Featured Post

MAGONJWA YA SUNGURA: KUVIMBA VIFUNDO KATIKA MIGUU (ARTHRITIS)


Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog

Arthritis ni neno la kitaalam ambalo linamaanisha kuvimba kwa vifundo. Yawezekana wewe mfugaji wa sungura umekwishawahi kuona sungura wako akiwa amevimba kwenye vifundo vyake na ukimgusa anaonekana kabisa kuumia.

Tatizo hili hutokea mara kadhaa na mara nyingi septic arthritis ni hali ambayo hutokea wakati bacteria wanashambulia kifundo kimoja au zaidi vya sungura.
Tatizo hili huwakumbuka sungura wa aina zote bila kujali umri, aina ya sungura au jinsi yake.

Dalili

* Tabia ya ulegevu – mara nyingi sungura ataonekana hapendi kuruka ruka ama kukimbia
* Ulemavu – sungura ataonekana kama mlemavu
* Anorexia
* Maumivu ya vifundo na kuvimba
* Joto kali kutoka kwenye vifundo
* Kupungua kwa kasi ya kutembea
* Dalili za maaumbikizo (kama, maambukizi kwenye njia ya mkojo au ugonjwa wa meno).

Chanzo

Bacteria aina ya Pyogenic ndio husababisha septic arthritis. Kuna aina nyingi za bacteria wa pyogenic, wakiwemo staphylococci, pasteurella, na anaerobic (ambao wanaweza kuishi hata kama watakosa oksijeni).
Bacteria hawa wanaweza kusababisha maambukizi mwilini na wanaweza pia kuhamia kwenye vifundo, ambako husababisha ugonjwa wa septic arthritis.
Kuna baadhi ya dalili ambazo zinaweza kumfanya mnyama huyo kuwa katika hatari ya kupata septic arthritis.
Hizi ni pamoja na maambukizi ya muda mrefu (chronic) ya bacteria, majeraha ya ajali kwenye vifundo, na kinga ya mwili kutofanya kazi sawa sawa (immunosuppressive disorders).
Baadhi ya sababu za maambukizi zinaweza kuwa ugonjwa wa meno, uambukizi kwenye njia ya juu ya mfumo wa kupumulia (upper respiratory tract), au kidonda.

Uchunguzi

Sungura mwenye historia ya matatizo katika mfumo wa juu wa upumuaji, matatizo ya meno, au kuwahi kupata jeraha la ajali – kama kung’atwa – anaweza kuwa na tatizo la septic arthritis.
Kama tatizo hili litabainika, vipimo kadhaa vinaweza kufanywa na ofisa mifugo. Uchunguzi wa ute au majimaji kutoka katika maeneo ya vifundo (synovial fluid analysis) unaweza kuonyesha dalili za uwepo ama kutokuwepo kwa septic arthritis, kama kuongezeka kwa kiwango cha majimaji au uwepo wa bakteria.
Sampuli hizi za majimaji zinachukuliwa kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini aina ya bacteria waliomo na kutoa tiba stahiki. Vipimo vingine mbadala ni pamoja na X-ray na uchunguzi wa mkojo.

Tiba

Kama unawatibu sungura, ni vyema kutimu viini vya matatizo ili kutibu septic arthritis. Mara kadhaa, dawa za aina ya antibiotics hutolewa ili kupambana na maambukizi hayo, ingawa wakati mwingine upasuaji unaweza kuhitajika.

Maisha na Utunzaji

Kuna mambo machache unayoweza kufanya kumfanya sungura wako awe katika hali nzuri na mazingira rafiki.
Sehemu anapolala unaweza kuweka nyasi laini, hii itasaidia apone haraka baada ya kufanyiwa upasuji. Wacha kumshughulisha mpaka dalili za tatizo hilo zitakapokwisha.
Ni muhimu kuhakikisha kwamba sungura wanakula vizuri katika kipindi chote wanachougua; wape vyakula vibichi kama za majani mabichi na nyasi bora kavu.
Kama ofisa mifugo ataelekeza utoaji wa dawa, zingatia maelekezo kwa usahihi. Kwa vyovyote vile, dawa za aina ya antibiotics zitatakiwa kwa muda mrefu kidogo.
Kuna hatari pia ya kuibuka upya kwa ugonjwa wa vifundo – ugonjwa sugu ambao unaweza kusababisha vifundo hivyo kushindwa kabisa kurudi katika hali ya kwaida – yakiwa ni matokeo ya septic arthritis.

Kinga

Kutokana na kuwepo kwa sababu nyingi za visababishi vya septic arthritis kwa sungura, kuziorodhesha zote siyo kazi rahisi.
Hata hivyo, ni busara kuwaweka sungura wako katika mazingira ya usafi na salama, bila kuwepo na hatari yoyote ya kuwafanya wapate majeraha. Hakikisha unasafisha mabanda kila wakati.

 

Imeandaliwa na www.maendeleovijijini.blogspot.com. Tupigie: +255 656 331974


Comments