Featured Post

TGGA YAENDESHA KAMBI YA MAFUNZO YA MTOTO WA KIKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI

 Washiriki wa Kambi ya Mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wakiimba wimbo wa Taifa baada ya kujifunza jinsi  ya kufunga kamba vifundo na kupandisha bendera ya Taifa katika kambi ya siku tano iliyoandaliwa na Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Mombasa, Dar es Salaam.
 
 Wakiimba wimbo wa Taifa

 Walimu na viongozi wa chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), wakijenga mahema kwa ajili ya kambi  ya kumjengea uwezo mtoto wa kike yaliyoandaliwa na TGGA, Mombasa, Dar es Salaam jana. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Wakitundika vikombe kwenye matawi
 Wapika chakula
 Wakiwa kwenye kalo la kuoshea vyombo waliliolitengeneza wenyewe
 Sehemu ya kutupia taka
 Usafi eneo la vyoo
 Kamishna Msaidizi wa TGGA Mkoa wa Tanga, Fatuma Juma akiwafundisha washiriki jinsi ya kufunga vifundo vya kamba vinavyoo kwa daraj, bendera na mapambo hotelini
 Wakiunga vifundo hivyo
 Washiriki wakiwa busy kujifunza kufunga vifundo
 Fatuma akiwasimamia washiriki
 Sehemu ya kambi ambamo Girl Guides hao wanalala
 Fatuma ambaye ni Msimamizi wa kambi hiyo akimwelekeza kufunga vifundo mmoja wa washiriki
Wakijifunza kufunga vifundo kwenye mti


Na Richard Mwaikenda 
MAFUNZO ya kujiamini na kujitambua kwa mtoto wa kike yamepamba moto katika kambi maalumu inayoendelea eneo la Mombasa, Ilala, Dar es Salaam.

Kambi hiyo iliyoandaliwa na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), inashirikisha walimu na viongozi wa chama hicho kutoka  mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza na mwandishi wetu aliyetembelea kambi hiyo leo,
Kamishna wa TGGA,Mkoa wa Tanga, Modesta Mshata alisema kuwa lengo la kambi hiyo ni kuwajengea uwezo walimu na viongozi wa kujiamini na kujitambua.

"Tunata mtoto wa kike popote alipo ajiamini, ajitambue na kuwa jasiri ikiwemo pia kumudu maisha kwa kushirikiana vyema na jamii inayomzunguka."Alisema Mshata.

Pia alisema kuwa, lengo ni kumfundisha mtoto wa kike kuwa mama na kiongozi bora wa familia na taifa kwa ujumla.


Washiriki 36 wa kambi hiyo ya siku tano wanatoka Kondoa, Dodoma, Tanga, Lindi, Rukwa na Dar es Salaam pamoja na nchi za Uganda, Rwanda na Madagascar.

Naye Emiliana Stanslaus ambaye ni  Mkufunzi Mkuu wa mafunzo kutoka Makao Makuu ya TGGA, alisema kuwa lengo la kambi hiyo ni kutoa mafunzo kwa washiriki ili wakirudi mikoani wakawafundishe watoto wa kike.

Alisema washiriki hufundishwa jinsi ya kutengeneza karo, bafu, shimo la uchafu, kichanja cha kuanikia vyombo, kamba ya kuanikia nguo, sehemu ya kunawia mikono, sehemu ya kupata maji ya kuoga, kuandaa eneo la kulala, jiko na kufanya mazoezi mbalimbali ya viungo. 

Emiliana ambaye amewahi kuhudhuria Kambi ya Kimataifa ya Skauti wa kike nchini Norway, alisema kuwa kambi hiyo inakuwa kama ya kijeshi kwani hujifunza mambo mengi ya ukakamavu na jinsi ya kujiamini na kuwa na ujasiri katika mazingira yoyote.

Kiongozi wa Girl Guides, Rachel Baganyila kutoka Uganda, ambaye yupo nchini kwa mafunzo ya miezi sita ya kubadilishana uzoefu, alisema kuwa amefarijika sana kupata mafunzo hayo ambayo asilimia kubwa ni mapya na kwamba atakaporejea kwao atawafundisha wenzie.

Alisema kuwa amejifunza utamaduni wa kitanzania na masuala ya uongozi pamoja na jinsi ya kutengeneza mafundo yanayosaidia kupandisha na kushusha bendera ya taifa na kuiheshimu pia.

Sharifa Mkwango ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, alisema kuwa mafunzo aliyoyapata atahakikisha akirejea kwao atawafundisha watoto wa kike kuhusu ukakamavu, kufunga mafundo, alama za TGG, stadi za kazi na jinsi ya kuandaa kambi za mafunzo.

Comments