Featured Post

COBRA: NYOKA HATARI MWENYE SUMU KALI

NYOKA ameorodheshwa katika kundi la viumbe 10 hatari kwa maisha ya binadamu kutokana na kuwa na sumu kali inayoweza kuua katika muda mfupi, au kuleta madhara makubwa.

Viumbe kama Simba, Tembo, Nge, Jerry Fish, Kiboko, Nyati na Mamba japo kwa kuvitaja vichache, ni miongoni mwa hivyo hatari kwa mujibu wa wataalam wanaofuatilia kwa ukaribu wa binadamu na viumbe hai wengine.
Hata hivyo, si nyoka wote walio hatari kwa binadamu isipokuwa baadhi yao tu akiwemo nyoka aina ya Cobra, ambaye anapatikana sehemu nyingi duniani, lakini zaidi katika ukanda wa Bahari ya Hindi, Pacific na Jangwa la Sahara.
Cobra ana tabia ya kupenda kujificha, na mara nyingi huwa hapendi kuonekana kwenye maeneo wanayoishi zaidi watu.
Watafiti wanasema kuwa, tabia zake za kutopenda kuonana na watu au kuishi kwenye mazingira kama hayo, ni kutokana na kutambua kwamba binadamu ni adui yake mkubwa.
Kimaumbile Cobra wako wa aina nyingi hali inayowafanya kutofautiana kimaumbo, tabia, mazingira ya kuishi na umri pia.
Hata hivyo, Cobra mrefu zaidi anaweza kufika urefu wa futi sita au zaidi.
Ana uwezo wa kutambaa kwa kasi iwe kwenye mchanga au majani, kusimamisha kichwa juu na kurusha mate mwendo mrefu.
Anakula vitu vingi, lakini hupendelea zaidi ndege na jamii nyingine ya viumbe vinavyotambaa wakiwemo mijusi mikubwa, na wanyama kama panya, nguchiro na sungura.
Lakini pia Cobra wakati mwingine hula nyoka ambao ni jamii yao.
Cobra anayependa zaidi kula nyoka wenzake ni Yule anayejulikana kama King Cobra (Koboko), ambaye anaelezwa kwamba ni mkali na anaweza kumfukuza adui yake iwapo atakorofishwa.
Nyoka aina ya Koboko (King Cobra) akimmeza nyoka aina ya Moma.
Hakuna ushahidi kama kuna Cobra mkubwa anayeweza kummeza binadamu kama walivyo nyoka wa aina nyingine kama Chatu na Anaconda wanaopatikana zaidi katika Bara la Amerika hasa kwenye Misitu ya Amazon.
Kwa kwaida, Cobra huwinda chakula chake kwa kuvizia, ambapo akishakamata sumu yake kali inaua kwa haraka kiumbe na kuanza kumeza taratibu. Akishashiba hupenda kwenye kujificha sehemu yenye utulivu.
Sumu ya Cobra inapoingia mwilini mwa kiumbe alichokimata huenda kuharibu chembe uhai mwilini ambazo nazo ambazo nazo baada ya kushambuliwa hushindwa kulinda mfumo wa mawasiliano na kusababisha misuli kukosa nguvu.
Misuli inapokosa nguvu maana yake pia kiumbe kilichoshambuliwa kinakosa uwezo wa kujihami na hivyo kulegea.
Hata hivyo, si Cobra wote wanaouma wana sumu kali, lakini baadhi yao ambao kwa jina la kitaalam wanajulikana kama ‘Dry Bites’ hawa ni hatari zaidi kwa vile sumu kidogo tu inaweza kusababisha madhara makubwa.
Uchunguzi unaonyesha kuwa, mate ya Cobra wakati mwingine huwa na bacteria wanaoweza kuwa hatari kama wataingia kwenye mzunguko wa damu ya mtu baada ya kugongwa.
Inaelezwa kuwa, asilimia 75 ya watu waliowahi kugongwa na nyoka wa aina hii hufa kutokana na athari za dawa ambazo hutumia baada ya kushambuliwa kwa vile sumu ya nyoka huyo inapokuwa na dawa huleta athari zaidi.
Kijiografia, nyoka aina ya Cobra hupatikana zaidi pia Afrika hasa kwenye Ukanda wa Jangwa.
Wana uwezo wa kutaga mayai kati ya 20 hadi 40 kutegemeana na hali ya hewa katika eneo husika.
Cobra jike hutaga mayai hayo wiki tisa baada ya kupandwa na nyoka dume ambao kimaumbile ni wadogo kulinganisha na majike.
Baada ya mayai kutagwa huchukua takriban miezi miwili na zaidi kidogo kabla ya kuanguliwa.
Ni hatari kudharau nyoka mdogo aina ya Cobra kwani punde wanapoanguliwa tayari wanakuwa na uwezo wa kuuma na kuleta madhara.
Cobra wanapenda zaidi kujificha katika maeneo yanayofanana na rangi ya ngozi yao ili iwe vigumu kugundulika na maadui zao au mawindo yao.
Kuna baadhi ya Cobra wana uwezo wa kujilinda kupitia mate hasa wanapokabiliwa na shambulizi kutoka kwa viumbe wengine.
Kwa baadhi ya viumbe wanavyovitemea mate vinaweza kufa, hayana uwezo wa kuua mtu zaidi ya kuleta madhara makubwa ikiwa ni pamoja na upofu au kovu kama matibabu hayatafanyika haraka.
Imeandaliwa na www.maendeleovijijini.blogspot.com. Simu: +255 656331974.


Comments