Featured Post

NJIA SALAMA ZAIDI YA KUTUMIA INTANETI UKIWA MAJUMBANI NA MAKAZINI

Wateja na wapenzi wa 4G nchini Tanzania wamekuwa wakifurahia intaneti yenye kasi na muda zaidi, kitu ambacho kwa kiasi kikubwa kimewashawishi wafanyabiashara na wananchi, hasa wazazi na wamiliki wa nyumba wenye bajeti ndogo kutumia mtandao huo ni baada ya Smile Communications Tanzania kupunguza bei na kuongeza thamani kwenye vifurushi vyake vya internet.

Ingawa matumizi ya intaneti yamerahisishwa sana, hasa kupitia teknolojia ya 4G, bado kumekua na uhitaji mkubwa wa usalama pindi wateja wanapokuwa mitandaoni. Wateja wengi hasa wafanyabiashara na wazazi wamekua wakijiuliza ni kwa jinsi gani watoto na waajiriwa wao wataweza kutumia intaneti kwa manufaa na si vinginevyo. Kutokana na wasiwasi huo Smile Tanzania ikawaletea watanzania uwezo wa kudhibiti matumizi ya vifaa vyao hata kupitia kwa simu zao za mkononi, suluhisho ambalo limepokelewa vyema sana na wapenzi wa mtandao wa 4G nchin Tanzania, hasa wale wanaojali usalama wa watoto wao na wafanyakazi wao pindi wawapo mtandaoni.

Wateja wa Smile sasa wanaweza kutumia akaunti zao za "MySmile" kudhibiti matumizi ya vifaa vyao kadri wanavyopenda, ikiwapa nguvu za kufanya mengi kupitia vipengele vilivyoongezwa. Baadhi ya vipengele vilivyopatikana kwenye MySmile Portal ni kama ilivyoorodheshwa hapa chini.

Historia na Grafu ya Matumizi: Hii inaruhusu mtumiaji kufuatilia matumizi yake ya kila siku na shughuli zilizofanywa kutoka kwa akaunti yake ya MySmile

Uwezo wa kudhibiti line na vifaa zaidi ya kimoja kwa Akaunti moja tu: Kipengele hiki kinawawezesha wateja wa Smile kuwa na udhibiti wa vifaa vyao vyote kwa kutumia akaunti moja tu

Nguvu ya kudhibiti matumizi ya vifurushi kwa kudhibiti vipengele: Baadhi ya vipengele ni downloads za automatic – unazoweza kuzizuia kwa kuingia tu na kuchagua "Manage my data usage ".

Mteja wa Smile anaweza pia kuzuia Uhifadhi wa Cloud, Torrent na Video kupitia MySmile kitu kitakachompa matumizi rahisi zaidi ya vifurushi, hususan unaposhea mtandao (wireless) na watumiaji wengi kwa kuunganisha na vifaa vyao kupitia Wi-Fi kwenye Router moja au MiFi.

Kupitia MySmile Pia mteja anaweza kudhibiti kasi ya vifurushi vyake wakati wote: Ni kweli! Ingawa Smile inakupa kasi kubwa Zaidi ya 4G nchini Tanzania, mteja ana chaguo la kutumia kikamilifu au kuipunguza kasi ya mtandao kadri apendavyo. UKIWA NA SMILE PEKEE!

Kuna faida nyingi ambazo wapenzi wa mtandao wa 4G na wateja wa Smile wanaweza kufurahia kila siku kupitia vifurushi vya Smile 4G. Zaidi ya hayo, Smile pia hupendekeza njia rahisi ambazo zinaweza kusaidia wateja wao kuona jinsi vifurushi vyao vinatumiwa. Mawakala wa Smile Huduma kwa wateja wako tayari kutoa ushauri juu ya jinsi ya kuepuka matumizi yoyote yasiyotakiwa. Tafadhali wasiliana na 0662 100 100 kwa maelezo zaidi au, kwa njia ya barua pepe customercare@smile.co.tz

Comments