Featured Post

UBALOZI WA KUWAIT WAKABIDHI VIFAA VYA WALEMAVU NA MISAADA MBALIMBALI MKOANI TABORA


Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kwa wenye Ulemavu, Ikupa Stela Alex na Mwenyekiti wa Taasisi ya Dkt. Amon Mkoga, Amon Mkoga (wa tatu kushoto) wakimkabidhi cherehani Shamsa Awadhi, mmoja wa mzazi wa mtoto mwenye ulemavu kutoka Mkoani Tabora kwa ajili ya kuisadia familia hiyo. Ubalozi wa Kuwaiti umetoa vyerehani, fimbo za kutembelea walemavu na baiskeli za walemavu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 18 kwa watu wenye mahitaji maalum kutoka mkoa wa Tabora. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)

 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kwa wenye Ulemavu, Ikupa Stela Alex akiomsikiliza mmoja wa mzazi mwenye mtoto mlemavu wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi ya vifaa mbalimbali kwa watu wenye ulemavu kutoka mkoani Tabora katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem. Ubalozi wa Kuwaiti umetoa vyerehani, fimbo za kutembelea walemavu na baiskeli za walemavu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 18 kwa watu wenye mahitaji maalum kutoka mkoa wa Tabora


Sehemu ya wanufaika wa msaada huo kutoka ubalozi wa Kuwait.

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem, akipeana mkono na Mwenyekiti wa Taasisi ya Dkt. Amon Mkoga, Amon Mkoga (kulia) wakati wa hafla ya kuwakabidhi vyerehani, fimbo za kutembelea walemavu na baiskeli vyenye thamani ya shilingi milioni 18 kwa watu wenye mahitaji maalum kutoka mkoa wa Tabora. Pamoja nao ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kwa wenye Ulemavu, Ikupa Stela Alex na baadhi ya wanufaika wa msaada huo.  

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kwa wenye Ulemavu, Ikupa Stela Alex na Mwenyekiti wa Taasisi ya Dkt. Amon Mkoga, Bwana Amon Mkoga wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi na watoto wenye ulemavu kutoka Mkoani Tabora wakati wa hafla hiyo. Ubalozi wa Kuwaiti umetoa vyerehani, fimbo za kutembelea walemavu na baiskeli za walemavu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 18 kwa watu wenye mahitaji maalum kutoka mkoa wa Tabora.


TAASISI YA DK. AMON MKOGA FOUNDATION YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA WATU WENYE ULEMAVU NA VIKUNDI VYA KINAMAMA WA MKOA WA TABORA KUTOKA UBALOZI WA KUWAIT TANZANIA:

Taasisi ya Dk. Amon Mkoga Foundation wamepokea msaada wa Vifaa vya watu wenye Ulemavu na Vikundi vya kinamama wa mkoa wa Tabora

-Wheel Chair Normal (Baiskeli za walemavu wakubwa)-15
-Wheel Chair For Infant (Baiskeli za walemavu wakubwa)-10
Crutches Elbow type pair (Fimbo za kutembelea)-10
-Crutches Elbow types pair (Fimbo za kutembelea)-10
-Walking stick brown (Fimbo za kutembelea )--10
-Stick for Blind (Fimbo za kutembelea vipofu)-20
-Spectacles for Blind people (Miwani ya jua kwa Albino)-15
-Sewing machines (kwa Walemavu na Wajane)-30


Katika Muendelezo wake Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Jasem Al Najem katika kusaidia watu wenye ulemavu na mahitaji maalumu.

Kwa muda mrefu tumekuwakuwa tukishuhudia Ubalozi wa Kuwait ukisaidia makundi maalumu hapa nchini,hii itakuwa fursa kwa watu wenye ulemavu na vikundi mbalimbali vya kinamama kufaidika na mradi huu.

Kwanini msaada huu?kumekuwepo walemavu wengi wasiona uwezo wa kununu vifaa mbalimbali vya kuwasaidia hivyo kudumaza utendaji wao wa kazi,wajane pia watafaidika na msaada huu wa cherehani kwani migogoro ya ndoa  na vifo vya wenza imesababisha ongezeko la wajane katika siku za hivi karibuni.

Misaada hii italenga walengwa kutoka vijijini ambao hawana uwezo wa kununua vifaa hivi,baadhi ya Kata za Tabora ambazo wafaidika watatoka ni-

  • Chemchem
  • Cheyo
  • Gongoni
  • Ifucha
  • Ikomwa
  • Ipuli
  • Isevya
  • Itetemia
  • Itonjanda
  • Kabila
  • Kakola
  • Kalunde
  • Kanyenye
  • Kiloleni
  • Kitete
  • Malolo
  • Mbugani
  • Misha
  • Mtendeni
  • Ndevelwa
  • Ng`ambo
  • Ntalikwa
  • Tambukareli
  • Tumbi
  • Uyui


Tunashukuru mgeni Rasmi; Mhe. Stella Ikupa Naibu waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu kuja kushiriki nasi leo katika makabidhiano haya.


Waweza tembelea Tovuti yetu : www.dramonmkogafoundation.or.tz

Comments