Featured Post

WAHAMIAJI HARAMU 45 WAKAMATWA WILAYANI MKINGA

IDARA ya Uhamiaji Mkoani Tanga imewakamata wahamiaji haramu 45 kutoka nchini Ethiopia katika Kijiji cha Horohoro wilayani Mkinga mkoani Tanga kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa shambani kwa wananchi wanakula mahindi kabla ya kutiwa nguvuni.

Licha ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao lakini pia idara hiyo inamshikilia raia mmoja kutoka nchini Kenya ambaye ndio alikuwa akiwaongoza wahamiaji haramu hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari,Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Crispin Ngonyani alisema wahamiaji haramu hao walikamatwa June 18 mwaka huu katika kijiji hicho baada kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema  wa eneo hilo.

Alisema wahamiaji haramu hao walikamatwa wakiwa porini katika jiji hicho wakati wakisafiri kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo waligunduliwa na wananchi baada ya kufika mashambani mwao wakawakuta wanakula mahindi ndio walipotoa taarifa kwa askari wa Polisi wa Horohoro na hivyo wakaenda kuwakamata.

Aliwataja wahamiaji haramu hao kuwa ni Melesa Manesha, Asaf
Erisid,Ashnif Agide,Mulugeta Menano,Demek Sorebeto,Samal
Latbo,Temesgen Tefera,Tememi Juheri, Mubarc Lamago, Temesa
Kibemo, Haftamu Tumiso,Teshum Assfe,Yohanness Ayano na Daniel Abbate.

Aidha Ofisa Uhamiaji huyo aliwataka wengine walio kamatwa kuwa ni Kibmam Abab,Temesgzeen Ayele, Akilu Abraham, Pxirose Makore, Munyasha Lombaso, Berekei Cezenzeni, Detebo Erikato, Ayele Kebamo, Tamrat Mamo.

Wengine waliokamatwa kuwa ni Saniel Wolde,Tomiot Deto Gem, Abeje Alemeyo, Ashenaf Waje, Tariko Dutamo, Birhanu Atso, Tesefaye Dena, Tekel Abush, Tesyfe Landu na Abdi Hassani.

Kwa mujibu wa ofisa uhamiaji huyo aliwataja wengine kuwa ni Daafa Daimo, Getahun Zeleke, Yonas Liliso, Amanei Ashebo, Xesabo Womago, Isagay Tikie Mubarik Analo, Begaye Ganorem, Dawit Teso, Teshele Kemiso,Samweli Hyle na Tamasgen Sorsa.

Alisema wahamiaji haramu hao wamefikishwa mahakamani jana kujibu tuhuma zinazowakabili akiwemo msindikizaji  Mongela Kidhome ambaye ni Mkenya na mkazi wa mpakani mwa Kenya na Tanzania Horohoro.

Hata hivyo aliwataka mawakala wa wahamiaji haramu kuacha mara moja vitendo vya kuwaingiza nchini kwani watakaobainika watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kujibu tuhuma zinazowakabili.
 Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Comments