarisha katika teknolojia ambayo iliyohitajika kimataifa kama vile teknolojia ya Tehama. Na katika miaka ya 2000, nchi ilieweza kuwa na mapinduzi makubwa ya viwanda vya kubuni bidhaa mbalimbali kama vile simu za mikononi, komptuta, magari n.k.
Hayo yote ni matokeo ya uzalendo, kusomesha wataalamu, kuanzisha na kusimamia masuala ya utafiti na maendeleo, kufanyakazi kwa bidii kwa wananchi wa Korea Kusini. Masuala ya Utafiti na Maendeleo ni nguzo imara katika kuendesha sekta mbalimbali katika nchi. Alisisitiza pia , ushirikiano kati ya serikali na vyuo vikuu amboko ndio sehemu ambayo kutafumbuliwa na kukuzwa kwa sayansi, teknolojia na ubunifu.
Profesa Lee alisema katika upande wa viwanda Tanzania inatakiwa kuwa na viwanda vya msingi, masoko na kuwa na uelewa wa soko la kimataifa. Aidha kama taifa linatakiwa kuwa na nadharia zinazofaa kwa ajili ya kubeba mfumo huo wa viwanda kama
Pia vyuo vikuu vinatakiwa kutengeneza wataalamu wa ngazi za juu watakaoweza kusaidia sekta mtambuka kwenye masuala ya sayansi na teknolojia kufanyakazi.
Aidha ameshauri serikali kujenga uwezo wa viwanda nchini kwa kuviwezesha kushindana huku ikitilia maanani soko la ndani na nje.
Katika hilo inatakiwa kukuza ujasirimali kwa kuwezesha maarifa katika menejimenti, kujiamini na kutengeneza ushirika na makampuni ya kigeni
Aidha alihimiza uzalendo na kujitosa huku mtu akiwa na mawazo, maono na mikakati ya kusonga mbele huku utekelezaji wa mambo kuelekea katika ustawi wa viwanda ukiambatana na sera .
Profesa Lee aliyasema hayo katika warsha ambayo ilijadili mafanikio ya Korea Kusini katika viwanda na nini kinaweza kuigwa na watanzania kufikia uchumi wa kati mwaka 2025. Alikuwa akizungumza kama mgeni mwalikwa katika warsha iliyoshirkisha wataalamu mbalimbali nchini Tanzania kutoka serikali na sekta binafsi
Akizungumzia sekta binafsi alitaka, kuchukua pale ambapo serikali itakuwa imeishia katika kutengeneza mifumo ya kuwezesha uchumi mkubwa kwa kuwa na utaratibu wa kuwezesha sayansi, teknolojia katika kukuza shughuli zao.
Naye mtaalamu wa Maendeleo ya Sekta binafsi Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) Ernest Salla akizungumza wakati wa kufunga warsha hiyo alisema kwamba ipo haja ya watanzania kuwa wazalendo na kuhakikisha wanatimiza ndoto ya nchi ya viwanda kwa kuwekeza zaidi.
Aidha alisema kutokana na kuwapo kwa maendeleo makubwa ya teknolojia na sayansi Tanzania inaweza kutumia nafasi hiyo kusonga mbele kwa kasi kuelekea sekta ya viwanda
Alitaka kwa sasa sekta binafsi kuhakikisha inatumia fursa zilizopo kuleta maendeleo badala ya kuwa na woga na hofu kutokana na vikwazo vya hapa na pale.
Comments
Post a Comment