Featured Post

MARIO: UJUMBE KWA WANAUME WANAOPENDA ‘KULELEWA’ NA WANAWAKE


Na Daniel Mbega
WENGI wanaujua wimbo huu wa Mario unamaanisha nini. Lakini hapa nimeuleta mzima mzima nikiwa nimeutafsiri pia: 

Oh Mario
Luka ata mwasi yo moko obala
(Oh Mario, tafuta mwanamke uoe)
Mario mosala kolinga ba mama mobokoli
(Una tabia ya kwenda kwa wanawake wazee)
Basuka yo te?
(Hivi hutosheki nao?)

Lelo makambo lobi makambo nalembi
(Leo matatizo, kesho matatizo nimechoka)
Lelo bitumba lobi koswana nabaye
(Leo kupigana, kesho ugomvi, nachukia)
Naboyi kobebisa nzoto na manzaka nalembi eh
(Sitaki tena uuharibu mwili wangu na kucha zako)
Mario nalembi e e
(Mario nimechoka)
Mario nabaye e e
(Mario sipendi)

Oh Mario nasi napekisa yo
Kolingaka basi bazali na mbongo-
(Mario nimekuwa nikukataza usijenge mazowea na fedha)
Yoka ndenge azali kokaba yo na mitema ya basi mpe mibali-
(Sikia jinsi anavyokuumbua mbele ya wanawake na wanaume)
Sala quand mome effeot oluka mosala Mario-
(Fanya bidii utafute kazi Mario)
yo mutu ozali na ba diplomes mitano Mario-
(Wewe una digrii tano Mario)
Mpona nini ozali kobebisa kosambuisa kombo nayo-
(Kwa nini unaharibu na kuchafua hadhi na jina lako)
Mario ah nalembi-
(Mario nimechoka)
Ba produits ngai napokaolaka nzoto ekoma sembe sembe-
(Vipodozi ninavyopaka kwenye ngozi yangu vimeufanya mwili wangu uwe laini)
Okobeteke ngai ti na zoka lobi na zwa maladie ya cancer-
(Unanipiga mpaka navuja damu, kesho niugue maladhi ya kansa)
Lobi tango na kopolo yo okimi ngai eh-
(Kesho nikianza kuoza utanikimbia)
Mario nalembi eh-
(Mario nimechoka)
Bima bima na ndako na ngai Mario-
(Ondoka ondoka nyumbani kwangu Mario)
Mpo na nininiongo ya kolinga-
(Kwani huu ni utumwa wa mapenzi?)
Akobeteke ngai na zwa epayi zuwa ya lokuta epayi
Zuwa ya biloko akutaki ngai na yango-
(Ananipiga kutokana na wivu wa kipuuzi, kwa uongo na kwa mali, mali alizozikuta nyumbani kwangu)
Likambo mosusu mosala koboma biloko ya ndako na somba-
(Kitu kingine anachokifanya ni kuharibu mali za nyumbani kwangu, vitu ambavyo nilinunua mwenyewe)
Nalembi eh Mario na baye yo-
(Nimechoka eeh Mario nakuchukia)
Kende Mario nalembi yo oh-
(Nenda zako Mario nimechoka)
Mario akuti ngai na biloko mobali mosusu asomba-
(Mario alinikuta nina mali, nyingine zilinunuliwa na mwanamume mwingine)

Oyoka elengi ya kovanda te Mario? -
(Unafurahi kukaa bila kazi?)
Oyoka elengi te olia na mesa? -
(Hufurahii kulia chakula mezani?)
Kaka soki zuwa ekangi yo na poitrine -
(Sasa vipi wivu unapokuzidi)
Olingi kaka kobeta ngai na koboma biloko -
(Unachofanya ni kunipiga na kuharibu mali)
Mario si na salisa yo mingi -
(Mario nimekusaidia sana)
Diplome ya sima ngai na salisaki yo Mario-
(Nilikusaidia kupata shahada yako ya mwisho)
Bongo lelo ngai nakomi mwasi mabe?-
(Lakini leo nimekuwa mwanamke mbaya)
Mario likambo te-
(Mario hakuna tatizo)
Ah mokili eza kaka boye hum-
(Aah hayo ndiyo maisha, hivyo ndivyo dunia ilivyo)

Mobali akuti ngai na bomemgo
Asengi akomander ngai na ndimi-
(Mwanamume huyu alinikuta nikifurahia maisha mazuri, aliomba anidhibiti name nikakubali)
Mobali akuti ngai na bangenge
Asengi adiriger ngai na ndimi-
(Mwanamume huyu alinikuta nikifurahia utajiri, alinitaka yeye ndiye awe na mamlaka nikakubali)
Nabandi kobima na ye babandi kobenga ye Monsieur-
(Nilipompenda kila mmoja akaanza kumwita Bwana)
Mario nale mbongo ya likelemba mitu tuku misato
Nasombi Mercedes 190 nayebisi Mario mokolo mosusu tobima-
(Nilinunua Mercedes Benz 190 kwa ajili yangu siku moja nikamwambia Mario tukatembee tule raha)
Tokende kosala promenade-
(Twende tukafurahi na kupata promenade)
Tokomi na nzela Mario alobi na ngai
Y o zonga cete ngai ngai na zali-
(Tulipofika barabarani Mario akaamuru nimpeleke kule alikokuwa anaishi zamani)
Nakumba voiture mpo bamona que ngai
Moto nasombeli yo yango-
(Ili watu wajue kwamba ni yeye aliyenunua gari)
Nayebisi Mario te-
(Nilimwambia Mario hilo haliwezekani)
Ngai kutu na za na posa na kumba eloko nasombi sika-
(Bado ni hamu ya kuendesha gari langu jipya)
Bato nionso bamonaque ngai moto nasombi-
(Ili watu wajue mimi ndiye hasa niliyenunua gari hili)
Toweli volant ngai na Mario-
(Tupigana na Mario tukigombea usukani)
Mario atuteli ngai voiture na nzete-
(Mario akagongesha gari langu kwenye mti)

Nzoto ezali nanu ya meme olingi obebisa ngai elongi-
(Mwili wangu bado mbichi lakini unataka kuharibu uso wangu)
Il para et basi nionso ozwaka mosala kobebisa bango bilongi-
(Tabia yake imekuwa kuharibu nyuso za wapenzi wake wote wa zamani)
Epayi na ngai na stopper nalembi yo-
(Kwangu mimi haiwezi kuwa hivyo nimeshindwa na nimekuchoka)
Mario papa na baye yo oh-
(Mario nakuchukia)
Kende na yo nalembi yo-
(Mario nimekuchoka)
Mario azongi epayi ya baboti
Akuti mbeto na ye ya bomwana-
(Mario alikwenda nyumbani kwa wazazi wake na kukikuta kitanda cha utoto wake)
Ekomi tango ya kolala mbeto mokuse makolo milayi Mario-
(Ulipofika wakati wa kulala miguu yake ilikuwa mirefu kuliko kitanda chake cha utotoni)
Mario nalembi somba mbeto na baye e-
(Mario nimechoka, nunua kitanda chako nimeshindwa na nimechoka)
Koyoka motema pasi te ndako ngai moko nafutaka
(Uache moyo wako usihangaike, mimi ndiye ninayelipa kodi ya nyumba)
Bilamba nasombela yo natikeli yo souvenir ya bolingo-
(Chochote nilichokununulia wakati tulipokuwa tunapendana, kiweke kiwe ukumbusho wa penzi letu)
Oyo ezali na lavage nakotindela yo na bato-
(Kilichoko kwenye beseni la kufulia nitawapa wengine)
Mario nale mbi yo oh-
(Mario nimekuchoka)
Kende na yo na baye yo oh-
(Ondoka zako nakuchukia)


IMETAYARISHWA NA www.maendeleovijijini.blogspot.com. Ukirejea ni lazima eleze chanzo ambacho ni www.maendeleovijijini.blogspot.com.

Comments