Featured Post

MAGONJWA YA SUNGURA: DAMU KATIKA MKOJO (HEMATURIA)


Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog

WIKI iliyopita msomaji wangu mmoja kupitia blogu hii, Janeth Mchau, alinipigia simu akiwa amefadhaika baada ya kuona sungura wake anakojoa mkojo uliochanganyika na damu. Japokuwa nilijaribu kumwelekeza, lakini sina uhakika kama aliweza kunielewa vyema.

Kwa kuwa ufugaji wa sungura ndiyo kwanza umeanza kushika kasi, basi hata changamoto za magonjwa nazo zimeonekana kuwatatiza na hili linatokana na ukweli kwamba, magonjwa ya sungura bado wataalam wetu wa mifugo hawajayafahamu kwa kina.
Ninaamini tatizo lililompata dada Janeth linawapata wafugaji wengi wa sungura na linaweza kuwa kikwazo kwa sababu hata kwenye maduka ya dawa za mifugo baadhi wamekuwa hawapati ushauri unaokidhi kwa sababu magonjwa ya sungura yanaonekana kuwa ‘mageni’.
Uwepo wa damu kwenye mkojo kitaalam wanaita Hematuria. Ugonjwa huu unaweza kuwapa changamoto kubwa wafugaji wengi ikiwa hawataelewa vyema.
Japokuwa mabaki ya vyakula (kama mabaki ya vyakula visivyomeng’enywa vyema au vinywaji) au damu kutoka kwenye via vya uzazi vya sungura vinaweza kusababisha uwepo wa rangi ya damu kwenye mkojo, lakini hayo yote yasichanganywe na tatizo halisi la hematuria, ambalo linaashiria damu iliyotoka moja kwa moja kwenye mrija wa mkojo.

Dalili na aina zake

* Mkojo wenye rangi nyekundu (kutokana na kutoka kwa mabonge ya damu)
* Maumivu makali ya tumbo hasa katika eneo la palpation
* Kuonekana kwa uvimbe au majipu
* Kuongezeka kwa ukubwa wa kibofu cha mkojo, kunakosababisha tumbo kukaa upande
* Michubuko ya mara kwa mara (kutokana na damu kuweka mabonge)
* Mawe kwenye kibofu cha mkojo (Urocystoliths) yanaweza kugundulika kwa kutomasa tumbo; mara nyingi, jiwe moja, kubwa linaweza kugundulika kwa kutomasa katika eneo la utumbo

Chanzo

Sungura Sedentary, sungura majike, na sungura wenye umri wa kati wako katika hatari ya kupata tatizo la hematuria.
Hili linaweza kusababishwa na mawe kwenye figo, maambukizi ya bacteria kwenye kibofu cha mkojo, na/au kuzidi kiwango cha madini ya calcium kwenye damu.
Chanzo kikubwa cha hematuria kwa majjike, hata hivyo, kiwango kidogo cha nguvu za uzazi katika via vya uzazi.
Coagulation, clotting disorders, au jeraha katika via vya uzazi, mrija wa mkojo au kibofu cha mkojo kunaweza kuwa sababu za kuonekana kwa damu kwenye mkojo.

Uchunguzi

Ofisa mifugo wako anapaswa kwanza kupuuza sababu za kuonekana kwa mkojo mwekundu kwamba ni sababu ya lishe.
Pia mkojo usio na rangi au wa rangi ya udongo unapaswa kutofautishwa na hematuria halisi.
Damu na mkojo huo mwekundu unapaswa kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kujiridhisha kama ni kwa sababu ya wingi wa calcium au kama kuna chembe chembe za saratani kwenye damu.
Kama daktari wa mifugo atahisi chanzo cha damu kwenye mkojo ni kutoka ndani ya kibofu cha mkojo, kama uvimbe, au mawe kwenye kibofu, uchunguzi wa kina (endoscopy) unaweza kutumika ili kujua nafasi ya kibofu cha mkojo.
Mbinu hii hutumia kamera ndogo sana ambayo hufungwa kwenye mrija maalum, ambayo inaweza kuingizwa katika nafasi halisi inayopaswa kuchunguzwa. Kamera hiyo ndogo (endoscope) inaweza kuingizwa kwenye kibofu kupitia katika mrija wa mkojo, kwa kutumia kitu kinachoitwa cystoscope, au inaweza kuingizwa kupitia kwenye eneo dogo baada ya kufanya upasuaji mdogo kwenye tumbo.
Kwa njia hii, ofisa mifugo ataweza kupata taswira halisi ya athari zilizomo, au majeraha, na kama itabainika, atachukua sampuli ya tishu kwa ajili ya kuifanyia biopsy hasa kama kuna uvimbe.

Tiba

Hematuria halisi inaweza kuashiria ugonjwa, ambao utahitaji tiba ya haraka.
Inawezekana kwamba sungura wako amepoteza damu nyingi kupitia kwenye mkojo; kama ni tatizo la upungufu mkubwa wa damu (severely anemic), anaweza kuongezewa damu. Hypercalciuria inahitaji mabadiliko ya chakula pamoja na kubadilisha mazingira pia.
Kama sungura wako anaonyesha kutotulia kutokana na maumivu, dawa za kupunguza maumivu zinaweza kutumika ili pia kupunguza uvimbe.
Dawa za majimaji au mafuta zinaweza kutumika kutibu dehydration, na matatizo ya figo na mawe kwenye njia ya mkojo yanahitaji upasuaji ili kuyaondoa.

Jinsi ya kuwatunza

Baada ya tiba ya awali kupungua au kuondoa tatizo la visababishi vya hematuria, ofisa mifugo anaweza kuweka ratiba ya ufuatiliaji ili kuangalia namna sungura anavyoendelea na tiba au tiba hiyo inavyofanya kazi.
Uchunguzi wa kawaida, vipimo vya maabara, na hata vipimo vya X-Ray au ultrasonic vinaweza kuhitajika, kwa kadiri daktari atakavyokuwa akichunguza matatizo yoyote au kurudia tena kwa upungufu wa damu (anemia), kusinyaa kwa mrija wa mkojo, au figo kushindwa kufanya kazi.

 

Imeandaliwa na www.maendeleovijijini.blogspot.com. Tupigie: +255 656 331974


Comments