Featured Post

MAANDALIZI MECHI YA SIMBA NA YANGA NGAO YA JAMII YAMEIVA


Maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii utakaowakutanisha Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2016/17, Young Africans na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup), Simba yanakwenda vema.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kuwatangazia umma kuwa viingilio katika mchezo huo vimepangwa katika makundi manne.

Sehemu ya VIP ‘A’ tiketi zake ni Sh 25,000; sehemu ya VIP ‘B’ na ‘C’ Sh 20,000; Viti vya Rangi la Chungwa Sh 10,000 na mzunguko kwa vitu vya rangi za bluu na kijani ni Sh 7,000.

Tiketi zimeanza kuuzwa leo Jumanne Agosti 15, 2017 ili kuwapa fursa wadau wa mpira wa miguu kununua tiketi mapema kujipeusha na usumbufu.

Wakati huo huo, Viongozi wa Klabu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL), wanatarajiwa kuwa na kikao na uongozi wa Bodi ya Ligi (TPLB), kitakachofanyika Ijumaa Agosti 8, 2017 kuanzia saa 3.00 asubuhi kwenye Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kitakuwa maalumu kwa ajili ya kujadili Ligi Daraja la Kwanza lakini pia kutoa semina kwa viongozi hao kuhusu Leseni za Klabu (Club License).

TFF inatoa wito kwa viongozi wa juu wa klabu kuhudhuria kikao hicho muhimu. TFF ingependa kusisitiza kuzingatia muda wa kuanza kikao.

Comments