Featured Post

BIDHAA ZA SUGAR FREE NI MKOMBOZI KWA KUPUNGUZA MATUMIZI MAKUBWA YA SUKARI KATIKA JAMII

Na Dotto Mwaibale

BIDHAA za Sugar Free ambazo zimezinduliwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ni mkombozi mkubwa kwa jamii hasa katika kukabiliana na matumizi makubwa ya sukari kwenye vyakula.

Sugar free tayari zimeanza kushika soko nchini Tanzania zinaingizwa hapa nchini na kusambazwa na Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD kwa kupitia maofisa masoko wake waliobobea kwa usambazaji na kuzielezea kwa kina bidhaa hizo kwa wananchi.

Kwa kuzisogeza bidhaa hizo karibu na wananchi tayari Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD imezindua bidhaa hizo na kupokelewa kwa mikono miwili na wadau mbalimbali waliokuwepo kwenye uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam wiki iliyopita katika Hoteli ya Best Western.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu alisema bidhaa hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi makubwa ya sukari katika vyakula. 


Alisema bidhaa hizo zimetengenezwa mahususi ili kukabiliana na ongezeko la sukari mwilini na hivi sasa zinapatikana kwa bei ya chini katika soko la nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi na kuwa bei hizo zipo kuanzia shilingi,4200, 4,500, 5,700, 8,850 na za bei ya juu ni shilingi 13,000 na kuwa zinategemea bidhaa husika.


"Bidhaa hizi zipo za aina mbili za sugar free gold  ambazo hutumika katika chai, uji, na vinywaji baridi tu  na sugar free natura hutumika katika baking, kupikia vyakula vinavyohitaji sukari katika upishi na pia hutumika katika chai, uji na vinywaji baridi na matumizi yake ni rahisi sana," alisema Babu.


Alisema kwa Tanzania bidhaa hizo zimeanza kuchukua soko kubwa baada ya wananchi kuona umuhimu wake na hivyo wanategemea muitikio utaendelea kuwa mkubwa.


Aliongeza kuwa, lengo kubwa la kampuni hiyo kusambaza bidhaa hizo ni kusaidia jamii kuelewa matumizi ya bidhaa hizo ambazo hazina sukari ingawa zina ladha ya sukari kama ile ya kawaida  na kwamba bidhaa hizo zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Akizungumza katika uzinduzi huo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga alisema ugonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa kwani Tanzania ni nchi ya tano Barani Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi.


Alisema hali hiyo inatokana na watu wengi hasa vijijini kutojijua mapema kama wameathiriwa na ugonjwa huo ambapo baadhi yao huanza kugundua baada ya kupata upofu, kukatwa miguu na kadhalika. (Kwa maelezo zaidi kuhusu bidhaa hizo piga simu namba 0784834010)

Aliongeza kuwa, matibabu ya mgonjwa mmoja wa kisukari yanafikia asilimia 25 ya pato la familia fedha ambazo ni nyingi jambo linalowafanya wauguzaji kukata tamaa ya kumtibu mgonjwa na kuamua fedha hizo kuzielekeza katika matumizi mengine.

Dk.Chiwanga alitoa mwito kwa kusema ni vizuri kuzuia kupata kisukari kuliko kutibu.

Akizungumzia bidhaa za sugar free alisema hazitibu ugonjwa wa kisukari isipo kuwa zinamsaidia mgonjwa au mtu mwenye kisukari anapokula vyakula vingine visivyo na sukari kupata radha ile ile.


Alisema mtu mwenye ugonjwa wa kisukari hatakiwi kabisa kuvuta sigara ingawa vitu vingine kama vinywaji na pombe anatakiwa kutumia kwa uangalifu.

Comments