Featured Post

MAKAO MAKUU OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU KUKAMILIKA BAADA YA MIEZI KUMI



Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Albina Chuwa akitoa maelekezo wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi hiyo unaondelea Mkoani Dodoma leo (jana), wa kwanza kulia ni Injinia Lan Shuiqing kutoka Kampuni ya Hainan Internationa.(Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).




Benjamin Sawe – Maelezo, Dodoma
MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dk. Albina Chuwa ametaka ujenzi wa makao makuu ya ofisi hiyo unaoendelea mjini Dodom ukamilishwe kwa wakati.
Akizungumza mjini hapa jana baada ya kukagua ujenzi wa ofisi hiyo, Dk. Chuwa alisema ni wakati sasa kwa NBS kuwa na ofisi yenye hadhi kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha shughuli za takwimu nchini.
Dk. Chuwa alisema NBS ni miongoni mwa taasisi kongwe nchini na ambayo imekuwa ikibadilika na kwenda na wakati hivyo kupatikana kwa jengo hilo ni jambo linalopaswa kutimia haraka.
“Jengo letu ni la ghorofa tano tu, kwa kuwa mkandarasi umepewa muda wa miezi 10 sioni sababu ya kuchelewa kukamilishwa.
“Hivi karibuni nilizungumza na wenzetu wa Uganda wao walijenga jengo lao la ghorofa 12 kwa mwaka mmoja tu sasa sioni sababu kwa nini letu lisikamilike kwa wakati,”alisema.
Kwa mujibu wa Dk. Chuwa jengo hilo litakuwa ni la ghorofa tano na kwamba kwa kuwa wanazo ofisi katika kila mkoa nchini, makao makuu hayo yatatumika kuratibu uendeshaji wa shughuli za takwimu na mambo mengine ya maendeleo yanayohusiana na NBS.
Dk. Chuwa alisema jengo hilo litagharimu sh. Bilioni 11.6 hadi kukamilika kwake fedha ambazo zinatokana na mkopo kutoka Benki ya Dunia.
Kwa upande wake, Msimamizi Mkuu wa ujenzi huo, Mtumwa Shomvi kutoka kampuni ya Y&P Achtects Limited, alisema watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu katika kuusimamia mradi huo.
Shomvi  alisema jukumu kubwa wanalolisimamia ni kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati, gharama na ubora uliokubaliwa.
Aidha, Msimamizi kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo ya Hainani International Limited ya China, Lan Shuiqing alisema kazi ya ujenzi inaendelea vyema na kwamba anaamini kila kitu kitakamilika kwa wakati.

 Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Albina Chuwa akitoa maelekezo wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi hiyo unaondelea Mkoani Dodoma leo (jana).(Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
 Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Albina Chuwa akitoa maelekezo wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi hiyo unaondelea Mkoani Dodoma leo (jana), wa kulia ni Mkurugenzi wa Kampunu ya Anova Consult  Injinia Kitery Kamaley.(Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).
 Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Albina Chuwa akitoa maelekezo wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi hiyo unaondelea Mkoani Dodoma leo (jana),katikati ni Mkurugenzi wa Kampunu ya Anova Consult  Injinia Kitery Kamaley.(Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).
 Msimamizi Mkuu kutoka Kampuni ya Y and P Bw. Mtumwa Somvi wa kwanza kulia akitoa maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Albina Chuwa wakati menejimenti ya Taasisi hiyo ilipokagua  maendeleo ya ujenzi  mkoani Dodoma leo (jana).(Picha na Benjamin Sawe -Maelezo.
 Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu lenye urefu wa ghorofa tano linaloendelea kujengwa Mkoani Dodoma.(Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).
Muonekano wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu unavyoendelea mkoani Dodoma.(Picha na Benjamin Sawe -Maelezo)


Comments