- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
MAAMBUKIZI ya bacteria katika ngozi ya sungura kitaalam huitwa pyoderma.
Mara
nyingi maambukizi haya hutokea wakati ngozi ya sungura inapochanika, au wakati
ngozi inapokuwa wazi hasa katika mazingira ya unyevu nyevu, hivyo kuathiri hali
ya kinga iliyomo ndani.
Kwa
kawaida, bacteria wa afya hupatikana katika ngozi ya sungura na hasa katika ute
wa juu.
Hata
hivyo, wakati mwingine hali hiyo inaweza kuathiriwa na kuruhusu bacteria wabaya
kumea humo na kuleta madhara.
Dalili
Dalili
nyingi za pyoderma hutegemea na aina ya maambukizi ya bacteria
kwa sungura, lakini baadhi ya dalili ambazo aghalabu huonekana ni pamoja na:
* Kunenepeana hovyo
* Kuhara damu
* Maumivu ya misuli
* Kutokwa na majimaji puani (na mara chache kwenye macho)
* Maambukizi ya njia ya mkojo
* Hali ya uchafu
* Kukunjamana kwa manyoya (hasa katika sehemu ya haja kubwa,
mapaja na tumboni)
* Wekundu katika eneo lililoambukizwa
* Ugonjwa wa meno (kuvimba kwa fizi na kuoza kwa meno).
Chanzo
Kwa
kawaida maambukizi ya bacteria kwenye ngozi hutokea wakati ngozi ya sungura
inapokuwa imechanika, mara nyingi hutokea wakati ngozi hiyo inapokuwa wazi
katika mazingira duni, yakiwemo ya unyevu.
Inaweza
kutokea pia wakati anapokuwa na majeraha au msukumo dhaifu wa damu mwilini.
Pyoderma, kwa kiasi kikubwa,
huonekana mara nyingi kama ilivyo kwa majeraha
na michubuko kwa binadamu, hasa watoto.
Bacteria
wanaosababisha pyoderma ni pamoja na:
* Staphylococcus
aureus
* Pseudomonas aeruginosa
* Pasteurella multocida.
Bacteria wanaweza
pia kupenya kwenye sehemu zilizo wazi au kunaswa kwenye manyoya
yaliyokunjamana, hususan kwa sungura walio dhaifu au wenye kunenepeana hovyo.
Uchunguzi
Bwana
mifugo atahitaji kutazama sababu zote kabla ya kuanza uchunguzi wa kina, kwani
kuna baadhi ya mambo ambayo yanaweza kufanana na maambukizi ya ngozi.
Hayo ni
pamoja na:
* Utitiri kwenye masikio (Ear mites), ambao unaweza kusababisha michubuko
pembezoni mwa masikio, na kusababisha kunyonyoka kwa manyoya pembezoni mwa
masikio na kwenye mfereji wa sikio
* Chawa, ambao wanaweza kusababisha kunyonyoka kwa manyoya
na kukunjamana kwa manyoya katika maeneo mengi ya mwili
* Hali ya ngozi baada ya kuchomwa sindano ya chanjo, ambayo
inaweza kusababisha michubuko na hata vijipu
* Kaswende ya Sungura (Rabbit
syphilis), hali ambayo mara nyingi husababisha kunyonyoka kwa manyoya.
Kama
mojawapo ya sababu hizi hazitaonekana, basi bwana mifugo anaweza kuchukua
sampuli ya ngozi au culture ili kubaini visababishi vya tatizo.
Tiba
Kutibu
maambukizi ya bacteria kwenye ngozi ya sungura hufanyika kwa njia ya nje ya
mwili.
Sungura
wengi watahitaji kuogeshwa; eneo husika linapaswa kukaushwa ili kuondoa unyevu.
Kama
maambukizi ni makubwa, eneo linalozunguka litahitaji kunyolewa.
Bwana
mifugo anaweza kuandika dawa za jamii ya
antibiotics ili kupakaa eneo lililoathirika.
Kinga
Ni muhimu
kuwapa sungura mlo kamili. Kuzuia kunenepeana hovyo kutapunguza athari za
maambukizi katika ngozi.
Kupunguza
manyoya marefu na kuwasafisha kwa brashi manyoya yao kutapunguza pia uwezekano
wa maambukizi.
Imeandaliwa na www.maendeleovijijini.blogspot.com.
Tupigie: +255 656 331974
Comments
Post a Comment