Featured Post

MASAUNI AWATAKA WANANCHI WAISHIO MPAKANI MWA TANZANIA NA MSUMBIJI KUFUATA SHERIA ZA UHAMIAJI, ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAKATA GESI ASILIA MADIMBA



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia Madimba wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), mkoani Mtwara, Mhandisi Sultan  Pwaga, wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara kiwandani hapo kuangalia jinsi gesi inavyozalishwa. Hata hivyo,  Masauni alitoa ahadi, Jeshi lake litafanya taratibu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda (katikati) pamoja na TPDC kufanikisha uwepo wa Kituo cha Polisi kama walivyoomba uongozi wa Kiwanda hicho kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kiwandani hapo pamoja na wananchi waishio jirani na kiwanda hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kilambo kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. Masauni aliwataka wananchi hao kudumisha amani mpakani hapo pamoja na kufuata sheria za uhamiaji za nchini pamoja na za Uhamiaji Msumbiji endapo watahitaji kuvuka mpaka huo. Masauni baada ya kukagua mpaka huo aliwataka maafisa wake kuimairisha ulinzi zaidi mpakani hapo. Wapili kulia ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiiangalia moja ya nyumba za askari wa Jeshi la Magereza ambazo zinahitaji marekebisho katika Gereza Lilungu mkoani Mtwara. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi hilo mkoani humo, Ismail Mlawa.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuhitimisha ziara yake kukagua mpaka wa Tanzania na Msumbiji uliopo katika Kijiji cha Kilambo, mkoani Mtwara. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda. Wapili kulia ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, Rose Mhagama, na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa huo, Neema Mwanga.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwapa maelekezo maafisa wake wakati alipokuwa Mto Ruvuma, Kijiji cha Kilambo kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, mkoani Mtwara. Wapili kushoto ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, Rose Mhagama, na anayefuata ni Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa huo, Neema Mwanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mtwara, Ismail Mlawa kwa ajili ya kwenda kukagua nyumba za askari Magereza wa Gereza Lilungu mkoani humo ambazo zinahitaji marekebisho kutokana na kuharibika. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Comments