Featured Post

DR. DALLO: OLE WAKE MGOMBEA ATAKAYEKWENDA KINYUME NA SHERIA YA UCHAGUZI


Na Woinde Shizza, Arusha



Wagombea wa nafasi mbalimbali za ungozi ndani ya chama cha mapinduzi wilaya wa Arusha wametakiwa kufuata kanuni na sheria za zilizowekwa  na chama hicho.



Hayo yamebainishwa na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Arusha Dr, Ramathani Dallo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na  tuhuma za kuwepo na baadhi ya wagombea kuja kwenye usahili na watu wanaodaiwa sio wagombea bali ni waganga wa kienyeji.



Alisema kuwa ni muhimu sana wagombea wakifuata kanuni taratibu na sheria zilizowekwa  katika uchaguzi  kwa mujibu wa kanuni ya  muongozo wa uchaguzi ya mwaka 2010



Alisema kuwa yeye binafsi ajawaoana watu hao wanaodaiwa ni waganga wa kienyeji na usahili  ulienda vizuri na k atika kipindi hichi  uchaguzi unaendelea vyema ,huku akibainisha kuwa iwapo kutakuwa na mgombea yeyote ambae atakwenda kinyume na sheria ya uchaguzi atamuaonea huruma bali atuakali zidi yake itachukuliwa .



“nasema kwakweli ili swala na mgombea  wa UWT kuja na mganga wa kienyeji kwenye usaili sijaliona ila ukweli napenda kuchukua nafasi hiii kuwasihi iwapo tutamkamata mgombea yeyote Yule anaekwenda kinyume na sheria tutamchukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuinta kikao kama jambo ni gumu sana pia itatulazimu tumkate jina lake na asiwepo kwenye kinyanganyiro chochote”alisema Dr,Dallo

Alizitaja baadhi yakanuni kuwa ni pamoja na kutofanya kampeni ,kukusanya watu kufanya mikutano isioyo rasmi kichama pamoja na  nyingi 



Aidha akiongelea baadhi za uchaguzi zilizopita alisema kwa upande wa uchaguzi wa kata ,mitaaa umemalizika vizuri sasa ivi ndio wanaendelea na maeneo mengine yaliyobaki



Awali baadhi ya wagombea ambao hawakutaka majina yao yaandikwe walisema kuwa kuna mmoja wa mgombea mwenza sik u ya usahili alikuja akiwa na mganga wa kienyeji kitu ambacho ni kinyume na sheria ya uchaguzi

Comments