Featured Post

MATENGENEO MAKUBWA MASHINE NAMBA MOJA YA KUFUA UMEME KIDATU YAFIKIA ZAIDI YA ASILIMIA 95 KUKAMILIKA

 Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), wakishirikiana na wakandarasi kutoka kampuni ya Concar kutoka Croatia, wakifanya matengenezo makubwa ya mashine namba moja ya kufua umeme, kwenye Kituo cha kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro Desemba 22, 2017. Kituo hicho kina jumla ya mashine 4 (Turbines) za kufua umeme wa Megawati 204.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Kidatu
MATENGENEZO makubwa ya mashine namba moja kati ya nne za kufua umeme wa maji kwenye Kituo cha kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro yamefikia zaidi ya asilimia 95 kukamilika.
Msimamizi wa matengenezo ya mashine hiyo Mhandisi Rajabu Kindunda amewaambia wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea kituo hicho Desemba 22, 2017.
"Kwa sasa tumeanza majaribio ya mashine kuzunguka bila kutumia nguvu za maji, mafundi wanazungusha mashine hiyo kwa kutumia mikono ili kuangalia usahihi wa unyookaji wa shafti,”alisema
Alisema hatua itakayofuata ni kuunganisha kipande yanapoingilia maji ili kuzungusha huo mtambo na sehemu ya kuzalishia umeme na Jumapili mafundi hao wanaoshirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya Concar kutoka Croatia wataanza majaribio ya kuzungusha mtambo wenyewe.
Aidha Meneja wa Kituo hicho, Mhandisi Anthony Mbushi Amesema Kidatu kuna mitambo minne na kila mmoja unauwezo wa kuzalisha umeme Megawati 51 na hivyo kufanya jumla ya Megawati 204 za umeme ambao unaingizwa kwenye Gridi ya Taifa.
”Tuliona tufanye matengenezo makubwa kwani kila baada ya miaka 20 huwa tunafanya zoezi kama hili ili kurejesha mashine kufanya kazi bora kwa kipindi hicho ili kuhakikisha mtambo unarejea kwenye hali yake ya kawaida.” Alisema.
Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme (Power Generation), Mhandisi Abdallah Ikwasa, alisema, umeme unaozalishwa kutokana na maji ni wa bei nafuu na kupongeza juhudi za serikali katioka kuhakikisha wananchi wanatunza mazingira ili kutunza vyanzo vya maji ambayo hutumika kuzalisha umeme.
“Tunaishukuru sana serikali kwa hatua inazochukua kama kuboresha upatikanaji wa maji kwa kutunza vyanzo vya maji (mazingira), hususan bonde la Mto Rufiji, timu iliyoundwa na Makamu wa Rais ambayo imefanya kazi nzuri nahuenda baada ya muda matokeo mazuri tutayaona.” Alisema.
Akifafanua zaidi alisema, juhudi zinazofanywa na serikali kuongeza vyanzo vya kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo vya maji kama vile Stigler Gorge zitasaidia sana nchi yetu na hii inaonyesha serikali ilivyodhamiria kupunguza gharama za umeme kwa wananchi kwa vitendo.” Alisema.
Kwa upande wake, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO Bi. Leila Muhaji, amesema Shirika limekuwa karibu na wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji na vituo vya umeme ili kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kutunza mazingira ili kunusuru vyanzo vya maji.
“Na ushirikiano wetu na wananchi uko katika maeneo mbalimbali kama vile kutoa huduma za afya bure kwa wananchi wanaoishi jirani na vituo vyetu vya kufua umeme, shule za awali lakini pia hata usafiri yumekuwa tukiwapatia usafiri wa bure wananchi ambapo hutumia magari yetu ya wafanyakazi kwenda maeneo jirani na vituo.

Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine turbines kwenye bwawa la Kidatu mkoani Morogoro
 Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine za kufua umeme wa maji Kidatu.
  Geti la kuruhusu maji kuelekea kwenye mashine za kufua umeme wa maji Kidatu.
 Mhandisi Abdallah Ikwasa, (kulia), akizungumza kuhusu kituo cha kufua umeme wa maji Kidatu, mkoani Morogoro. Katikati ni Meneja wa Kituo hicho, Mhandisi Anthony Mbushi na kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji.
 Mhandisi Ikwasa, (kulia), akibadilishana mawazo na Afisa Mazingira wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bw. Yusuf Kamote.
 Geti la kupitishioa maji Kidatu.
 Meneja wa Kituo cha kufua umeme Kidatu mkoani Morogoro, Mhandsi Anthony Mbushi (kushoto), akifafanua masuala ya kiufundi kwenye chumba cha udhibiti umeme kilichoko chini ya ardhi kwenye Kituo cha Kidatu mkoani Morogoro.
 Maafisa wa TANESCO na baadhi ya wahariri wakiangalia mashine iliyoharibika, a,mbayo kwa sasa iko kwenye matengenezo makubwa.
Wasimamizi wa chumba cha kudhibiti mifumo ya umeme wakiwa kazini wakati walipotembelewa na wahariri wa vyombo vya habari Kituo cha Kidatu mkoani Morogoro.
Peter Rauya, (kushoto) na Senorina Maganga  wa chumba cha udhibiti mifumo ya umeme wakiwa kazini.
Wahariri wakipatiwa maelezo na maafisa wa TANESCO kuhusu utendaji kazi wa mashine za kufua umeme (Turbines) kituom cha Kidatu.
Waharorio wakiangalia mashine iliyoharibika ambayo sasa iko kwenye matengenezo makubwa.
Mameneja wa vituo vya kufua umeme kutoka mikoani wakiwa kwenye kituo cha kufua unmeme Kidatu mkoani Morogoro. Mameneja hao kwa sasa wako katika kikao kazi hapo Kidatu.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (wapili kushoto), akiwa na baadhi ya Mameneja wa vituo vya kufua umeme vilivyoko mikoani ambao kwa sasa wako katika kikao kazi hapo Kidatu.
Mhandisi Ikwasa, akijadiliana na maafisa wake.
Mhandisi Ikwasa, akijadiliana na maafisa wake.
Wasimamizi wa chomba cha udhibiti mifumo ya umeme cha Kidatu mkoani Morogoro; kutoka kushoto ni Peter Rauya, Senorina Maganga na Nicomedy Mhina.
Msimamizi wa matengenezo ya mashine hiyo Mhandisi Rajabu Kindunda (kushoto), akiwa sambamba na wakandarasi kutoka kampuni ya Concar ya Croatia wakati wakiendelea na matengenezo hayo.
Sehemu ya kuingilia "mgodini" chini ya ardhi kwenye mitambo ya kufua umeme wa maji Kidatu mkoani Morogoro.

Comments