- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na Daniel Mbega
Badibanga
wa Tshilumba ‘Kai Kai’ (alizaliwa mwaka 1946, Mbuji Mayi, Mashariki wa Congo)
alikuwa mwanamuziki wa Congo aliyepitia katika bendi nyingi akiwa mtunzi,
mwimbaji na mpiga tumba, tarumbeta na trombone.
Maisha yake ya awali
Mwaka 1966
alijiunga na Jeshi la Congo (ANC) ambako alijiunga na bendi ya jeshi hilo akiwa
anapiga tarumbeta na trombone.
Mnamo
mwaka 1968 alijitoa kwenye jeshi na kujiunga na Orchestra Lupa Jazz iliyokuwa
na maskani yake mjini Lubumbashi, wakati huo ukijulikana kama Elisabethville
ambako alitunga nyimbo kama Tatu Kalonji na Tikela Ngay ye.
Katika
mwaka 1970 aliyekuwa anapiga muziki wa Congo nchini Zambia alimwita Kai Kai
aende Zambia na kujiunga na Orchestra Micky Jazz iliyokuwa ikitumbuiza kwenye
ukumbi wa La Gondola jijini Lusaka.
Mwaka 1972
bendi ya Micky Jazz ilikwenda kwa ziara jijini Dar es Salaam, ambako Ndala Kasheba
alimuona Kai Kai na kumtaka ajiunge na bendi yao ya Fauvette Jazz. Ndala
Kasheba na Micky Kalonda walikuwa anafahamiana tangu wakiwa mjini Likasi, mji
ambao wakati huo uliitwa Jadotville.
Baadaye akajiunga na bendi ya Baba
Nationale iliyokuwa chini ya Baba Gaston ambayo ilikuwa inakusudia kufanya
ziara nje ya Congo.
Kai Kai alikuwa mmoja wa wanamuziki waliokuwa katika kundi
la Baba Gaston Ilunga wa Ilunga lililoondoka Congo na kwenda Afrika Mashariki
kutafuta maisha, na walipokewa vyema Dar es Salaam na bendi hiyo kurekodi
nyimbo kadhaa katika studio ya TFC.
Hatimaye
kundi hili lilihamia Nairobi na kuwa likifanya maonyesho Park Restaurant
iliyoko Uhuru Park, na hapo ndipo walipokuja na kibao Kakoele Viva Christmas ambamo Kanema wa Kanema anasikika
akilalamika kwenye wimbo huo maarufu.
Wakati
Baba Gaston anamchukua kwa Ndala Kasheba alimuahidi kwamba angempatia Dola 100
ndipo wakaondoka kwenda Dar es Salaam.
Lakini mpaka walipofika Nairobi, Baba
Gaston hakuwa amemlipa hiyo fedha, hivyo Kai Kai na Nana Akumu wa Kudu (mwanamuziki
aliyeitikia katika wimbo wa Mamou wa T.P. O.K. Jazz), Kalenga Nzaazi ‘Vivi’,
Coco Mukala na wengineo wakamkimbia Baba Gaston na kuunda kundi la Mangelepa
lililojaa wanamuziki Wacongo watupu.
Mwaka 1976
baada ya kuondoka katika bendi ya Baba National akiwa na Soliste Bwami Walumona
Capitaine, Kasongongo wa Kanema, Evani Kabila Kabanze (mpwa wa Rais wa zamani
wa Congo hayati Laurent Kabila), Kalenga ‘Vivi’ Nzaazi, Lutulu, Kaniki Macky,
Twikale wa Twikale wakaanzisha bendi ya Les Mangelepa ambapo Kai Kai aliibuka
na nyimbo za Walter, na Bibi.
Umaarufu
wa Les Mangelepa ulifanya vikundi vingi vya wanamuziki wa Congo kuhamia Nairobi,
hivyo kukaweko na makundi kama Les Kinois, Super Mazembe, na Viva Makale, Shika
Shika na mengine mengi na kufanya biashara kuwa ya mashindano magumu ya
kimuziki, ukichukulia pia kulikuwa na bendi kama Simba wa Nyika, Les Wanyika,
na bendi za Wakenya kama Maroon Commandoes, Kilimambogo Boys na kadhalika.
Kati ya mwaka
1985 na 1986, bendi hiyo ilifanya ziara katika nchi za Djibouti, Malawi, Zambia
na wakiwa huko wakapata matatizo na bendi ikasambaratika. Kai kai alibakia
nchini Zambia kwa muda kabla ya kuhamia Afrika Kusini, wakati wanamuziki
wengine wakarejea Nairobi baadhi yao wakajiunga na bendi ya Cheers Boys
iliyoutwa na Wacongo ikiwa katika mji wa Kitwe.
Kai Kai
ndiye aliyetunga wimbo maarufu wa Nyako
Konya wa Orchestra Les Mangelepa, bendi iliyotingisha anga la muziki la
Afrika Mashariki na Kati enzi hizo ikitamba pia na vibao maarufu kama Embakassy, Walter, Maindusa.
Mauti
Badibanga
Wa Tshilumba Kai Kai alifariki Jumatatu, Februari 2, 2015 nchini Afrika Kusini na
akazikwa Johannesburg Februari 7, 2015 na kuzikwa.
Imeandaliwa
na www.maendeleovijijini.blogspot.com.
Ukinakili tafadhali taja chanzo hiki.
Comments
Post a Comment