Featured Post

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AMUANGUKIA WAZIRI MWIJAGE

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na waandishi wa Habari ambao hawapo pichani kuhusiana na suala hilo


 Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro, Vivek Pandey akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutotoa kibali cha ubora unaohitajika na hivyo kusitisha  uzalishaji
Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha
Kilimanjaro ,Vivek Pandey  kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutokutoa kibali cha ubora unaohitajika wa kiwanda hicho  na hivyo kusitisha uzalishaji kulia ni Msimamizi wa Kiwanda hicho,Paskal Dimelo
Msimamizi wa Kiwanda cha kuzalishaji Saruji Mkoani
Tanga cha Kilimanjaro, Paskal Dimelo akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutokutoa kibali cha ubora unaohitajika na hivyo kusitiza uzalishaji wake kushoto ni Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro, Vivek Pandey,
MBUNGE wa Jimbo la Tanga kupitia Chama cha Wananchi CUF Alhaj Mussa Mbaruku amemuomba Waziri wa Viwanda na biashara Charles Mwijage kuingilia kati ucheleweshawajiwa wa cheti cha ubora wa viwango unaotolewa na shirika hilo la TBS na kusababisha zaidi ya watumishi 300 kupoteza ajira baada ya  kiwanda hicho kufungwa.

Ameyazungumza hayo jana baada ya siku kadhaa kutolewa taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa shirika hilo limechangia kwa kiasi kikubwa kupoteza ajira kwa zaidi ya watumishi 300 kutokana na agizo lao la kusitiza uzalishaji katika kiwanda hicho kwa madai ya kukosa ubora unaotakiwa.

Alionyesha masikitiko yake hayo juu ya hataua iliyochukuliwa na shirika hilo la Ubora wa viwango Tanzania (TBS) ya kukifungia kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro kilichopo Jijini Tanga kwa kudaiwahawajafikia ubora unatakiwa katika bidhaa hiyo bila ya kuangalia athari za mwekezaji huyo na ajira zilizopotea kiwandani hapo.

Aidha alisema ni jambo la kushangaza kwa viongozi wa mamlaka hiyo husika(TBS)ambapo kwa namna moja au nyingine wanaonekana wanaikwamisha Serikali katika mpango wake wa kukua katika uchumi wa viwanda ambavyo vinaweza kuwa mkombozi wa ajira hapa nchini.

“Serikali inapambana na uchumi wa viwanda vitakavyoweza kusaidia ajira kwa vijana wetu sasa kinachotokea katika kiwanda hiki kunaonekana kuna watu wachache wanataka kumkwamisha muwekezaji huyu,hivi wizara husika iko wapi?nini hatma ya mwekezaji huyu na kufanya hivi hatuoni kama tunawafukuza hawa wawekezaji?”Alihoji Alhaj Mbaruku.

Hatua ya kusitiza huduma ya uzalishaji wa kiwanda hicho licha ya kuathiri ajira za wafanyakazi hao lakini pia itasababisha serikali kukosa mapato yanayoweza kusaidia kukuza uchumi wa Taifa na Mkoa wa Tanga .

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Kiwanda hicho,Vivek Pandey alisema kinachowaasumbua wao ni cheti bora kutoka kwa shirika la viwango cha kutambuliwa hivyo wanaomba suala hilo liingiliwe kati na mamlaka husika ikiwemo serikali ili waweze kuendelea na uzalishaji ambao utaweza kuongeza wigo wa ajira kwa vijana.

Alisema baada ya taarifa zao kutoka kwenye vyombo vya habari alifika mmoja kati ya wataalamu kutoka katika shirika hilo Jijini Dar es saalm na kuondoka na sampo ya bidhaa hiyo ambapo mpaka sasa bado hawajapata majibu sahihi ya hatma yao.

“Baada ya taarifa zetu kuruka kwenye vyombo vya habari siku ya pili tu alitumwa mtu kutoka makao makuu ya TBS Jijini Dar es salaam na niliondoka nae sambamba na sampo ya bidhaa hiyo nahii leo ja (jana)kwenda tena ili kuona hatua gani zimechukuliwa dhidi
yetu”Alisema Pandey.

Aidha alisema hatua hiyo ya kusitisha uzalishaji mbali na kupoteza ajira kwa vijana lakini wamekisababisha hasara kiwanda kwa zaidi ya shilingi Milioni 200 ambazo zinatokana na tani elfu 11 zilizozalishwa kisha kuonekana zipo chini ya kiwango.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Comments