Featured Post

HISTORIA YA SARAFU YA TANZANIA TANGU MKOLONI

  1. [​IMG]

    Nimesikia kuwa hivi karibuni, nchi zote za Afrika ya Mashariki zitatumia sarafu moja. Nimekuwa natafiti pole pole kutafuta picha za pesa tulizowahi kutumia hapa kwetu, nikaona nizitundike hapa kukumbushana tulikotoka.
    Kuna sarafu ambazo nimeshindwa kupata picha zake, lakini hata hivyo nadhani nimefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90 kukusanya ukweli kuhusu sarafu yetu. Najua kuwa hadithi hii ni ndefu sana, hata hivyo kama unataka kujua historia ya sarafu yetu jipe dakika kumi hivi kuisoma yote hapa; ni burudani ya aina yake.
    Kabla ya mwaka 1884, nchi yetu ilikuwa inatumia sarafu moja ya Riyal iliyokuwa imetolewa na Sultan wa Zanzibar chini ya Sultani wa Oman. Sarafu za Riyal zilikuwa kama ifuatavyo

    Riyal

    [​IMG]

    [​IMG]

    [​IMG]
    Baada ya 1884, Zanzibar ilitumia sarafu za aina tatu kwa mpigo. Sarafu ya kwanza ilijulikana kama Maria Theresa Thaler iliyotolewa Italy, ilikuwa na sura ifuatayo.

    Maria Theresa Saler

    [​IMG]
    Sarafu ya pili ilikuwa ni rupia ya kihindi pamoja na visehemu vyake ambavyo vilikuwa vingi kidogo. Sehemu kubwa za rupia zilikuwa ni Anna, pice , robo rupia na nusu rupia:

    1 Anna

    [​IMG]

    1/4 Rupee


    [​IMG]

    1/2 Rupee

    [​IMG]
    1 Rupee 

    [​IMG]

    Pesa hizi zilikuwa ngumu sana hasa kwa vile Anna ilikuwa na vipande vingine kama 1/12 ya Anna, 1/6 ya Anna, 1/4 ya Anna na kadhalika. Sikuweka picha za vipande hivi ingawa ninavyo.
    Sarafu ya tatu ilikuwa inajulikana kama Zanzibari Rupee ambao kimsingi ilikuwa sawa na rupee ya kiingereza iliyokuwa ikutumika Kenya na Uganda. Sikupata picha yake.
    Kwa upande wa bara, kuanzia mwaka 1884 ilikuwa inatumia Rupie za kijerumani. Rupie moja ilikuwa imegawanyika katika pesa 64. Neno la kiswahili "pesa" linatokana na sehemu hii ya rupie.

    Pesa 1

    [​IMG]

    Rupie 1

    [​IMG]

    Mwaka 1891 ziliongezwa sarafu za robo rupie na za nusu rupie kama ifuatavyo.

    1/4 Rupie

    [​IMG]

    1/2 Rupie

    [​IMG]

    Ilipofika mwaka 1893 ikaongezwa sarafu ya rupie 2 iliyoonekana kama ifuatavyo

    2 Rupee

    [​IMG]

    Sarafu zote hizo ziliendelea kutumika hadi mwaka 1904 ambapo sarafu ya rupie iligawanywa katika vipande mia moja (decimalization), kila kipande kikijulikana kama "heller." Neno la kiswahili "hela" limetokana na mgawanyo huo. Sarafu za
    nusu heller na heller moja zilitolewa wakati huo zikiwa na sura zifuatazo.

    1/2 Heller

    [​IMG]

    1 Heller

    [​IMG]

    Kipindi hicho, sarafu za robo rupie, nusu rupie, na rupie 1 zilitolewa upya zikiwa na sura zifuatazo:

    1/4 Rupie

    [​IMG]

    1/2 Rupie

    [​IMG]

    1 Rupie

    [​IMG]

    Mwaka 1908, serikali iliamua kuongeza idadi ya sarafu kwa kuingiza sarafu ya heller 5 na heller kumi zilizokuwa na sura zifuatazo. 

    5 Heller 

    [​IMG]

    10 Heller

    [​IMG]

    Hata hivyo, ilipofika mwaka 1913 sarafu ya heller 5 ilibadilishwa sura na kuwa kama ifuatavyo

    5 Heller 

    [​IMG]

    Sarafu hizi ziliendelea kutumika hadi vita ya kwanza ya dunia ilipoanza mwaka 1916. Mwaka huo serikali ilitoa sarafu ambazo hazikuwa zimetengenezwa kwa ufundi kabisa. Sarafu zilizotolewa wakati huo zilikuwa zile za heller 5, heller 20 na rupie 15. Sarafu za heller 5 na heller 20 zilikuwa na sura ifuatayo.

    Heller 5

    [​IMG]

    Heller 20

    [​IMG]

    Sarafu ya rupie 15 ilikuwa ya dhahabu, ilijulikana kama "Tabora Pound." Ni kati ya sarafu ambazo zilikuwa ghali sana katika historia ya nchi. Kwa bahati mbaya siyo sarafu nyingi zilizoingia kwenye mzunguko kutokana na vita, kwa hiyo nyingi ziliishia kwenye minada ya wakusanya sarafu. Sura yake ilikuwa kama ifuatavyo

    Rupien 15

    [​IMG]


    Baada ya vita ya dunia mwaka 1919, Bara na Zanzibar pamoja na Kenya na Uganda zilikuwa chini ya himaya ya mwingereza ingawa kwa mikataba tofauti. Kuanzia hapo nchi hizo zilianza kutumia sarafu moja. Katika kipindi kifupi kuanzia mishoni mwaka 1919 hadi kati kati ya mwaka 1920, bara walitumia rupie za kijerumani pamoja na rupie za kiingereza zilizokuwa zikitumika nchini Kenya, Uganda na Zanzibar. Baada ya hapo, sarafu mpya ya Florin ya Afrika Mashariki iliingizwa kwenye mzunguko badala ya rupie na rupee. Kwa bahati mbaya sarafu hii ya Florin haikudumu muda mrefu na mwanzoni mwa mwaka 1921 ikabadilishwa na Shillingi ya Afrika ya Mashariki. Kwa hali hiyo kuna sarafu chache sana za Florin zilizotolewa katika kipindi hicho na sikufanikiwa kupata picha yake. Sarafu ya Shilingi ya Afrika Mashahariki ni kati ya sarafu imara sana zilizokaa kwenye mzunguko kwa muda mrefu bila kufanyiwa mabadiliko yoyote. Ilitolewa katika vipande vya senti 1, senti 5, senti 10, senti 50(nusu shillingi) na shilingi 1. Upande mmoka wa sarafu hizo ulionyesha jina la mtawala wa himaya ya uingereza, na upande wa pili ama ulikuwa na ama pembe za tembo au picha ya simba dume. Pembe za tembo zilikuwa kwenye sarafu za senti 1, senti 5 na senti 10 wakati simba dume alikuwa kwenye sarafu za senti hamsini na shilingi moja kama ifuatavyo
  2. Nyuma ya sarafu
    [​IMG]

    [​IMG]

    Upande ulioonyesha mtawala wa uingereza ulifanyiwa mabadiliko ya mara kwa mara kulingana na mabadiliko ya kiutawala. Kuanzia mwaka 1921 mpaka mwanzoni mwa mwaka 1936 wakati wa utawala wa Mfalme George wa tano sarafu zilikuwa na sura ifuatayo.

    [​IMG]

    [​IMG]

    Baada ya kifo cha Mfame George wa tano na utawala kuchukuliwa na Mfalme Edward wa nane, ni sarafu moja tu iliyobadilishwa kwa vile mfalme huyu alivuliwa madaraka baada ya muda mfupi tu kutokana na uamuzi wake wa kuoa mwanamke aliyekuwa ameachika Marekani. Sarafu iliyobadilika wakati huo ilikuwa ya senti tano tu, ambayo ilionekana kama ifuatavyo

    Senti 5

    [​IMG]

    Mfalme George wa sita aliyekuwa mdogo wa mfalme Edward wa nane alichukua madaraka mwishoni mwa mwaka huo huo wa 1936. Sarafu zilizotengezwa wakati wa utawala wake zilikuwa na sura za aina mbili. Sura ya kwanza ilionyesha mfalme kama GEORGIVS VI. Sarafu za aina hii zilitolewa kati ya mwaka 1937 hadi mwaka 1946; zilikuwa na sura ifuatayo.

    [​IMG]

    [​IMG]

    Sarafu za aina ya pili cghini ya Mfalme george wa sita silikuwa na maneno ya GEORGIVS SEXTVS REX. Hizi zilitolewa kati ya 

    mwaka 1949 hadi mwaka 1952 alipofariki. sarafu hizo zilionekana kama ifuatavyo.

    [​IMG]

    [​IMG]

    Baada ya mfalme George wa sita kufariki, alirithiwa na binti yake Malkia Elizabeth wa pili mwaka 1952. Chini ya malkia huyu sarafu ziliokena kama ifuatavyo.

    [​IMG]

    [​IMG]

    Sarafu hizi zilendelea kutumika hata baada ya kupata uhuru wetu. Kwa mafano sarafu zilizotolewa mwaka 1963 (baada ya uhuru)
    zilionekana ifutavyo.

    [​IMG]

    Ilipofika mwaka 1964, kukafanyika mabadiliko kidogo katika sura ya sarafu yetu kwa kuondoa maneno yanayoonyesha mtawala wa himaya ya kiingereza. Sarafu za senti tano na senti kumi zilizotolewa mwaka 1964 zilikuwa zinaonekana kama ifuatavyo.


    [​IMG]

    Hata hivyo sarafu ya pamoja ya Afrika Mashariki ilifikia kikomo chake mwaka 1966 wakati Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki ilipovunjwa na kuundwa kwa benki kuu za Tanzania, Kenya na Uganda. Sijaelewa sababu ya kuvunjika kwa bodi hiyo ya sarafu, bado ninafanya utafiti. 
     
    Benki Kuu ya Tanzania ilitoa sarafu nne za kwanza mara tu baada ya kuundwa 1966. Sarafu hizo zilikuwa za senti tano, senti ishirini, senti hamsini na shilingi moja. sarafu hizo zilionekana kama ifuatavyo: 
    Senti 5

    [​IMG]
  3. Senti 20
    [​IMG]

    Senti 50

    [​IMG]

    Shilingi 1

    [​IMG]

    Sarafu hizi zinaendelea kutumika hadi leo ingawa thamani ya shilingi imeshuka kiasi kuwa zinaonekana hazina thamani yoyote. Ilipofika mwaka 1971 wakati wa sherehe za miaka kumi ya uhuru, sarafu mpya ya shilingi tano iliyokuwa na pembe kumi na mbili ilitolewa. Wakati huo exchange rate ya dola kwa shilingi ilikuwa ni shilingi tano kwa dola moja ya kimarekani. Kwa hiyo sarafu hii ya shilingi tano ilijuikana pia kama "dola" au "DALA" ingawa kwenye mikoa ya ziwa ilijulikana zaidi kama "Scania." Nadhani mnakumbukua chanzo cha neno "dala dala" ni kutokana na nauli ya mabasi hayo wakati huo kuwa shilingi tano. Sarafu hii ya miaka kumi ya uhuru haikudumu sana na mwaka 1972 ikabadilishwa sura na kuwa na pembe kumi kama ifuatavyo.

    Shilingi 5

    [​IMG]

    Kuna taarifa kuwa mwaka 1974 sarafu mpya za shilingi 25 na shilingi 1000 zilitolewa ingawa benki kuu haikutunza picha zake. Ingawa sikuweza kupata sura ya sarafu ya shillingi 1000, nimefanikiwa kupata picha ya sarafu ya shillingi 25 ambayo ilikuwa na sura ifuatayo:

    Shilingi 25

    [​IMG]

    Mara baada ya kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977, thamani ya pesa ilianza kupunguka pole pole kiasi kuwa kulikuwa na haja ya kuwa na sarafu kati ya senti ishirini na senti tano. Hivyo sarafu ya senti kumi iliingizwa kwenye mzunguko; sarafu hii ilikuwa kama ifuatavyo.

    Senti 10

    [​IMG]

    Kufuatia mkutano wa FAO uliofanyika Arusha mwezi September mwaka 1978, sarafu chache za shillingi 5 zilitolewa kukumbukia mkutano huo; sarafu hizo zikuwa na sura ifuatayo

    Shillingi 5

    [​IMG]

    Baada ya hapo, hakukuwa na sarafu mpya hadi mwaka 1982 wakati wa sherehe za miaka 20ya uhuru ambapo sarafu mpya ya shillingi 20 ilitolewa ikiwa na sura ifuatayo.

    Shillingi 20

    [​IMG]

    Hiyo ndiyo iliyokuwa sarafu ya mwisho kutolewa wakati wa utawala wa Nyerere. Rais Mwinyi alipochukua madaraka mwaka 1985, aliendelea na sarafu zenye picha ya Nyerere hadi mwaka 1986 zilipotolewa sarafu zenye picha ya Mwinyi. Sarafu za senti tano, 
    kumi, na ishirini hazikutolewa tena. Sarafu zilizotolewa wakati huo zilikuwa za senti 50, Shilingi 1, shilingi tano na shilingi kumi ambayo ilikuwa na sura ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Sarafu hizo ni hizi hapa:


    Senti Hamsini

    [​IMG]

    Shilingi Moja

    [​IMG]

    Shilingi Tano

    [​IMG]

    Shilingi 10

    [​IMG]


    Kadri thamani ya shilingi ilivyoendelea kudorora, ilibdi kutengeneza sarafu nyingine ambapo sarafu ya shilingi 20 ilitolewa mwaka 1990 ikiwa na sura ya Mwinyi kama ifuatavyo.

    Shilingi 20

    [​IMG]

    Mwaka huo huo sarafu nyingine ya shilingi 5 ilitolewa kwa kumbukumbu ya jengo jipya la benki kuu. Kwa bahati mbaya sikufanikiwa kupata picha yake. Mwishoni mwa utawala wa mwinyi, thamani ya shilingi ilikuwa chini kiasi kuwa sarafu ya Baba wa Taifa yenye thamani ya shilingu kumi ilikuwa inakimbilia kuishiwa nguvu yake. Hivyo sarafu mpya yenye sura wa baba wa taifa ikatengezwa ikiwa na thamani ya shillingi 100.

    Shilingi 100

    [​IMG]

    Rais Mkapa alipoingia madarakani mwaka 1995, akapiga marufuku matumizi ya sura za raisi aliyeko madarakani kwenye sarafu: alipendelea sura za waasisi wa taifa tu na picha alama za asili za nchi ndizo zitumike. Hata hivyo hakutaka kuondoa kabisa sura ya rais Mwinyi kwenye sarafu, hivyo ikatengezwa sarafu mpya ya shilingi 50 iliyokuwa na sura ya Mwinyi kama ionekanavyo hapo chini iliyotolewa mwaka 1996.

    Shilingi 50

    [​IMG]

    Wakati huo huo sarafu tatu zilitolewa kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 35 ya uhuru pamoja ni michezo ya 26 ya olimpiki iliyofanyika Atlanta Marekani mwaka huo. Sarafu hizi zilionyesha wachezaji wa kutupa tufe, riadha, na karate kama ifuatavyo.
    Tufe

    [​IMG]

    Riadha

    [​IMG]
    Karate
    [​IMG]

    Mwaka 1997 kulitolewa sarafu mbili mpya: moja ilikuwa na thamani ya shillingi 500 ikiwa inakumbukia miaka 75 tangu malkia Elizabeth mama wa malkia Elizabeth II alipotembelea nchi yetu mwaka 1923. Sarafu ya pili ilikuwa na thamani ya shillingi 200 ikiwa inatukuza mbuga za wanyama pori wa Afrika. Sarafu hizo zilikuwa na sura zifuatazo:

    Shilingi 200

    [​IMG]


    Shilingi 500

    [​IMG]

    Mwaka 1998, ilitolewa sarafu nyingine ya kudumu ya shilingi 200 kuchukua nafasi ya sarafu zote za kumbukumbu zilizokuwa na thamani hiyo. Sarafu hiyo ilikuwa na picha Karume na inaonekana kama ifuatavyo:

    Shilingi 200

    [​IMG]

    Mwaka huo huo, ilitolewa sarafu nyingine ya thamani ya shilingi mia tano kutukuza mbuga za Serengeti. Sarafu hiyo ilikuwa na sura ifuatayo.

    Shilingi 500

    [​IMG]



    Kuanzia mwaka 1998, sarafu yetu ilikuwa imara tena na haijatolewa sarafu nyingine mpya kwa karibu miaka tisa sasa. Mpaka sasa sarafu kubwa zinazotumika ni zile za shillingi 50, 100 na 200 zionekazo hapa chini:
     
    Shilingi 50[​IMG]
    Shilingi 100
  4. [​IMG]
  5. Shilingi 200
  6. [​IMG]
  7. Hata hivyo, sarafu zote zilizowahi kutolewa na benki kuu ya Tanzania bado ni halali ingawa ama hazipatikani tena kwenye mzunguko au zimashekuwa na thamani ndogo kiasi kuwa zinahitajika nyingi sana ili kufanya manunuzi ya aina yoyote. Katika historia ya benki kuu, hakuna sarafu yake iliyowahi kufutwa.
    Chanzo: JamiiForums 

Comments