Featured Post

WAZIRI JENISTA, NAIBU WAZIRI DKT. KALEMANI WAZINDUA MRADI WA USAMBAZAJI UMEME VIJINI REA III KWA KUGAWA VIFAA MKOANI RUVUMA



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe.Jenista Mhagama, akikabidhi kifaa kijulikanacho kama umeme tayari(Ready Board) kikichobuniwa na Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO),  kwa mwanakijiji wa kijiji cha Litapwasi, Peramiho, Mkoani Ruvuma wakati wa uzinduzi wa mradi wa Usambazaji umeme vijijini unaoratibiwa kwa pamoja na Wakala wa Umeme Vijijini REA na Shirika la Umeem Tanzania , (TANESCO), ambapo uzinduzi huo ni awamu ya tatu. Uzinduzi huo ni mwendelezo wa kazi kama hiyo ulioanzishwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medad Kalemani(aliyeshika vipaaza sauti) kwenye mikoa mbalimbali nchini.


NA MWANDISHI WETU SONGEA.
KAMPENI ya kuhakikisha vijiji vyote nchini vinapatiwa umeme, imeendelea jana (Agosti 16, 2017), mkoani Ruvuma, ambapo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, amezindua  mradi huo kwenye kijiji cha Litapaswi, wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma, kwa kugawa vifaa vijulikanavyo kama umeme tayari (Ready Board) kwa wanakijiji.
Katika hafla ya uzinduzi huo, uliofanywa kwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu), Mheshimiwa Jenista Mhagama, Wanakijiji walipatiwa vifaa hivyo vinavyowezesha umeme kuwaka mara moja bila ya kuhitaji (mtandao wa waya kwenye nyumba- (Wiring).
“Kifaa hiki ni maalum kwa matumizi ya nyumba isiyozidi vyumba viwili na mwanakijiji analipia shilingi elfu 36,000 tu kupata kifaa hiki.” Amefafanua Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji ambaye anafuatana na Naibu Waziri kwenye ziara hiyo.
Hali kadhalika alisema, kifaa hicho kwa sasa kinapatikana kwenye ofisi zote za TANESCO za Mikoa na Wilaya kwenye mikoa ambayop tayari mradi huo umezinduliwa.
Alisema, tayari Naibu Waziri amekwishazindua mradi kama huo kwenye mikoa yote ya Tanzania bara isipokuwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, na Katavi.
“Jambo la kufurahisha sana ni kwamba mradi huu wa REA III, unafadhiliwa na Serikali yetu kupitia Wakala wa Nishati Vijijini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)” alifafanua Bi. Muhaji.




Comments