Featured Post

WIZARA YA MALIASILI YATOA MAFUNZO YA KIJESHI KWA MAAFISA WAKE

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence S.
Milanzi


Na Twaha Twaibu, Katavi
WIZARA ya Maliasili na Utalii imewaasa maofisa vijana wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) waliohitimu mafunzo yanayowaandaa kuingia kwenye mfumo wa Jeshi Usu, wasijihusishe na  biashara haramu ya wanyamapori na mazao ya misitu.

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ni mamlaka iliyoanzishwa kwa Amri ya Serikali na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali Na.135 la tarehe 9 Mei, 2014. Uanzishwaji wa Mamlaka hii ni utekelezaji wa kifungu cha 8 cha Sheria ya kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009.
Mamlaka ya Wanyamapori imeanza kazi rasmi tarehe 1/Julai/2016. Makao makuu yake kwa sasa yapo Morogoro katika jengo la Taasisi ya utafiti wa mazao ya misitu (TAFORI).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi amewataka wahitimu wa mafunzo hayo  wasijichukulie sheria mikononi kuwaadhibu watuwanaobainika kuingia ndani ya Mapori ya Akiba, bali wawakamate na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria  ili sheria ichukue mkondo wake.

alitoa nasaha hizo wakati akifunga mafunzo ya wiki sita ya kuwaandaa watumishi wa wizara hiyo kuingia kwenye mfumo wa kijeshi (Jeshi Usu) katika hafla iliyofanyika tarehe 11/3/2017 kwenye Kituo cha Mafunzo kilichopo wilayani Mlele Mkoani Katavi.

Mafunzo hayo yalianza Januari 30, mwaka huu 2017 kwa maofisa 100 kati yao,
99 wakiwa ni kutoka TAWA na mwingine ni ofisa kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa). Waliohitimu na kuwa tayari kwa majukumu walikuwa 99.


 
Katibu Mkuu aliwaeleza wahitimu kuwa, ‘ Mimi binafsi natambua kuwa mafunzo haya hayakuwa rahisi kwenu haswa ukizingatia wengi wenu kama siyo wote, hii ndiyo mara yenu ya kwanza kupata mafunzo kama haya,lakini kwa dhamira nzuri na yenye mtazamo chanya mliyokuwa nayo imepelekea wote kumaliza salama. Ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yatasaidia kuimarisha nidhamu kwenye maeneo yetu  ya kazi katika kipindi hiki tunachojianda kuingia katika mfumo wa kiutendaji wa jeshi usu’’ Nanukuu.
Katibu Mkuu aliendelea kuwaeleza kwamba, lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kuongoza watumishi walio chini yao ambao wengi ni askari.wakati wahitimu hawa wengi wao hawajapata mafunzo ya kijeshi tangu wamalize elimu yao ya chuo kikuu. Katibu Mkuu alisema ,majukumu waliyopewa ni makubwa ambayo lengo lake ni kuwaanda kuwa wahifadhi wakuu na baadaye. Hivyo ni vyema wakatambua kuwa baada ya mafunzo haya wanajukumu yanawasubiri mbele yao.
Katibu Mkuu alisisitiza kwenye  hotuba yake kwa kusema kwamba, Wizara ya Malaisili na Utalii itaendelea na hatua za kuanzisha mfumo wa Jeshi Usu katika sekta za wanyamapori na Misitu. Hivyo, mpanmgo wa kutoa mafunzo haya ni endelevu na yatatolewa kwa watumishi wote wanaohusika na ulinzi wa raslimali za maliasili katika sekta za wanyamapori na misitu. Lengi ni kudumisha nidhamu na kuongeza ufanisi ili wahifadhi wote waweze kuongea lugha moja ya uhifadhi.
Akiitimisha hotuba yake alizungumzia suala la ujangili kwa kusema, Wizara inaamini kwamba changamomoto za ujangili na uvunaji haramu wa misitu na matatizo mbalimbali yanayohikabili uhifadhi nchini hayawezi kutatuliwa kwa mfumo wa utendaji kazi wa kiraia. Hivyo, Wizara inakamilisha taratibu za kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka wa kiraia kwenda jeshi usu.Mabadiliko haya ya kimfumo ni matakwa ya Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Na.5 ya mwaka 2009 ambayo imeanisha kwamba kutaundwa kikosi cha jeshi usu (Wildlife Protection Unit), ili kuhakikisha ulinzi kamili wa rasilimali katika maeneo yaliyohifadhiwa
Katika Maadhimisho hayo pia kulikuwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, ambaye liwakilishwa na Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya TAWA Inspekta Jenerali  Abdulrahman Kaniki, kwa kusema, Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori inafuatilia kwa karibu matayarisho yanayofanywa ya kuandaa watumishi kuingia kwenye mfumo wa Jeshi usu ili kuboresha ulinzi wa raslimali za maliasili kwa ujumla.
Inspekta Jenerali Kaniki, alimalizia hotuba yake kwa kuwajulisha wahitimu kuwa, Bodi ya TAWA inao wajumbe waliobobea kwenye masuala ya Ulinzi na usalama wa nchi. Watatumia utaalamu wao kuishauri vizuri mamlaka na Wizara kwa ujumla ili kuhakikisha kwamba mfumo wa jeshi usu unaanzishwa rasmi ili kuongeza ufanisi katika ulinzi wa raslimali za maliasili kwa faida ya vizazi vyote.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Bw. Martin T.Loibooki, alianza hotuba yake kwa kumshukuru Katibu Mkuu kukubali kuja kufunga mafunzo hayo ya Maafisa wanyampori daraja la 11 kutoka TAWA na TANAPA.
Bw.loibooki alielezea kidogo Mamlaka anayoisimamia kwa kuanza kusema, Mamlaka ilianzishwa na Serikali kama chombo cha utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa niaba ya Serikali chini ya uangalizi wa Serikali na  kuwa na mfumo unaonesha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi zaidi. Kama ilivyo kwa Mamlaka Serikali nyingine nchini, lengo la kuanzishwa TAWA ni kutekeleza majukumu ya Idara ya Wanyamapori hasa ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini. Majukumu ya TAWA ni kusimamia shughuli za utawala, ulinzi, usimamizi wa raslimali ya Wanyamapori katika maeneo yote nje ya Hifdahi za Taifa na Hifadhi ya Ngorongoro.
Baada ya maelezo hayo mafupi, Bw.Loibooki alimueleza mgeni rasmi kuwa, kozi ya kwanza ya mafunzo haya ilifanyika mwezi Oktoba, 2016 ambayo ilihusisha Maafisa wanyamapori daraja la pili 40. Na hii ni ya pili ambayo tunaishuhudia leo imejumuisha watumishi 99. Hivyo jumla Mamlaka inakuwa na jumla ya watumishi 139 amabo wamepata mafunzo katika kituo cha Mlele.
Bw.Loibooki alisema kwa kukamilika kwa kozi hii ni faraja kub  wa sana kwa Mamalaka kwani kundi hili ndilo lilikuwa na changamoto kubwa za kiutendaji kwa kutokuwa na msingi wa mafunzo ya kijeshi.
Aliendelea kumueleza mgeni rasmi kuwa, kwa kuanzia kozi mbili zilizofanyika katika kituo cha Mlele zilihusisha Maafisa wanyamapori kutoka TAWA ambao waliajiriwa kutoka vyuo vikuu lakini hawakupata mafunzo ya awali ya kijeshi. Maafisa hawa ndiyo wasimamizi wa askari katika kazi za kila siku pamoja na doria.Hivyo,kulikuwa na upungufu mkubwa kiutendaji kwa wahifadhi ambao hawakupata mafuzo ya kijeshi kuwasimamia waliopata mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu alimueleza mgeni rasmi kuwa mwezi Februari 2017.Mamlaka ilikamilisha draft ya Sheria yake (The Tanzania Wildlife Management Authority Act of 2017) Sheria itakapopitishwa itaongeza nguvu ya utekelezaji wa mfumo wa Jeshi usu. Aidha, Taasisis za wanyamapori zimeandaa draft ya kanuni za jeshi usu (The wildlife protection regulations) ambazo zipo katika hatua ya kupitiwa na Menejement ya Wizara kabla ya kuidhinishwa na Mheshimiwa Waziri wa Malaisili na Utalii.
Bw. Loibooki alimueleza mgeni rasmi kuwa TAWA imeunda kikundi kazi cha kuanda TAWA General Orders ambao utakuwa muongozo wa utekelezaji wa kazi za kila siku.
Alimaliza hotuba yake kwa kusema kwamba mamlaka ianjipanga na inachukulia kwa makini wa hali ya juu maandalizi ya kuingia mfumo wa jeshi usu.
Bw.Loibooki alihitimisha hotuba yake kwa kusema kwamba, katika mwaka wa fedha 2017/18 ,mamlaka imetenga fedha kwa ajili ya kuendelea kutoa mafunzo ya utayari wa kupokea mabadiliko kuelekea katika mfumo wa jeshi usu.Watumishi wote watapata mafunzo hayo kufuata ratiba itakayowekwa na mamlaka.Ratiba ya mafunzo itawekwa bayana ili kuwatoa hofu watumishi na kuwapa nafasi ya kufanya maandalizi mapema. Mwezi Mei 2017 ,mamlaka italeta watumishi wengine kwenye mafunzo.Kozi hii itakuwa ni maalum kwa wakuu wa vituo na baadhi ya maafisa wa makao makuu.

Comments