Featured Post

KAMPUNI YA TATA YAWAFADHILI WATANZANIA KWENDA NCHINI INDIA KWA MAFUNZO YA KUTENGENEZA MAGARI

 Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla (kulia), akizungumza Makao Makuu ya Kampuni hiyo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam jana, wakati wa  hafla ya kuwaaga vijana wanne wa kitanzania ambao wanakwenda nchini India kwa mafunzo ya miezi tisa ya kutengeneza magari. Kutoka kushoto ni viongozi wa kampuni hiyo, Sarvan Keshri na Udayagiri Veeru.

  Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla (kulia), akisisitiza jambo.
 Mgeni rasmi katika hafla fupi ya kuwaaga vijana hao Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu Masingi akizungumza katika hafla hiyo. Kutoka kushoto ni mmoja wa viongozi wa kampuni ya Tata, Udayagiri Veeru na Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla.
 Viongozi wa kampuni hiyo ukitoa zawadi ya ua kwa mgeni rasmi Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu Masingi.
 Viongozi wa kampuni hiyo mgeni rasmi, wazazi na ndugu wa vijana hao wakiwa katika picha ya pamoja.
  Mgeni rasmi katika hafla fupi ya kuwaaga vijana hao Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu Masingi (kulia), akikabidhiwa zawadi ya picha ya tembo na viongozi wa kampuni hiyo. Kutoka kushoto ni Udayagiri Veeru na Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania, Prashant Shukla.
 Mama wa msichana pekee anayekwenda kupata mafunzo hayo, Fatma Mussa Ngulangwa (kushoto), akimkabidhi binti yake, Mariam Shamte maua ikiwa ni ishara ya kumuaga.
 Fr.Lucas Wakuganda akimkabishi maua mtoto wake anayeondoka kwenda masomoni nchini humo.
 Mhitimu wa mafunzo hayo, Osmund Kapinga (katikati), akiwa amewainua mikono vijana hao ikiwa ishara ya kuwaaga. 
 Mkufunzi wa mafunzo wa kampuni hiyo, Oscar Mwakagenda (kushoto), akitoa maelekezo ya injini za gari zinazofanya kazi mbele ya mgeni rasmi na uongozi wa kampuni hiyo.
 Ni furaha tupu katika hafla hiyo.
Viongozi wa kampuni hiyo mgeni rasmi, wazazi na ndugu wa vijana hao wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya karakana ya mafunzo.
Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Tata imetoa ufadhili kwa vijana wanne wa kitanzania kwenda nchini India kujifunza utengenezaji wa magari.

Kati ya vijana hao msichana ni mmoja ambapo wanatarajia kuondoka nchini kesho kuelekea mji wa Jamshedpur nchini humo kwa mafunzo ya miezi tisa kupitia mpango wa Skill pro- International Business Commarcial Vehicles Skill Development Program.

Mgeni rasmi katika hafla fupi ya kuwaaga vijana hao Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masatu Masingi akizungumza Dar e Salaam jana aliwataka vijana hao wakiwa nchini humo kuwa mabalozi wa kutangaza sifa nzuri ya Tanzania na si vinginevyo.

"Tumieni fursa hii mliyoipata  kwenda kusoma na kuitangaza nchi yetu msiende kucheza na kututia aibu kwani katika vijana 25 kutoka nchi mbalimbali za Afrika nyie wanne ndio mnaiwakilisha nchi yetu" alisema Masingi.

Masingi aliishukuru kampuni hiyo kwa kuwawezesha vijana hao na kuahadi serikali kushirikiana nayo ili kupanua soko la ajira kwa vijana nchini.

Mkuu wa Kitengo cha Magari wa Kampuni ya Tata Tanzania Prashant Shukla alisema hii ni awamu ya tatu kwa kampuni hiyo kupeleka vijana nchini India kujifunza kutengeneza magari ambapo kwa awamu ya kwanza hakuna kijana wa kitanzania aliyehudhuria mafunzo hayo.

Alisema kwa awamu ya pili alipelekwa mtanzania Osmund Kapinga ambaye aliibuka kuwa mwanafunzi bora na katika awamu hii ya tatu wanakwenda hao wanne.

Alisema lengo la kuwapeleka vijana hao nchini India ni kujifunza kazi hiyo ili nao wakirudi waweze kuwa walimu wa wenzao hivyo kuisaidia serikali kukuza ajira nchini hasa kwa vijana.

Alisema kampuni hiyo kwa Tanzania inafanya kazi  mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza lakini wanatarajia kwenda mkoani Mbeya kufungua tawi na baadae itafuatia  mikoa mingine ambapo vijana wanaopata mafunzo kupitia mpango huo wataenda kuwafundisha wenzao.

Mhitimu wa mafunzo hayo nchini humo Osmund Kapinga alisema kampuni hiyo ni kubwa na mbali ya kutengeneza magari ya aina zote inavitu vingi inavyo tengeneza hivyo aliwasihi wenzake wanaoondoka kuchangamkia fursa hiyo hadimu ili wakirudi waweze kuwasaidia watanzania wenzao.

Vijana waliopata fursa ya kwenda kupata mafunzo hayo ni Mariam Hemed Shamte, Anord Peter Nditu, Elias Jones Tette na Adam Abdallah Pwimu.


Comments