Featured Post

RIWAYA TAMU: JENEZA KUTOKA HONG KONG (23)




Ilionekana kama ni muda mrefu tangu nilipoondoka jijini Pasadena. Safari yangu ilicheleweshwa kwa siku mbili kwa sababu ya yule kijana muuajji aliyenivamia nyumbani kwangu. Sikuwa nimemweleza Retnick kisa kamili. Nilimwambia kwamba niliingia nyumbani mwangu, nikamkuta kijana huyo na kuanza kupigana. Alikuwa anafanya nini pale, nikadanganya, kwamba sijui – pengine ni mwizi tu. Retnick hakuipenda hadithi hiyo. Hususan, hakupenda kuona kwamba kijana huyo alikuwa na kiwambo cha kuzuia sauti kwenye bastola yake, lakini nikasisitiza maelezo yangu kama yalivyo. Hatimaye nilifanikiwa kuondoka kuja Hong Kong na hicho ndicho kitu pekee nilichokuwa nakihofia.

Nilikuwa na uhakika kwamba mtu aliyemtuma yule kijana aniue anaweza kuwa ndiye John Hardwick. Nilikuwa nimenunua bastola nyingine .38 maalum kwa ajili ya Polisi. Nikajiambia kwamba kamwe sitathubutu kutembea bila kuwa nayo hapo baadaye: kitu ambacho nilijiapiza, lakini nikasahau haraka.
Bodi ikagonga ukingo wa upande wa pili na kila mtu, nikiwemo mimi mwenyewe, tukaanza kuteremka.
Wanchai lilikuwa ni eneo ambalo asilimia karibu mia moja lilikaliwa na Wachina. Zaidi ya Wamarekani wawili wenye maumbile makubwa aliokuwa wakitafuna bazooka na wakitazama pembeni, eneo lote la ufukwe na hapo bandarini lilisheheni Wachina, makuli wakiwa na mizigo, wauzaji wa mboga waliochuchumaa pembeni, watoto wa Kichina wakiwalea watoto wa Kichina, mabinti kadhaa wa Kichina waliokuwa wakinitazama kwa macho ya matamanio na vijana wa mikokoteni wallioshangaa baada ya kuniona.
Sandwiched between a shop selling watches and a shop selling cheap toys was the entrance to the Celestial Empire Hotel.
Nikiwa na begi mgongoni, nilifanikiwa kukatisha barabara bila kugongwa na kuanza kupandisha ngazi ndefu, nyembamba kuelekea mapokezi katika hoteli hiyo.
Kwenye dawati la mapokezi mwisho wa ngazi aliketi mzee wa Kichina akiwa amevalia kofia nyeusi na koti jeusi. Ndevu ndefu nyeusi zilifunika kidevu chake. Macho yake yalikuwa hayana hisia zozote.
“Ninahitaji chumba,” nilisema, nikiweka begi langu chini.
Alinitazama kuanzia juu hadi chini, akitumia muda mrefu kidogo. Sikuwa nimevalia suti yangu nzuri zaidi na shati langu lilikuwa limechafuka wakati nikiwa safarini. Sikuonekana kama mhuni, lakini hata hivyo sikuonekana kama mtu mwenye fedha.
Alivuta kitabu chenye umbile kama sikio la mbwa akanisogezea pamoja na peni. Kitabu hakikiwa na chochote zaidi ya alama za Kichina. Niliandika jina na utaifa wangu katika nafasi zilizostahili na kumrejeshea. Akachukua ufunguo uliotundikwa pembeni yake na kunikabidhi.
“Dola kumi,” akasema. “Chumba Namba Ishirini na Saba.”
Nikampatia dola kumi za Hong Kong, nikachukua ufunguo na aliponielekeza upande wa kulia, nikaondoka, nikibeba begi langu. Katikati ya korido mlango ulifunguliwa na baharia Mmarekani mweupe, mwembamba, akatoka mbele yangu. Hakukuwa na nafasi ya kupitia hivyo nikabana upande mmoja na kusubiri apite. Nyuma yake akatokea msichana wa Kichina akiwa amevaa nguo ya rangi ya pinkki ya Cheongsam, uso wake ukionekana kuchoshwa. Akanikumbusha taswira ya mbwa aliyelishwa vizuri wa aina ya Pekin. Baharia akapita pembeni yangu, akiwa anajifyonya. Yule msichana akamfuata. Nikaendelea mbele hadi nilipofika kwenye chumba namba ishirini na saba. Niliingiza ufunguo kwenye kitasa, nikafungu na kuingia kwenye chumba chenye ukubwa wa futi kumi kwa kumi kikiwa na kitanda kipana cha watu wawili, kiti kimoja, kabati, bakuli la kunawia lililoegeshwa kwenye samani nzuri, zuria lililochakaa na dirisha ambalo lilionyesha mandhari ya jengo linguine ambalo inawezekana lilikuwa kwa ajili ya kufulia nguo, kwa kuangalia mataulo, mashuka na chupi za aina tofauti zilizotundikwa kwenye mianzi iliyoonekana kutoka dirishani.
Niliweka begi langu chini na kujibwaga kitandani. Nilikuwa natokwa jasho na kuhisi uchovu mno. Ningekuwa nimefurahi zaidi kama ningefikia kwenye hoteli ya Gloucester au Peninsular ambako ningeoga vizuri na kupata bia baridi, lakini hii ilikuwa safari ya kikazi, siyo utalii. Sijui mbali kote huku kujiingiza kwenye starehe. Hapa ndiyo mahali Herman Jefferson na mkewe Mchina waliishi. Kama kwao palikuwa mahali pazuri, basi patakuwa pazuri pia kwangu.
Baada ya muda, jasho likapungua. Nikamimina maji kwenye beseni na kwenda kuoga. Baadaye nikatoa vitu vyangu kwenye begin a kuweka kabatini. Hoteli ilikuwa kimya mno. Niliweza kusikia miungurumo ya magari kwa mbali, lakini hakuna cha zaidi. Nilitazama saa yangu ya mkononi. Ilikuwa saa kumi na mbili kasoro dakika ishirini. Niliiona kadi ambayo yule Mchina mfupi alinipatia ikiwa kwenye mkanda wa saa na kuichomoa ili kusoma maelezo. Ilisema: Wong Hop Bo. Mwongoza watalii anayezungumza Kiingereza. Kulikuwa na nambari ya simu. Nikaiweka kadi hiyo kwenye pochi yangu, halafu nikafungua mlango, na kutoka nje kwenye korido.
Itaendelea kesho…

Comments