Featured Post

WAZIRI MWIGULU AIONGOZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE YA ULINZI NA USALAMA KUKAGUA MRADI WA UJENZI KITUO CHA POLISI OYSTERBAY



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (katikati), akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu baada ya kuwasili katika eneo la mradi unaoendelea wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi, Oysterbay,leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (kushoto), akiongozana na wajumbe wengine wa kamati hiyo wakati wakiwasili katika eneo la mradi wa ujenzi wa kituo cha polisi, Oysterbay, leo jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mtaalamu wa Majengo kutoka kampuni inayojenga Kituo cha Polisi Oysterbay, Mhandisi Fanuel Malekela, akitoa maelezo ya mchoro wa ujenzi wa kituo hicho kwa  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (wapili kushoto),wakati kamati hiyo ilipotembelea ujenzi wa mradi huo.Wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(watatu kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu. Ziara hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna wa Fedha wa Jeshi la Polisi, Albert Nyamhanga, akitoa maelezo ya mradi wa Ujenzi wa kituo cha Polisi,Oysterbay kwa  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu(watatu kulia), wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba(kulia), akiwaongoza kutoka ndani ya jengo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama baada ya kumaliza kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa kituo cha polisi,Oysterbay leo jijini Dar es Salaam.Huku sehemu kubwa ya mradi huo ikiwa imekamilika. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Comments