Featured Post

MHANDISI MTIGUMWE ATEMBELEA CHUO CHA KILIMO KILIMANJARO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisisitiza jambo wakati akizungumza na Baadhi ya watumishi wa Chuo cha Kilimo Kilimanjaro (Kilimanjaro Agricultural Training Center (KATC) kilichopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akizungumza na Baadhi ya watumishi wa Chuo cha Kilimo Kilimanjaro (Kilimanjaro Agricultural Training Center (KATC) kilichopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe (Katikati) akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuwasili Chuo cha Kilimo Kilimanjaro (Kilimanjaro Agricultural Training Center (KATC), Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bi Hilda Kinanga (Kushoto) na Mkuu wa Chuo cha KATC Ndg Dominick Onesmo Nkollo.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bi Hilda Kinanga akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuwasili Chuo cha Kilimo Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisindikizwa na wenyeji wake Mara baada ya kumaliza Kikao kazi katika Chuo cha Kilimo Kilimanjaro.

Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe leo Novemba 11, 2017 ametembelea Chuo cha Kilimo Kilimanjaro (Kilimanjaro Agricultural Training Center (KATC) kilichopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Katika ziara hiyo ya Kikazi Katibu Mkuu amefanya kikao na wafanyakazi ili kubaini Changamoto zinazokikabili chuo hicho na kutafuta namna ya kuzitatua.

Chuo hicho kilichoanza rasmi Julai 1, 1994 kutokana na hitaji la Taifa la kusambaza mafanikio ya mradi wa Lower Moshi kwenda kwenye sehemu zote za nchi.

Katibu Mkuu Mhandisi Mtigumwe ameutaka uongozi wa Chuo hicho kuongeza idadi ya wanafunzi wanaohitimu kwani ni maafisa Ugani 308 pekee ambao wamehitimu tangu Mwaka 2007 wakiwemo Astashahada 85 na Stashahada 223 sawa na wastani wa asilimia 30 kwa Mwaka.

Alisema idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha na mahitaji ya Wataalamu wa Kilimo katika Kata na Vijiji mbalimbali kote nchini.

Chuo hicho cha Kilimo Kilimanjaro kinafundisha kozi za (Astashahada na Stashahada) na kozi fupi (Wakulima na Maafisa Ugani).

Aidha, Mwaka 2007 Taifa lilikuwa na uhitaji mkubwa wa kuzalisha maafisa Ugani ili kujaza pengo lililokuwepo kwenye vijiji vingi ndipo KATC ilitakiwa kutoa mafunzo ya kozi ndefu kufundisha Astashahada na Stashahada.

Comments