Featured Post

RUGE ASEMA ANAMHESHIMU MAMA WATOTO WAKE ZAMARADI MKETEMA

Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba leo amemzungumzia Zamaradi Mketema ambaye alikuwa mpenzi wake, mahusiano yao yaliweza kudumu kwa muda kiasi cha kutoa matunda ya watoto wawili (2) kwa mujibu wa maelezo ya Ruge.

Akiwa kwenye mahojiano Clouds TV kupitia kipindi cha asubuhi CLOUDS 360 Ruge amefunguka kama ifuatavyo baada ya kuulizwa  maswali yafuatayo: 1. Je ulikuwa unajua kama Zamaradi anaelekea kufunga ndoa? 2. Ile sauti ni ya kwako?

RUGE: "Kila kilichofanyika nilikuwa na taarifa nacho na ninakipa baraka asilimia mia moja 100%,  kwa sababu hii ni sehemu ya maisha tunapita.  Kubwa kuliko yote nina watoto wawili (2) ambao nimezaa na Zamaradi Mketema namuheshimu mno mpaka sasa naendelea kumheshimu kama Mama watoto wangu. Naheshimu na kuwapenda sana watoto wangu na nimewaona weekend iliyopita so heshima inatakiwa iwepo".   (Mwandishi Victor Petro)

Comments