Featured Post

PAMOJA NA KUCHUKULIANA MABIBI, LAKINI FRANCO ALIMPIGIA KAMPENI MOBUTU 1984

Na Daniel Mbega
WAKATI wa kampeni za uchaguzi, mara nyingi wagombea hutumia njia mbalimbali ili kunadi sera zao, ambapo licha ya kusimama majukwaani, kupita nyumba kwa nyumba na kuweka mabango, lakini pia huwatumia wasanii wa kila fani.
Jambo hili haliko Tanzania au Afrika pekee, bali hata katika mataifa yaliyoendelea ambako tumeshuhudia mara nyingi wasanii nyota wakitangaza kuwaunga mkono baadhi ya wagombea huku wengine wakipanda majukwaani kuwaombea kura.
Wanamuziki mara nyingi sana, hata kama hawakupanda majukwaani, lakini hutunga nyimbo mbalimbali za kuwanadi wagombea na inategemea na ushawishi wa wanamuziki wenyewe pamoja na nguvu ya wagombea husika kuweza kubadili mitazamo ya wapiga kura.
L'Okanga La Ndju Pene Luambo Luanzo Makiadi 'Franco', mwanamuziki aliyeweka historia ya pekee Afrika, naye alikuwa miongoni mwa wapiga kampeni, si za siasa tu, bali hata za kijamii kuanzia nchini kwake 'Zaire' na Afrika pia.

Zaire, au kama inavyotambulika sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inafahamika kwamba ilitawaliwa kwa mkono wa chuma na utawala wa kiimla wa mwandishi wa habari, Joseph Desire Mobutu, maarufu kama Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Zabanga, ama kwa kifupi, Mobutu Sese Seko.
Wawili hawa walikuwa marafiki sana kiasi kwamba waliokuwa karibu nao walidai kwamba ilifikia mahali walikuwa 'wakichukuliana mabibi', kila mmoja akitambia nafasi yake, lakini wakati mwingine walikuwa wakipishana.
Inaelezwa kwamba, kuna wakati Franco alishona suti maridadi sana, akapigilia na kwenda Ikulu kumsalimia Mobutu. Alipofika akashangaa kitambaa cha suti yake ndiyo mapazia ya Mobutu! Haijulikani kama Mobutu alisikia kwamba jamaa anashona suti halafu yeye akaamua kumfanyia hiana au la, lakini ndivyo ilivyoelezwa.
Lakini Franco kila ulipowadia uchaguzi, alimuunga mkono rafikiye huyo Mobutu na mwaka 1984 alitunga kibao hiki mahiri sana kiitwacho Candidat Na Biso Mobutu ambacho alikiimba kwa kuchanganya Kilingana na Kifaransa.
Hebu tazama mashairi yake na tafsiri yake ya Kiswahili:
1) Zairoise pe Zairois
Bima na balabala eh
Panzana na ba zone
Ganga lokola kake
Po na candidature ya Marechal
Mobutu Sese Seko (x2)

1) Wanawake na wanaume
Tokeni nje
Tawanyikeni katika kanda zenu
Pigeni kelele kama radi
Kwa ugombea wa Marshall
Mobutu Sese Seko (rudia mara 2)

2) Tozala sincere tozala franc
Hypocrisie to boyi
Ingratitude to boyi
Nani akoki ko sunga ekolo
Soki Mobutu te nani mosusu
Mobutu Sese Seko (x2)

2) Tuwe waaminifu Tuwe wakweli
Tuachane na unafiki
Tuachane na uzandiki
Nani atakayeiongoza nchi
Kama si Mobutu nani mwingine
Mobutu Sese Seko (rudia mara 2)

INSTRUMENTAL

3) Zairoise pe Zairois
Bima na balabala eh
Panzana na ba zone
Ganga lokola kake
Po na candidature ya Marechal
Mobutu Sese Seko

3) Wanawake na wanaume
Tokeni nje
Tawanyikeni katika kanda zenu
Pigeni kelele kama radi
Kwa ugombea wa Marshall
Mobutu Sese Seko

4) Tozala sincere tozala franc
Hypocrisie to boyi
Ingratitude to boyi
Nani akoki ko sunga ekolo
Soki Mobutu te nani mosusu
Mobutu Sese Seko

4) Tuwe waaminifu Tuwe wakweli
Tuachane na unafiki
Tuachane na uzandiki
Nani atakayeiongoza nchi
Kama si Mobutu nani mwingine
Mobutu Sese Seko

5) Yabiso candidat Mobutu Sese
Yabiso candidat Mobutu Sese, Mobutu
Nzambe a tinda yo
Comite central, bo keba naba ndoki
Etumba naba ndoki esili te

5) Mgombea wetu, Mobutu Sese
Mgombea wetu, Mobutu Sese, Mobutu
Mungu amekutuma
Kamati Kuu inamtafuta mchawi
Vita kati yao haijakwisha

6) Tango boko retenir candidat mobutu
Botalana bino na bino na miso
Mobutu, ba ndoki ba silite

6) Baada ya kumchagua tena Mobutu
Kila mtu amtazame mwenzake machoni
Mobutu, mchawi bado yuko pale

7) Janvier ti na mois de Mars
Conscientisation, sensibilisation ya ba peuple
Mars ti na mois mai
Responsalisation ya ba militantes na ba militants
Mois de mai ti na mois de novembre
Propagande electoral poya ko pona president ya MPR
Moto na moto a sala examen de conscience
A kanisa epyi to uti
um

7) Kuanzia Januari hadi Machi
Ni kazi ya uhamasishaji wa watu
Machi hadi Mei
Ni kazi ya uhamasishaji wa jeshi
Kuanzia Mei hadi Novemba
Propaganda kwa ajili ya kumchagua tena rais wa MPR
Kila mtu atapima umakini wake
Fikiria wapi tulikotokea
hum

8) Yabiso candidat Mobutu Sese
Yabiso candidat Mobutu Sese, Mobutu
Nzambe atinda yo
Comite central, bo keba naba ndoki
Etumba naba ndoki esili te

8) Mgombea wetu, Mobutu Sese
Mgombea wetu, Mobutu Sese, Mobutu
Mungu amekutuma
Kamati Kuu inamtafuta mchawi
Vita kati yao haijakwisha

9) Tango boko retenir candidat mobutu
Botalana bino na bino na miso eh
Mobutu, ba ndoki ba silite

9) Baada ya kumchagua tena Mobutu
Kila mtu amtazame mwenzake machoni
Mobutu, mchawi bado yuko pale

10) Belela, belela kombo ya Mobutu
Eko couter you rien, rien
Ganga, ganga na kombo ya mobutu

Azali candidat na biso
Naba zando, na bilanga, na misala epayi bozali
Candidat na biso Mobutu
Bana ya kelasi boyebisa ba tata na ba maman
Candidat na biso Mobutu

Yabiso candidat Mobutu Sese
Yabiso candidat Mobutu Sese, Mobutu
Nzambe a tinda yo
Comite central, bo keba naba ndoki
Etumba naba ndoki esili te

10) Piga kelele piga kelele jina la Mobutu
Haikugharimu chochote, chochote
Piga yowe, piga yowe jina la Mobutu

Yeye ni mgombea wetu
Sokoni,
Mashambani
Kwenye ofisi zenu
Mgombea wetu ni Mobutu
Wanafunzi waambieni wazazi wenu
Mgombea wetu ni Mobutu

Mgombea wetu, Mobutu Sese
Mgombea wetu, Mobutu Sese, Mobutu
Mungu amekutuma
Kamati Kuu inamtafuta mchawi
Vita kati yao haijakwisha

11) Tango boko retenir candidat mobutu
Botalana bino na bino na miso
Mobutu, ba ndoki ba silite

11) Baada ya kumchagua tena Mobutu
Kila mtu amtazame mwenzake machoni
Mobutu, mchawi bado yuko pale

12) Belela, belela kombo ya Mobutu
Eko changer bino rien
Comite centrale, bureau politique na ba commissaires du people

Candidat na biso Mobutu
Conseille executif, la magistrature na armee nationale
Candidat na biso Mobutu
Ba gouverneurs na ba commissaires de zone nyoso eh
Candidat na biso Mobutu

12) Piga kelele, piga kelele jina la Mobutu
Kamwe haitakubadilisha
Kamati Kuu
Idara ya siasa
Na Kamishna wa watu

Mgombea wetu ni Mobutu
Halmashauri kuu, mahakama na jeshi
Mgombea wetu ni Mobutu
Magavana na Mameya, mgombea wetu ni Mobutu

13) Yabiso candidat Mobutu Sese
Yabiso candidat Mobutu Sese, Mobutu
Nzambe a tinda yo
Comite central, bo keba naba ndoki
Etumba naba ndoki esili te

14) Mgombea wetu, Mobutu Sese
Mgombea wetu, Mobutu Sese, Mobutu
Mungu amekutuma
Kamati Kuu inamtafuta mchawi
Vita kati yao haijakwisha

14) Tango boko retenir candidat mobutu
Botalana bino na bino na miso
Mobutu, ba ndoki ba silite

15) Baada ya kumchagua tena Mobutu
Kila mtu amtazame mwenzake machoni
Mobutu, mchawi bado yuko pale

15) Ganga, ganga na kombo ya Mobutu
Eko couter bino rien
Mobutu a zongisa unite nationale
Tambola na kati ya Zaire mobimba
Loba mokoko nyosa yo olingi
Moto akotuna yo azali te
Est-ce que kala ezalaka bongo
Tala elengi ya unite nationale

15) Piga yowe, piga yowe jina la Mobutu
Haitakugharimu chochote
Mobutu alirejea umoja wa kitaifa
Zunguka Zaire yote
Zungumza lugha yoyote unayotaka
Hakuna atakayekuuliza
Je, iliwahi kuwa hivyo?
Haya ni matunda ya umoja wa kitaifa

16) Yabiso candidat Mobutu Sese
Yabiso candidat Mobutu Sese, Mobutu
Nzambe a tinda yo
Comite central, bo keba naba ndoki
Etumba naba ndoki esili te

16) Mgombea wetu, Mobutu Sese
Mgombea wetu, Mobutu Sese, Mobutu
Mungu amekutuma
Kamati Kuu inamtafuta mchawi
Vita kati yao haijakwisha

17) Tango boko retenir candidat mobutu
Botalana bino na bino na miso
Mobutu, ba ndoki ba silite

17) Baada ya kumchagua tena Mobutu
Kila mtu amtazame mwenzake machoni
Mobutu, mchawi bado yuko pale

18) Belela, belela kombo ya Mobutu
Azongisa la paix na Zaire
Mobutu flambeau ya la paix

Tambola ba region nyoso o mona eh
Mitema ya bato etonda bisengo na la paix

Zairois a boya mobulu na ko bomana
Kimia ekota na mboka eh
Mobulu elongwa

18) Piga kelele, piga kelele jina la Mobutu
Alirejesha amani nchini Zaire
Mobutu ni mwenge wa amani

Nenda kwenye mikoa yote na utagundua
Watu wana furaha na amani

Wazaire hawataki migogoro na kuuana wenyewe kwa wenyewe
Nchi imepata amani
Kipindi cha migogoro kimekwisha

19) Yabiso candidat Mobutu Sese
Yabiso candidat Mobutu Sese, Mobutu
Nzambe a tinda yo
Comite central, bo keba naba ndoki
Etumba naba ndoki esili te

19) Mgombea wetu, Mobutu Sese
Mgombea wetu, Mobutu Sese, Mobutu
Mungu amekutuma
Kamati Kuu inamtafuta mchawi
Vita kati yao haijakwisha

20) Tango boko retenir candidat mobutu
Botalana bino na bino na miso
Mobutu, ba ndoki ba silite

20) Baada ya kumchagua tena Mobutu
Kila mtu amtazame mwenzake machoni
Mobutu, mchawi bado yuko pale

21) Belela, belela kombo ya Mobutu
Eko couter bino eloko te
Ganga, ganga na bala bala kombo ya Mobutu
Azali candidat nabiso

Awa ngai nazali koyemba eh
Ba ndoki ba koti nase ya ba drap
Oh Luambo Mobutiste
Nalinbi na tuna bino bozalaka ba nani

21) Piga kelele, piga kelele jina la Mobutu
Haitakugharimu kitu
Piga yowe, piga yowe Mobutu mitaani
Ndiye mgombea wetu

Na hivi ninavyoimba
Wachawi wamejificha chini ya mablanketi yao
Oh Luambo ni mnazi wa Mobutu
Wewe uko kwenye chama gani

22) Yabiso candidat Mobutu Sese
Yabiso candidat Mobutu Sese, Mobutu
Nzambe a tinda yo
Comite central, bo keba naba ndoki
Etumba naba ndoki esili te

22) Mgombea wetu, Mobutu Sese
Mgombea wetu, Mobutu Sese, Mobutu
Mungu amekutuma
Kamati Kuu inamtafuta mchawi
Vita kati yao haijakwisha

23) Tango boko retenir candidat mobutu
Botalana bino na bino na miso eh
Mobutu, ba ndoki ba silite

23) Baada ya kumchagua tena Mobutu
Kila mtu amtazame mwenzake machoni
Mobutu, mchawi bado yuko pale

24) Bino batu bozali na kati ya bus pe ba voiture
Candidat na biso Mobutu
Ozali ko kende voyage na kati ya train avion to masuwa
Candidat na biso Mobutu

24) Nyie watu kwenye mabasi na magari
Mgombea wetu ni Mobutu
Kama unasafiri kwa treni, ndege au mashua
Mgombea wetu ni Mobutu

25) Ba patient nyoso na kati ya ba opitaux
Candidat na biso Mobutu
Ata ko ozali na kati ya boloko po osalaki mabe
Tango bokobima candidat na biso Mobutu

25) Wagonjwa wote hospitalini
Mgombea wetu ni Mobutu
Kama umefungwa kwa sababu ya uhalifu
Utakapoachiliwa huru, mgombea wetu ni Mobutu


Naam. Nadhani umeyapata vizuri na halikuwa (na siyo) kosa wala dhambi kwa mwanamuziki kumpigia kampeni.

IMETAYARISHWA NA www.maendeleovijijini.blogspot.com. Ukirejea ni lazima eleze chanzo ambacho ni www.maendeleovijijini.blogspot.com.

Comments