Featured Post

MARIE STOPES TANZANIA YAZINDUA TENA HOSPITALI ILIYOBORESHWA NA KITUO CHA KUPOKEA SIMU ZA WATEJA MWENGE

Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Hebogard Jensen (katikati) akikata utepe wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospitali iliyoboreshwa ya Marie Stopes Mwenge leo jijini Dar es salaam. Hospitali hiyo pia imezindua kituo cha kupokea simu na pia kuanzisha huduma ya bure ya siku tatu kwa watakaopenda kupima magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, Ukimwi, ushauri wa masuala ya uzazi wa mpango, Kansa ya mlango wa kizazi huku huduma nyingine za kitabibu zikitolewa kwa gharama.

Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar HebogÄrd Jensen akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa hospitali iliyoboreshwa ya Marie Stopes Mwenge leo jijini Dar es salaam. Hospitali hiyo pia imezindua kituo cha kupokea simu na kuanzisha huduma ya bure ya siku tatu kwa watakaopenda kupima magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, Ukimwi, ushauri wa masuala ya uzazi wa mpango, Kansa ya mlango wa kizazi huku huduma nyingine za kitabibu zikitolewa kwa gharama. Anayeshuhudia (kulia) ni Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay.
 Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospitali iliyoboreshwa ya Marie Stopes Mwenge leo jijini Dar es salaam. Hospitali hiyo pia imezindua kituo cha kupokea simu na kuanzisha huduma ya bure ya siku tatu kwa watakaopenda kupima magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, Ukimwi, ushauri wa masuala ya uzazi wa mpango, Kansa ya mlango wa kizazi huku huduma nyingine za kitabibu zikitolewa kwa gharama.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar HebogÄrd Jensen akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes Anil Tambay, wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospitali iliyoboreshwa ya Marie Stopes Mwenge leo jijini Dar es salaam. Hospitali hiyo pia imezindua kituo cha kupokea simu na kuanzisha huduma ya bure ya siku tatu kwa watakaopenda kupima magonjwa mbalimbali kama shinikizo la damu, Ukimwi, ushauri wa masuala ya uzazi wa mpango, Kansa ya mlango wa kizazi huku huduma nyingine za kitabibu zikitolewa kwa gharama.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Hebogard Jensen (katikati) akikata utepe wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha kupokea simu cha Marie Stopes Mwenge leo jijini Dar es salaam.Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa marie Stopes Tanzania Anil Tambay na Mratibu wa huduma ya Afya ya Mzazi na Mtoto Edith Manase Mboga.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Hebogard Jensen (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa dawa za usingizi na ganzi, David Chiunga wakati wa uzinduzi wa hospitali iliyoboreshwa ya Maries Stopes Mwenge pamoja na kituo cha kupokea simu leo jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam, 28 Septemba 2017– Marie Stopes Tanzania (MST) leo imeizindua upya hospitali yake iliyopo Mwenge inayopatikana kwenye kitalu namba 421 na 422 Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Hebogard Jensen ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliipongeza MST kwa kuonyesha juhudi za dhati za kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba wananchi wengi zaidi wanapata huduma za afya zilizo bora na bei nafuu.
“Nchini Tanzania, Marie Stopes inatambulika kwa utoaji wa huduma bora za afya ambazo wananchi wengi wanaweza kuzimudu, lakini kubwa zaidi ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za afya,” alisema Jensen.
Kuzinduliwa upya kwa hospitali hiyo ni matunda ya ushirikiano kati ya MST na DANIDA/ Ubalozi wa Denmark ambapo wameifanya hospitali hiyo kuwa miongoni mwa vituo bora vya afya kwa ajili ya uzazi wa mpango na huduma ya elimu ya afya ya uzazi.
Alisema ushirikiano wa DANIDA na Marie Stopes Tanzania utakuwa endelevu kwa manufaa ya Watanzania wote.
“Tutaendelea kuwekeza kwenye jamii ambayo tunafanya kazi ili kusaidia kutekeleza miradi yetu mbalimbali ya afya, elimu na pamoja na vita ya kutokomeza umaskini,” alisema.
Jensen pia alizindua kituo cha mawasiliano cha ‘MST Contact Centre’ ambacho kitakuwa ni kitovu cha huduma ya kupiga simu bure kutoka kwa wateja na umma kiujumla ili kuimarisha mawasiliano na watoa huduma wa MST.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Marie Stopes Tanzania, Anil Tambay alisema hospitali hiyo iliyozinduliwa upya itatoa huduma nzuri kwa wateja ikiwa pamoja na mazingira mazuri zaidi kwa wagonjwa.
Aliongeza kuwa huduma mbalimbali zinapatikana na kwenye vituo vya MST ikiwa ni pamoja na huduma ya afya ya uzazi inayotolewa mikoa yote ya Tanzania kupitia njia ya simu ya mkononi.
MST inafanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya Tanzania kwa hatua zote ikiwa ni pamoja na kusaidia awamu ya nne ya Mpango Mkakati wa Afya wa HSSP-IV wa mwaka (2015-2020) ikiwa kama mshirika wa sekta binafsi (PPP).
Kwa fedha zinazopatikana kutoka DFID, DANIDA, USAID na wengine wengi, MST imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali na kutekeleza utoaji wa huduma ya uzazi wa mpango wa familia na afya ya uzazi, huduma ya baada ya mimba kuharibika (CPAC) pamoja na unyanyasi wa kijinsia (GBV), vipimo vya HIV, utoaji wa huduma ya uzazi wa mpango pamoja na uchunguzi wa Miradi hii imezingatia kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na uzazi kwa jamii zenye mahitaji nchini Tanzania.
Marie Stopes Tanzania imejikita katika kutoa huduma bora za afya ya uzazi na uzazi wa mpango ambazo zinapatikana karibu mikoa yote nchini Tanzania kupitia huduma zinazohamishika. Aidha, huduma za matibabu za jumla zinatolewa pia katika vituo vya afya vya MST. MST hufanya kazi kwa ukaribu sana na Serikali ya Tanzania katika ngazi zote, kusaidia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya - HSSP-IV (2015 - 2020), kama ushirikiano wa kibinafsi wa umma (PPP). Mnamo mwaka wa 2016, MST iliwapokea wateja milioni 7 na kutoa huduma ya uzazi kwa wateja zaidi ya milioni 2.1.
MWISHO
Mambo ya msingi ya kuzingatia kwa wahariri
MST Contact (Call) Centre namba ni 0800753333

Kuhusu Marie Stopes Tanzania
Marie Stopes Tanzania (MST) ni taasisi iliyojikita katika utoaji wa huduma za uzazi wa mpango na afya ya uzazi ambayo imekuwa ikifanya kazi zake ili kuboresha afya za wanaume na wanawake katika mikoa yote nchini Tanzania pamoja na mambo mbalimbali yanayohusu afya.
Marie Stopes Tanzania imekuwa ikitekeleza kwa ufanisi kazi ya uchunguzi wa Saratani njia ya kizazi katika mikoa nane ambako MST ina zahanati. Zahanati hizi za MST zinapatikana Mwanza, Arusha, Mbeya, Iringa, Dar es Salaam, Kahama, Musoma na Zanzibar.
MST ni sehemu ya ushirikiano wa Marie Stopes International ambayo inafanya kazi katika mataifa 37 kwa kutoa huduma za afya kwa wanaume na wanawake.
Huduma hii ya Marie Stopes International inawapa mamilioni ya wanawake uwezo wa kuchagua ni muda gani wa kupata watoto ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao kuwa na maisha bora zaidi.

Comments