Featured Post

SERIKALI KUBORESHA VITUO VYA MALIKALE KUKUZA UTALII WA NDANI NCHINI


 Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eng Ramo  Makani akisisitiza jambo kwa wabunge wa kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na utalii mara baada ya kuwasili katika mapango ya Amboni Jijini Tanga.





 Wajumbe wa kamati hiyo waakiwa tayari kuingia kwenye mapango hayo
  Wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Guide wa Mapango hayo,Athumani Mangula kuingia kwenye mapango hayo
 Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Atashasta Nditiye kulia akiwa na mjumbe wa kamati hiyo,Marry Chatanda ndani ya mapango ya Amboni
 Wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa na wakiangalia maeneo mbalimbali ya utalii kwenye mapango hayo
Wajumbe wakionyeshwa baadhi ya maeneo kwenye mapango hayo
 Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa ndani ya Mapango ya Amboni Jijini Tanga
Muuongoza watalii kwenye Mapango ya Amboni ( Guide) wa Mapango hayo,Athumani Mangula kushoto akimsikiliza kwa umakini mjumbe wa kamati hiyo,Nape Nnauye


 Muuongoza watalii kwenye Mapango ya Amboni ( Guide) wa Mapango hayo,Athumani Mangula akiwaonyesha wajumbe baadhi ya maeneo ndani ya mapango hayo
 Muuongoza watalii kwenye Mapango ya Amboni ( Guide) wa Mapango hayo,Athumani Mangula akisisitiza jambo kwa wajumbe hao
 Wajumbe wa kamati hiyo wakiingia kwenye mapango ya Amboni
Meneja Mawasiliano wa Tanapa ,Pascal Shelutete kushoto akimsikiliza kwa umakini moja kati ya wajumbe wa kamati hiyo wakati wakiwa kwenye mapango ya Amboni.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani amesema serikali ina mpango wa kuboresha vituo vya malikale vilivyopo nchini kwa lengo la kukuza utalii wa ndani ili kuweza kuchangia uchumi.


Aidha pia alieleza mkakati wa kuwapatia njia mbadala wananchi wanaoendesha shughuli za kibinaadamu pembezoni mwa mto zigi eneo la hifadhi ya mapango ya Amboni Jijini hapa ili kunusuru mazingira.

Mhandisi Makani alisema kuwa mpango wa serikali ni kuinua utalii wa ndani pamoja na kutoa kipaumbele katika kuboresha miundombinu kwenye vivutio vya ndani kama hatua ya kuvitangaza.

Akizungumza  na waandishi wa habari eneo la mapango ya Amboni wakati akiwa kwenye ziara ya kamati ya kudumu ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea hifadhi hiyo ya asili iliyopo nje kidogo mwa Jiji la Tanga.

Mhandisi Makani alizieleza changamoto zilizojitokeza kwenye ziara hiyo kuwa pamoja na uduni wa miundombinu ya barabara, ofisi ya taarifa, kutokuwepo kwa vivutio na huduma muhimu lakini pia shughuli za kibinaadamu zinazofanywa katika eneo hilo zimeonekana kuwa tishio kwenye hifadhi hiyo.

Hata hivyo alisema kuwa serikali ya wilaya na Mkoa kwa upande wake zitalazimika kuchukua hatua ikiwemo kutafuta njia mbadala zitakazofanywa na wananchi hao ili kuacha uharibifu huo huku Wizara yake ikiangalia namna ya kushughulikia changamoto nyingine.

Miongoni mwa shughuli zinazo elezwa  kufanywa na wananchi kwenye maeneo hayo ni ugongaji kokoto na kilimo kazi zilizodaiwa kusababisha mmomonyoko wa ardhi nyakati za mvua na kutishia uwepo wa mapango hayo.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati hiyo, Injinia Atashasta Nditiye alisema kamati hiyo itaishawishi serikali kuwa na mpango wa kuwaendeleza watumishi wa Idara hiyo ili kuwapa utaalamu wa kutosha na hivyo kuleta ufanisi zaidi.

Nditiye alisema kuwa kamati yake pia itahakikisha kuwa vivutio vyote vya asili vinatangazwa na kwamba itawashawishi viongozi wakuu wa nchi kuvitembelea vivutio hivyo na kujionea changamoto zilizopo ili kurahisisha utatuzi wake.

Naye Mkurugenzi msaidizi wa Mambo ya Kale, Digna Tillya alieleza kuwa kituo cha Amboni ambacho kinasimamiwa na Mambo ya Kale kilianzishwa mwaka 1937  na wakoloni waingereza na kwamba vivutio vingine  kwa Mkoa wa Tanga  vilivyoibuliwa  karne ya 16 ni mji mkongwe
Tongoni.

Tillya alieleza changamoto wanazokabiliana nazo sambamba na shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo kuwa  ni uchakavu wa miundombinu ya barabara na kukosekana kwa ofisi kwa ajili ya kutolea taarifa za kituo.


Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Comments