Featured Post

DC MJEMA, AKAGUA UKARABATI MAJENGO SHULE ZA JANGWANI NA AZANIA

Mkuu wa Shule ya Azania Erasto Gwimile akisoma taarifa ya hali ya ukarabati wa majengo ya shule, alisema ukarabati ulichelewa kukamilika kwa wakati hivyo kusababisha shule kuhelewa kufunguliwa.
 Mkuu wa wilaya ya Ilala Sopphia Mjema akipozi kwenye kitanda alipotembelea Shule ya sekondari ya Jangwani, kukagua maendeleo ya ukarabati wa majengo unaogharamiwa na serikali kwa maelekezo ya Rais Dk. John Maguduli katika shule hiyo na shule ya Azania, jijini Dar es Salaam, leo. DC Mjema alitumia kitanda hicho wakati akisoma katika shule hiyo miaka zaidi ya 30 iliyopita.
 Mkuu wa shule ya Jangwani Geradine Mwaisenga akimpokea DC Mjema kuka alipowasili kwenye shule hiyo. 
 Mkuu wa Shule ya Jangwani Geradine Mwaisenga akieleza taarifa ya hali ya ukarabati wa majengo ya shule hiyo ulipofikia sasa ambapo amesema umekamilika kwa kiasi cha asilimia 90. Kulia ni Katibu Tawala wa Ilala Edward Mpogolo na katikati DC Mjema
Ofisa wa Wakala wa majengo akimpatia maelezo DC Mjema kuhusu mradi huo wa ukarabati wa vyoo kwenye majengo ya shule ya jangwani. Kulia ni Edward Mpogolo
Moja ya vyoo vilivyokarabatiwa kwenye shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema (kushoto) akizunguma alipokuwa akikagua chumba cha darasa kilichokarabatiwa
Mwalimu wa somo la fizikia wa kidato cha nne Felix Sameli akifundisha darasani muda mfupi kabla ya DC Mjema kuingia katika darasa la kidato hicho.
DC Mjema (kulia) akisalimiana na wanafunzinwa Kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya Jangwani akiwa katika ziara hiyo ya kukagua maendeleo ya ukaranbati wa majengo
DC Mjengwa akiwa na mwanafunzi wa kidato hicho  sabrina Saidi ambaye alikuta anakaa kwenye dawati alilokuwa akitumia wakati wakisoma katika shule ya Jangwani zaidi ya miaka 30 iliyopita.
DC Mjema akiwaonya wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari ya Jangwani kutojiingiza katika mambo ya utukutu ikiwemo kupata mimba wakiwa bado masomoni na badala yake wazingatie masomo kwa bidii.
DC Mjema akiongozwa na Mkuu wa shule hiyo kukagua mabweni ya wasichana yaliyokarabatiwa.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sopphia Mjema akipozi kwenye kitanda alipotembelea Shule ya sekonari ya Jangwani, kukagua maendeleo ya ukarabati wa majengo unaogharamiwa na serikali kwa maelekezo ya Rais Dk. John Maguduli katika shule hiyo na shule ya Azania, jijini Dar es Salaam, leo. DC Mjema alitumia kitanda hicho wakati akisoma katika shule hiyo miaka zaidi ya 30 iliyopita.
DC Mjema akihoji jambo alipokagua vyoo ambavyo ukarabati wake unaendelea katika shule hiyo.
"Hivi hii milango metengenezwa kwa mbao aina gani?" DC Mjema akahoji alipokagua ukarabati wa vyoo katika shule hiyo.
DC Mjema akijaribu kuhakikisha kama maji yanatoka kwenye bafu alipokagua ukarabati wa vyoo kwenye eneo la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema akionyeshwa sehemu ya wanafunzi kulia chakula ambayo bado ukarabati wake haujakamilika katika shule hiyo ya Jangwani.
baadhi ya wanafunzi wenye uhitaji maalum wakiwa darasani katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjengwa na msafara wake wakitoka baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjengwa na msafara wake wakitoka baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali katika shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema kabla ya kuondoka akakagua ukarabati wa chumba cha maabara katika shule hiyo
"Sasa chumba kama hiki cha maabara kinatakiwa kuwa na umeme muda wote" akasema DC Mjema.
DC Mjema akisonga mbele na msafara wake.
Ofisa wa wakala wa Majengo akitoa maelezo ya mwisho kabla ya kuondoka DC Mjema kwenye shule hiyo ya Jangwani.
DC Mjema akizungumza na waandishi wa habari alichoshuhudia na maoni yake baada ya kukagua ukarabati wa majengo kwenye shule hiyo ya Jangwani. " Nimerishwa sana na ukarabati uliofanyika, Walimu, wafanyakazi wa kawaida na wanafunzi hakikisheni mnaitunza miundo mbinu hii ilivyokarabatiwa na kuwa mizuri. namshukuru na kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa uamuzi wake wa kuielekeza serikali kukarabati shule hizi" Alisema DC Mjengwa.
DC Mjengwa akizungumza na wanafunzi aliowakuta wakijisomea kwenye viwanja vya shule ya Jangwani wakati akienda shule ya Azania kuendelea na ukaguzi wa ukarabati wa majengo pia katika shule hiyo.
DC Mjema akizungumza na wanafunzi katika shule ya Azania.
DC Mjema akiongozwa na Mkuu wa Shue ya Azania Erasto Gwimile (kushoto), kwenda kukagua maeneo mbalimbali ya majengo yaliyofanyiwa ukarabati katika shule hiyo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (katikati) akiinama wakati wakienda kukagua ukarabati katika moja ya madarasa ya shule hiyo ya Azania.
DC Mjema akikagua vyoo vilivyokarabatiwa kwenye shue hiyo ya Azania.
DC Mjema akizungumza wakati akikagua mabweni katika shule hiyi=o ya Azania. Alishauri kuwekwa milango ya dharula kuwezesha wanafunzi kutoka kwa urahisi wakati wa majanga kama ya moto, badala ya kutegemea kutoka katka milango yenye vizuizi vingi kama mageti.
DC Mjema akimpa pole mwanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya Azania Enock Michael ambaye alimkuta amelala bwenini kutokana na kuwa na homa.
Mkuu wa shule ya Azania akitoa maelezo kuhusu ukarabati wa moja ya vyumba vya madarasa.
DC Mjema na msafara wake wakiendelea na ukaguzi
DC Mjema (kulia) akizungumza na baadhi ya walimu wa shule ya Azania aliowakuta wakifanya kazi zao nje kutokana na ofisi zao kuwa katika ukarabati.
DC Mjema akiwa katika chumba cha darasa kwa ajili ya kuzungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Azania. Kulia ni Edward Mpologo na kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Erasto Gwamile.
Wanafunzi wakiwa wamesimama kumlaki DC Mjema
Wakishangilia baada ya kuambiwa wakae.
DC Mjema akizungumza nao
Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi wa Azania Goodlove Kapufi akizungumzia ukarabati wa majengo ya shule yao. " kwa niaba ya wenzangu tunamshukuru sana Rais Dk Magufuli kwa kuelekeza ukarabati huu ufanyike, tunasema asante sana," alisema. Makamu huyo wa Rais.
Katibu Tawala wa Ilala akimsalimia Makamu huyo wa Rais wa Serikali ya Wafnafunzi wa shule ya Azania
DAS wa Ilala Mpogolo akiwa na Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Azania.
Mkuu wa Shule ya Azania akimshukuru DC Mjema kwa kutembelea shule yao
DC Mjema akizungumza na baadhi ya wanafunzi za shule ya zanaki wakati ameketi nao kwenye dawati

DC Mjema akiagana na Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Azania
DC Mjema akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi katika msafara wake na baadhi ya viongozi wa shule hiyo ya Azania kabla ya kuondoka mwishoni mwa ziara yake.
DC Mjema akiagana na Mkuu wa Shue ya Azania  Erasto Gwamile baada ya ziara yake ya kukagua ukarabati wa majengo katika shule hiyo leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Comments