Featured Post

KAIMU MENEJA MKUU WA BANDARI YA KIGOMA AKANUSHA MADAI JUU YA KUTOKULIPWA WANANCHI 1228 WA ENEO KATOSHO

KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika  kikao cha menejimenti kilichofanyikia katika majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo hawajalipwa fedha zao kushoto ni Meneja wa Mawasiliano TPA Janeth Ruzangi.
KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika  kikao cha menejimenti kilichofanyikia katika majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo hawajalipwa fedha zao kushoto ni Maneja wa Mawasilino TPA Janeth Ruzangi
 PRO wa TPA Tanga Moni Jarufu akifuatilia mkutano huo
 Waanmdishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia matukio
 Waandishi wa habari wakiwa kazini kuchukua stori
KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza kushoto akimpa ufafanuzi mwandishi wa gazeti la Dail News Mkoani Tanga,Amina Kingazi
KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza amekanusha madai yanayoenezwa juu ya kutokulipwa wananchi 1228 wa eneo la Katosho katika Manispaa hiyo kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa bandari kavu ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 12 zimetengwa kwa ajili ya gharama za fidia.
 
Hayo ameyazungumza jana Jijini Tanga alipokuwepo kwenye kikao cha menejimenti kilichofanyikia katika majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo hawajalipwa fedha zao.

Aidha alisema jumla ya hekari 158 ndizo zilizochukuliwa na mamlaka ya bandari(TPA) kwa ajili ya mradi huo huku wananchi 1196 kati 1228 tayari wamekwisha lipwa fedha zao kama semehemu ya fidia za ardhi,mazao na makazi jambo ambalo limefanyika kwa mujibu wa kisheria na ushirikishwaji wa pande zote.
 
Mchindiuza alizidi kufafanua kuwa kutokana na hatua hiyo wananchi 32 kati yao walishindwa kulipwa fidia zao kutokana na kushindwa kuwakilisha akaunti zao katika Halmashauri ya manispaa ya Mji wa Ujiji jambo ambalo linapotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari.
 
“Yapo malalamiko mengi ya utaratibu wa ulipwaji wa fidia hizo kwa wananchi walioko katika maeneo ya ya maradi lakini labda niseme kitu tayari tumekwisha walipa wananchi 1196 kati 1228 na waliobakia ni 32 tu na fedha zao zipo wapeleke akauti zao tuweze kuwalipa”Alisema.

Alisema Mamlaka hiyo baada ya kukua kutokana na kuongezeka kwa shehena mamlaka ilitafuta eneo kwa ajili ya kujenga mradi wa bandari kavu ambalo litatumika kuhudumia nchi jirani za maziwa makuu kama DRC,Burundi na Rwanda.

Taratibu za kupatikana kwa eneo hilo ambalo lilikuwa mali ya wananchi katika eneo hilo la Katosho Mkoani humo zilifanyika kisheria na kuishirikisha Halmashauri ya Mji huo ambao wao ndio wanaozijua kaya zinazoishi katika maeneo hayo.
 
“Lengo letu la kuishirikisha Halmashauri ya manispaa hiyo ni
kuhakikisha wanafanya tathmini ya kina dhidi ya wananchi hao na tunatambua kuwa wanazitambua kaya zote zinazostahili kulipwa na hivi ndivyo tulivyo fanya”Alisema.

Hata hivyo aliwataka wananchi hao kama wanamadai kuhusiana na kiwango kidogo cha fidia wanaweza kufika katika mamlaka za sheria za ardhi na kufuata mkondo wa sheria ili waweze kupata msaada wa kisheria zaidi.
 
“Wananchi wasipotoshwe na wajanja wajanja idadi ya wafidiwa
inatambuliwa na na kama kuna kitu hakijafuatwa wafuate sheria ili mkondo huo uchukue maamuzi ya kisheria bila ya kuonea mtu na sisi kama viongozi wa mamlaka tupo salama na kwa wale ambao hawajalipwa wafike na vielelezo katika ofisi husika wachukue fedha zao.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi hao waache kupotoshwa na watu wachache ambao hawataweza kuwasaidia kitu chochote jambo la msingi kujenga ushirikiano katika miradi hiyo ya maendeleo ya Taifa.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Comments