- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mhandisi wa Mradi wa Maji kutoka
eneo la Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza kutoka kampuni ya
Koberg Construction Co.Limited Mhandisi Stepheni Kingili kushoto akitoa
maelekezo kwa Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu namna
watakavyoanza kutekeleza mradi huo kuanzia kesho(leo) wakati wa halfa ya
makabidhiano ya vifaa vya mradi huo yaliyofanyika ofisi ndogo za
mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) eneo la
Pongwe
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi
na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua
Mgeyekwa akiingia kwenye halfa hiyo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu |
Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza wakati wa halfa hiyo |
Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Muheza,Luiza Mlelwa akizungumza katika halfa hiyo
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji
Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo
akizungumza katika halfa hiyo
Sehemu ya wagen kutoka
maeneo mbalimbali waliojitokeza kushuhudia makabidhiaano haayo
Sehemu ya wadau
waliohudhuria makabidhiano hayo eneo la Pongwe Jijini
Tanga
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM)
Balozi Adadi Rajaabu wa pili kutoka kulia akiongozana na baadhi ya
viongozi kukagua mabomba yatakayotumikaa kwenye mradi huo kushoto ni
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga
(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa kulia ni Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Muheza Luiza Mlelwa na kushoto ni Mhandisi wa Mradi huo
ambao utatoa maji Pongwe Jijini Tanga Hadi wilayani Muheza
Moja kati ya vifaa mbalimbali
vitakayotumika kwenye mradi huo.
Sehemu ya Mabomba ambayo
yatatumika kwenye mradi huo mkubwa utakaogharimu zaidi ya milioni 400
kwa ajili ya kutoa maji eneo la Pongwe Jijini Tanga Hadi wilayani
Muheza
WANANCHI wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga wataondokana na adha ya huduma ya maji baada ya Serikali kutenga fedha zaidi ya milioni 400 kwa ajili mradi mkubwa wa kutoa maji kutoka eneo la Pongwe Jijini Tanga hadi wilayani Muheza.
Hatua hiyo ina lenga kuondoa changamoto ya uhaba wa maji wilayani Muheza ambayo ilikuwa kikwazo cha maendeleo kwa wananchi kutokana na kutumia muda mwingi kusaka
huduma hiyo badala ya kufanya shughuli za kujiingizia kipato.
Akizungumza jwakati wa kukabidhi mabomba yatakayotumika kwa mkandarasi wa mradi huo katika eneo la Pongwe Jijini Tanga, Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema mradi huo utakuwa ndio mkombozi mkubwa kwa wananchi.
Alisema mradi huo ambao ni mkubwa ni moja kati ya ahadi za Rais John Magufuli alipofanya ziara mkoani Tanga ambapo alihaidi kuhakikisha wakazi wa mji huo wanaondokana na changamoto ya uhaba wa maji.
"Kwanza nimshukuru mh Rais kwa kutekeleza ahadi yake mapema jambo ambalo limetupa faraja kubwa sisi wakazi wa Muheza na vitongoji vyake lakini niwaambie katika mradi huu nitakuwa mkali sana na nitafuatilia kila mwezi kuhakikisha unajengwa kwa viwango kutokana na thamani ya fedha"Alisema.
Aidha alimsisitizia mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo kuhakikisha ajira zitakazotolewa ziwalenge vijana waliopo katika maeneo hayo ili kuweza kupunguza ukali na ugumu wa maisha kwao na jamii zinawazunguka.
Awali akizungumza katika makabidhiano hayo,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa alisema mradi huo ni miongoni mwa miradi ya maji inayotarajiwa kutekelezwa wilayani Muheza ili kumaliza tatizo la maji wilayani humo.
Alisema katika mradi huo mamlaka hiyo imetumia zaidi ya milioni 30 katika bajeti zake kufanya tathimini ya mradi huo huku serikali itokea fedha zote ambazo zitatumika katika mradi huo ambao utakwenda sanjari na ujenzi wa tanki la kuhufadhia maji eneo la Kilapura litakalokuwa na ujazo wa lita laki saba.
"Lengo la mamlaka ya maji na serikali ya wilaya ya Muheza pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya huduma ya maji ambayo ndio kilio chao kikubwa kwa wilaya hiyo "Alisema.
Akizungumzia suala la utunzaji wa mradi huo,Mhandisi Mgeyekwa alisema mradi huo ni mali ya wananchi hivyo lazima wahakikishe wanakuwa mabalozi wazuri wa kulinda miundombinu ya maji ili iweze kuwasaidia wao na vizazi vijavyo.
Naye kwa upande wake,Mkandarasi wa Mradi huo kutoka Kampuni ya Koberg Construction Limited,Mhandisi Stephen Kingili alisema mradi huo utatekelezwa kwa wakati ili kuweza kutoa fursa kwa wananchi wa wilaya ya Muheza kuweza
kunufuika na huduma hiyo.
Alisema utekelezaji wa mradi huo utaanza kutekelezwa kesho (Septemba 21) ambao utakamilika Mei 19 mwakani ukichukua miezi 8 ili kuweza kukamilika na hivyo wananchi kuweza kuutumia.
Aidha alisema mradi huo utakuwa na urefu wa km 16.9 kutoka eneo la Pongwe Jijini Tanga mpaka Muheza mjini ambao utakwenda sambamba na maungio ya kuchepusha maji katika vijiji vyote utakaopita ili kuwarahisishia wananchi kuweza kujiunganishia huduma hiyo pindi wanapokuwa wakihitaji.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
Comments
Post a Comment