Featured Post

MKUTANO WA KIMATAIFA WA SHUKRANI KUFANYIKA KESHO UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM

Muhubiri wa Kimataifa Dk.Nicku Kyungu akihubiri katika kongamano la siku mbili la viongozi wa dini lilifanyika Kanisa la Naoith Pentekoste Church Makuburi jijini Dar es Salaam leo kwa Askofu Dk. David Mwasota. Kongamano hilo linakwenda sanjari na mkutano wa kitaifa wa shukrani wa kuliombea taifa na Rais Dk.John Magufuli utakaofanyika kesho Uwanja wa Uhuru.

Mtumishi wa Mungu Askofu Mwaka kutoka nchini Zambia akihubiri katika kongamano hilo.
Askofu Timoth Joseph kutoka nchini Nigeria akihubiri  na kufundisha neno la mungu katika kongamano hilo.
Maaskofu na watumishi wa mungu wakiwa meza kuu wakati wa kongamano hilo.
Maombi yakifanyika.
Mchungaji Dk. William Kopwe wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania , kutoka Dodoma akiwa katika kongamano hilo na mkewe.
Viongozi wa dini maaskofu na wachungaji wakiwa kwenye kongamano hilo.
Maombi yakiendelea.
Kongamano likiendelea.
Taswira ya kongamano hilo.
Mwonekano  katika kongamano.
Watumishi wa mungu wakiwa katika maombi.
Utulivu katika kongamano hilo.

Na Dotto Mwaibale

KESHO Jumamosi maaskofu mbalimbali, viongozi wa serikali na taasisi na viongozi wa dini na wananchi watakutana Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maombi ya kitaifa ya shukrani ya kuiombea nchi na Rais Dk.John Magufuli.

Maombi hayo ya kihistoria yameandaliwa na viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali ya Huduma Tanzania na Taasisi ya I Go Africa For Jesus.

Katika maombi hayo yatakayofanyika kesho watumishi wa mungu kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwepo maaskofu watahudhuria.

Lengo kubwa la maombi hayo ni kuiombea nchi amani na  kumuunga mkono rais Dk.Magufuli ambaye amekuwa akiomba watanzania wamuombee mara kwa mara.

Kabla ya maombi hayo kwa jana na leo lilifanyika kongamano la viongozi wa dini ambapo watumishi wa mungu mbalimbali waliweza kufundisha mambo ya kiroho na somo la uaminifu na utunzaji wa fedha.

Muhubiri wa kimataifa 'Mama Afrika' Dk.Nicku Kyungu ameomba wananchi, viongozi wa dini kufika kuhudhuria maombi hayo bila kujali dini ya mtu kwani ni ya muhimu kwa nchi.

Alisema maombi hayo yanatoa fursa kwa kila mwananchi ya kuliombea taifa na kuwa yataanza saa tatu asubuhi hadi mchana ambapo kwaya mbalimbali zitakuwa zikitoa burudani ya nyimbo za kumtukuza mungu.



Comments