Featured Post

WAKAGUZI WA NDANI WATAKA TAARIFA ZAO KUFANYIWA KAZI




Na Woinde Shizza  wa libeneke la kaskazini blog
WAKAGUZI wa ndani Nchini wamewataka wakurugenzi wa taasisi za umma na sekta binafsi  kuzifanyia kazi taarifa zao za kiukaguzi  na kuacha  kuzikalia pindi wanapokabidhiwa  jambo ambalo linasababisha kupotea kwa ufanisi wa utendaji kazi kwa sekta hizo.


Kauli hiyo imetolewa  jijini Arusha na mkaguzi mkuu wa ndani wa serikali,Mohamedi Ntonga katika mkutano mkuu wa mwaka wa wakaguzi wa ndani unaowajumuisha wakaguzi kutoka  sekta ya umma na binafsi wakiwemo kutoka nje ya nchi.  
Ntonga alisema kuwa wakaguzi wa ndani wana umuhimu  mkubwa katika maendeleo ya Taifa lolote Duniani hivyo taarifa za kiukaguzi wanapozikabidhi zinapaswa kufanyiwa kazi kwani zinakuwa zimefanyika kitaalamu,hivyo kitendo cha kuzikalia taarifa hizo kinachofanywa na baadhi ya wakurugenzi wa Taasisi husika kinapelekea kupunguza weledi katika utendaji kazi wao.


Alisema kuwa Mkutano huo ni muhimu sana kwa wakaguzi wa ndani katika kubadilishana uzoefu wa taaluma na kukumbushana yale yaliyo muhimu kwa mujibu wa taaluma yao hivyo akiwasihi watanzanzia kuta mbua umuhimu wa kuwatumia wakaguzi wa ndani katika masuala ya uwazi na uwajibikaji.


Aidha akizungumzia faida za wakaguzi wa ndani kuwa wameweza kuibua wafanyakazi hewa,Mishahara hewa ,watumishi wasio kuwa na taaluma,na upotevu wa fedha unaofanyika kwenye taasisi mbalimbali zikiwemo Wizara, na Halmashauri za Serikali .


Kwa upande wake Rais wa Wakaguzi wa Ndani Tanzania Richard Magongo amesema wakaguzi wa ndani wamekuwa wakitumika kuchochea mabadiliko ya utendaji kazi ili kukabiliana na wizi wa kimtandao ambao umekuwa ukitumika kutokana na kuongezeka kwa Technolojia Duniani.


Magongo aliongeza kuwa  mkutano huo utajikita kuangalia jinsi gani ya kuzitumia taaluma za wakaguzi ili kuenenda sambamba na mabadiliko ya Technolojia yanayosababisha kuongezeka kwa wizi wa kimtandao .



Akizungumzia changamoto zinazo wakabili wakaguzi wa ndani ni pamoja na kufukuzwa kazi pindi wanapokuwa wamekamilisha taarifa za kiukaguzi zinazoonyesha kugusa maslahi ya baadhi ya watendaji jambo linalowapelekea baadhi yao kuingiwa na uwoga na kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Comments