Featured Post

RC MAKONDA AKABIDHIWA MAGARI 26 YA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM KWA AJILI YA KUYATENGENEZA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akikagua gwaride wakati wa hafla ya kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, SACP Gilless B. Muroto akisoma taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam mbele ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa hafla ya kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam
Baadhi ya magari Mabovu yaliyokabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akifatilia hafla ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) na Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Mhe ally Happi (Kushoto) wakijadili jambo mara baada ya kumalizika hafla ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam
Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akiyakagua magari mabovu aliyokabidhiwa kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam
Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akiyakagua magari mabovu aliyokabidhiwa kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, SACP Gilless B. Muroto akitoa maelezo ya magari hayo mabovu mbele ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe Paul C. Makonda wakati wa hafla ya kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Happi, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare makori, na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg john Lipesi Kayombo mara baada ya hafla ya kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda sambamba na wanajeshi wa Jeshi La Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakishirikiana kusukuma gari bovu tayari kwa safari ya kuelekea Mkoani Kilimanjaro kwa matengenezo, wakati wa hafla ya kukabidhiwa magari mabovu kwa ajili ya Matengenezo. Leo June 14, 2017 Oysterbay Jijini Dar es salaam

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda leo June 14, 2017 amekabidhiwa magari mabovu 26 ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuyatengeneza kwa lengo la kuliongezea ufanisi jeshi la polisi katika kukabiliana na uhalifu katika Mkoa wa Dar es salaam.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya magari hayo iliyofanyika katika kituo cha Polisi  Oysterbay ambapo ameelekeza magari hayo yote kwenda Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya matengenezo pasina gharama za serikali, Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa serikali imedhamiria kulifanya Jiji la Dar es salaam kuwa salama zaidi ili wafanyabiashara, Wanunuzi, na wananchi wote kufanya kazi zao kwa amani masaa 24.

Alisema kuwa safari ya mabadiliko katika Jeshi la polisi imefanywa kila mara lengo ikiwa ni kulifanya Jeshi la Polisi kuwa na weledi zaidi na kuondoa dhana na mazoea ambayo imeanza kujengeka kati ya Jeshi la Polisi na wananchi jambo ambalo limepelekea uwajibikaji kupungua kwa baadhi ya Askari.

Rc Makonda alisema kuwa pamoja na Jitihada mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Polisi Jijini Dar es salaam katika kukabiliana na uhalifu lakini zipo changamoto mbalimbali ambazo kwa njia moja ama nyingine zinakwamisha kufikiwa kwa malengo huku akizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na Upungufu wa magari ya Doria,, Vifaa vya mawasiliano, Radio za mkononi na za magari, ufinyu wa bajeti ya mafuta na matengenezo magari.

Mhe Makonda ameyataja mambo manne ambayo ameamua kuyafanya ili kuliongezea nguvu jeshi la polisi katika kukabiliana na uhalifu ambayo ni pamoja na kufanya mchakato wa kutafuta Bastola 500, Vitanda pamoja na Radio Call, Baiskeli 500 pamoja na Pikipiki 200 kwa ajili ya Doria.

Kufunga Kamera kwenye vituo 20 vya Polisi Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kupata taarifa na kuondoa usumbufu na mianya ya Rushwa, Kuweka kompyuta 8 kwenye vituo 20 sambamba na kuzindua utaratibu wa wahalifu kupigwa picha pindi wanapoingia kituoni na taarifa zao kuwekwa kwenye mfumo wa kompyuta ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wahalifu.

mambo mengine ni pamoja na kuhakikisha Jeshi la Polisi linaondoa biashara zote haramu na Bandari Bubu sambamba na kufunga kamera za barabarani ili kubaini utovu wa nidhamu unaofanywa na madereva na kurahisisha upatikanaji haraka wa taarifa za uvunjaji wa sheria barabarani badala ya askari kukimbizana na madereva wanaovunja sheria.

Mhe Makonda pia amelielekeza Jeshi la Polisi kubaini maduka yote yanayouza vifaa vya magari na utambuzi wa mahali wanaponunua vifaa hivyo lengo ikiwa ni kubaini na kukomesha wizi wa vifaa vya magari unaofanyika katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es salaam.

Amewasihi wananchi kuendelea kutoa taarifa za kufichua wahalifu sambamba na kuiombea serikali inayoongozwa na Rais Magufuli ili kuvuka kipindi hiki kigumu cha kuwakabili wanyonyaji na wabadhilifu wa rasilimali za watanzania.


Mhe Makonda pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kumteua kamanda Simon Sirro kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) kwani kwa muda mfupi aliofanya nae kazi ameonyesha weledi mkubwa katika uwajibikaji hususani katika kuukabili uhalifu katika Kanda ya Kipolisi ya Dar es salaam.

Awali akisoma taarifa kuhusu Uhalifu katika Jiji La Dar es salaam kwa niaba ya Inspekta Jenerali wa polisi (IGP) na askari wote wa Mkoa wa Dar es salaam Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, SACP Gilless B. Muroto alisema kuwa hali ya uhalifu imepungua kutoka matukio 56,856 yaliyoripotiwa kwa mwezi Januari hadi Mwezi Mei mwaka 2017 ikilinganishwa na Matukio 59,695 yaliyoripotiwa katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Mwezi Mei mwaka 2016.

Kamanda Muroto Alisema kuwa Matukio makubwa ya jinai yaliyoripotiwa mwaka 2017 ni 5,879 ambapo mwezi Januari hadi Mwezi Mei 2016 kulikuwa na matukio 8,252 pungufu ya matukio 2,373 sawa na asilimia 28.7%.

Alisema kuwa kupungua kwa uhalifu sambamba na matukio makubwa ya jinai ni kutokana na juhudi mbalimbali za kudhibiti uhalifu zinazofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi ambapo Oparesheni mbalimbali hupelekea wahalifu kukamatwa kwa wingi.

Comments