Featured Post

WAKULIMA WASHAURIWA KUJIUNGA NA BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO


 Afisa mahusiano Mkuu katika Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) Ndg Saidi Mkabakuli (Kushoto) akimkabidhi baadhi ya vipeperushi Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe (Kulia) wakati alipotembelea banda la Benki hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa katika viwanja vya kalangalala Mkoani Geita.

Meneja Mwendeshaji wakulima wadogo katika Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) Ndg Joseph Mabula (Kulia) akitoa maelezo ya namna wanavyofanya kazi mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe (Kushoto) wakati alipotembelea banda la Benki hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa katika viwanja vya kalangalala Mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe akisikiliza maelezo kutoka kwa afisa wa shirika la chakula Duniani (FAO) na Programu ya Chakula duniani (WFP) wakati alipotembelea banda la shirika hilo kwenye maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa katika viwanja vya kalangalala Mkoani Geita
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe akisikiliza maelezo kutoka kwa Msaidizi wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania Bi Eveline Massam wakati alipotembelea banda la shirika hilo kwenye maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa katika viwanja vya kalangalala Mkoani Geita


Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa Utafiti katika Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania  wakati alipotembelea banda la shirika hilo kwenye maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika viwanja vya Kalangalala Mkoani Geita

Na Mathias Canal, Geita

Wakulima kote nchini wameshauriwa kujiunga na Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) ili kuongeza Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo kwa kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini kwa wakulima nchini.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe wakati alipotembelea banda la Benki hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanataraji kufika ukomo Kesho Octoba 16, 2017 kwenye viwanja vya kalangalala Mkoani Geita.

Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha za mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka Taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa, riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo, Mikopo ya muda mfupi, masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Alisema kuwa kupitia changamoto hizo serikali imeamua kuanzisha Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika kilimo nchini.

Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa miongoni mwa madhumuni makubwa ya kuanzishwa kwa Benki hiyo ni pamoja na kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini pamoja na kuchagiza na kusaidia mapinduzi ya kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini.

Kwa upande wake Meneja Mwendeshaji wakulima wadogo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Ndg Joseph Mabula alisema kuwa pamoja na mambo mengine pia Benki hiyo imedhamiria na kujidhatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta Mapinduzi yenye tija katika sekta ya kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja na sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.

Mabula aliongeza kuwa malengo mkakati ya Benki hiyo ni kuinua uzalishaji wenye tija katika sekta ya kilimo kwa kuendeleza miundombinu muhimu, mathalani, Skimu za umwagiliaji, Usafirishaji, Hifadhi ya Mazao, Usindikaji na Masoko.

TADB imejipanga kutoa mikopo ya kilimo katika makundi matatu ambayo ni Mikopo ya muda mfupI, Mikopo ya muda wa kati na Mikopo ya muda mrefu kwa kutumia njia mbalimbali zinazojumuisha pamoja na mambo mengine; Mikopo ya moja kwa moja kwa vikundi vya wakulima wadogo wadogo.

MWISHO

Comments