Featured Post

MUHIMU SANA: MFUMO WA UHAKIKI WA TUZO (AWARD VERIFICATION SYSTEM) ZA STASHAHADA WAFUNGULIWA

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI 

(NACTE)

 


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU   KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA UHAKIKI WA TUZO (AWARD VERIFICATION SYSTEM) ZA STASHAHADA

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuufahamisha umma na wananchi kwa ujumla  kuwa limefungua mfumo wa uhakiki wa Tuzo (Award Verification System) za Stashahada kwa wale wanaopenda kujiendeleza katika ngazi ya shahada.

Baraza linawatangazia  wadau na wahitimu wa Stashahada wanaotaka kujiendeleza kuwa mfumo wa uhakiki wa tuzo umefunguliwa kuanzia leo Tarehe 20 Septemba, 2017 ili kuendelea na Zoezi la uhakiki wa tuzo na kupata Namba ya Uhakiki (Award Verification Number (AVN))

Hivyo kwa wale ambao hawakufanikiwa kumaliza maombi ya uhakiki na wale ambao hawajaombaAVN na wana nia ya kufanya hivyo, sasa wataweza kufanya uhakiki kwa kubofya kitufe kilichoandikwa Award Verification kwenye tovuti ya Baraza www.nacte.go.tz au kwa kubofya hapa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 20, Septemba, 2017

Comments