Featured Post

'FLORA UNE FEMME DIFFICILE' NI UJUMBE MUHIMU WA FRANCO KWA WANANDOA

Jalada la LP ya Les On Dit likionyesha picha ya Josky Kiambukuta, Nana Akumu, Franco na Baniel Bambo.

Na Daiel Mbega
Mwanzoni wa mwaka 1987, Franco aliachia wimbo mrefu wa dakika 15, akaupa jina la Attention Na Sida (Jihadhari na Ukimwi). Pia mwaka huo huo wa 1987, T.P.OK. Jazz ilialikwa kwenye Michezo ya Nne ya Afrika huko Nairobi, Kenya. Ni mwaka huo huo 1987, alitoa albamu ya Les On Dit, ikiwa na nyimbo nane.
Franco alitangaza kujiunga katika bendi yake kwa waimbaji wawili wa kike, Nana Akumu na Baniel Bambo.
Waimbaji hawa wanasikika vyema wakijibizana na Franco pamoja na kiitikio cha Madilu System katika wimbo maarufu wa Flora, une femme difficile (Flora, mwanamke mgumu). Tazama mashairi yake na tafsiri yake nimeiweka kwa Kiswahili kwenye mabano:

Mwanamume: Flora okosi ngai vraiment, kopesa addresse ya Balala pe zone olandaka Oh! Oh! Flora
(Flora hivi kweli umenidanganya na kunipa anuani ya uongo ya mahali unapoishi kweli, Flora).
Mwanamke: Nabangaki nabangaki kopesa yo addresse mobali na ngai azalaka matata oh! Dieu.
(Niliogopa niliogopa kukupa anuani ya kweli, mume wangu ni mkali sana oh! Mungu wangu).
Mwanamume: Kasi nasala boni lokola naluli yo, sala noki noki ngai nayo tokutana.
(Sasa nitafanyaje wakati ninakupenda, fanya juhudi zako basi mimi nawe tukutane).
Mwanamke: Naboyi na ngai, yo oza na mwasi nayo, ngai pe nazali na mobali na ngai oh! Dieu.
(Nasema sitaki, wewe una mke wako, mimi nina mume wangu, oh! Mungu wangu).
Mwanamume: Sala ngai plaisir, tokutana tosolola, nayebi oko reggrete moke te Flora.
(Naomba unifurahishe japo mara moja, tukutane tuzungumze, nakuahidi hutajutia Flora).
Mwanamke: Nayebi maloba ya mibali ya mikolo oyo eeh! Kasi po na ngai nazali occupe.
(Najua maneno ya wanaume wa siku hizi eeh! Sina muda wa kukutana nawe.)
Mwanamume: Flora, nalingi na pesa yo likolo na bomengo nanse, banana bazali kosenginya yo, Flora?
(Flora, nitakupa pesa uwe na maisha mazuri hapo duniani, hivi ni nani anayekudanganya, Flora?).
Mwanamke: Na moke azuaka na moke apesaka ngai wana ekoki na ngai oh! Dieu.
(Kwa kile kidogo akipatacho na kile kidogo anipacgo mume wangu nimeridhika oh! Mungu wangu).
Mwanamume: Est ce que okoki kolakisa ngai mobali nayo, natale soki aleki ngai na nini?
(Huwezi kunionyesha huyo mume wako siku moja ili nione amenizidi nini?).
Mwanamke: Est ce que yo! Pe okoki kolakisa ngai mwasi nay o natale soki naleki ye na nini?
(Hivi na wewe huwezi kunionyesha mke wako, ili nione nimemzidi nini?)

Naam. Ukiusikiliza wimbo huu utaamini jinsi ulivyopangiliwa vizuri kwa mashairi, vyombo na sauti mwanana za waimbaji.


IMETAYARISHWA NA www.maendeleovijijini.blogspot.com. Ukirejea ni lazima eleze chanzo ambacho ni www.maendeleovijijini.blogspot.com.

Comments