- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog
KIZAZI cha sasa cha muziki hakiwezi kuelewa, lakini ukweli
ni kwamba, bendi iliyojipatia umaarufu katika ukanda wa Afrika Mashariki, Simba
Wanyika, awali ilijulikana kama Arusha Jazz kabla ya kubadili jina.
Historia ni mwalimu mzuri, nami napenda historia, hivyo
nitawamegea kidogo.
Wakati wanandugu Wilson na George Peter Kinyonga
walipoachana na bendi ya Jamhuri Jazz ya Tanga walikwenda Arusha ambako
walianzisha bendi hiyo ya Arusha Jazz mwaka 1971, wakiwa na ndugu yao mwingine
William Peter Kinyonga.
Ukiangalia kwenye albamu
ya Simba Wanyika Greatest Hits
Vol. 1, nyimbo kadhaa ambazo zimerekodiwa humo kwa jina la bendi ya Simba
Wanyika, kama "Pamela,"
"Kenya Yetu," na "Marceline,"
awali zilikuwa zimerekodiwa chini ya jina la Arusha Jazz.
Sasa ilikuwaje hata wakajiita Simba Wanyika?
Mnamo mwezi Juni 1971, bendi hiyo ya Arusha Jazz iliyoundwa
na wanandgu watatu ilihamia mjini Mombasa, Kenya na ikajipachika jina la utani
wakijiita wao ni “Simba Wanyika” (Lions
of the Wilderness).
Lakini huo haukuwa mwisho wa jina la "Arusha Jazz".
Mwandishi mashuhuri wa masuala ya muziki wa Afrika, Peter
Toll, anasema, "Simba Wanyika ni jina ambalo wanandugu wa familia ya Kinyonga
waliamua kulitumia baada ya kutoka Arusha na kuhamia Mombasa mwaka 1971 lakini
waliendelea kulitumia jina la Arusha Jazz kwa muda.
“George alisema kwamba wakati walipoanza maisha mjini Mombasa
walikuwa wakitumia mabango mawili kwenye maonyesho yao, moja likiwa na jina la 'Simba
Wanyika,' na jingine 'Arusha Jazz.' Hata hivyo, inaonekana kwamba kuanzia mwaka
1973 waliamua kuachana kabisa na ‘Arusha Jazz’ na kutumia jjina la Simba
Wanyika."
Long Player za mapema kabisa za bendi ya Arusha Jazz
mwanzoni mwa miaka ya 1970 ni pamoja na Mama
Suzie / Mary Mtoto (7" 45; Polydor POL 185); Tutengane Salama / Mama Niache (7" 45; Polydor POL 186); Eliza Wangu b/w Jose Twende Zaire
(7" 45; Polydor POL 187) ilirekodiwa mwaka 1973.
Mnamo mwaka 1987, Wilson Peter Kinyonga alirekodia albamu akiishirikisha
Arusha Jazz kwa kurekodi upya nyimbo za mwaka 1973 iliyokwenda kwa jina la Mama Suzie (Cassette; ASL [Nairobi]
CASLP 2009).
Albamu hiyo iliyokuwa kwenye kaseti ilikuwa na nyimbo za Mama Suzie, Mary Mama, Bado Nakupenda, Eliza
Wangu na Jose Twende Zaire.
Nyimbo nyingine zilikuwa Kwaheri
Mpenzi, Sela Mbaa-Mbaa, Usinelewe Vibaya, Mbaya Wako Rafikiyo na Ewe Kijana.
Naamini tuko pamoja. Endelea kuperuzi MaendeleoVijijini
ili kujua mengi zaidi.
Imeandaliwa na www.maendeleovijijini.blogspot.com.
Simu: +255 656 331974.
Comments
Post a Comment