Featured Post

MAKONDA KWELI KIBOKO, JPM ASEMA 'CHAPA KAZI USIOGOPE KUCHAFULIWA MITANDAONI'!




KWA mara nyingine tena, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Christian Makonda, anaendelea kupeta na yaonekana hatikiswi na unyasi licha ya ukweli kwamba kitendo anachodaiwa kufanya cha kuvamia Kituo cha runinga cha Clouds TV Ijumaa usiku kulalamikiwa na jamii.
Hatua hiyo inafuatia kauli iliyotolewa leo hii na Rais John Magufuli wakati akizindua mradi wa ujenzi wa barabara za juu (flyovers) Ubungo, jijini Dar es Salaam, ambapo alisema hawezi kufanyia kazi maneno ya mitandao kwa sababu mengi yanaandikwa.

“Chapa kazi, huko kwenye mitandao hata mimi nimeandikwa sana, haya maneno yanachelewesha maendeleo, Watanzania wanataka kuona maendeleo,” alisema JPM.
Hii maana yake ni kwamba, wale waliokuwa 'wakishinikiza' kupitia mitandaoni kwamba Rais Magufuli amtimue kazi haraka walie tu, kwani kijana ataendelea kuchapa kazi mwanzo-mwisho.
Suala la Makonda limezua mjadala wa muda mrefu sasa tangu alipotangaza vita dhidi ya vigogo wa dawa za kulevya huku watu wengi maarufu wakiwemo wanasiasa, wafanyabiashara na viongozi wa dini wakifikishwa kwa vyombo vya sheria.
Miongoni mwa waliopatwa na zahama hiyo ni mfanyabiashara maarufu Yussuf Manji aliyekaa mahabusu kwa siku sita na kufunguliwa kesi, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Askofu Josephat Gwajima, wasanii mbalimbali kama Wema Sepetu, wanamuziki Vanessa Mdee, Nassib Abdul ‘Diamond Platinumz’, Khalid Mohammed ‘T.I.D.’, video queen Agnes Gerald ‘Masogange’ na wengineo.
Wakati Wema aliamua kukimbilia Chadema, Askofu Gwajima yeye ameamua kupambana na Makonda ambapo akishirikiana na mwanadada Mange Kimambi, waliibua hoja ya vyeti feki vya mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam na kwamba anatumia jina ambalo siyo lake.
Kwa mujibu wa Kimambi na Gwajima, ambaye amegeuza madhabahu ya kanisa lake la Ufufuo na Uzima kuwa sehemu ya ‘kujitakasa’ na uchafu wake, jina halisi la Makonda ni Daudi Albert Bushite, mzaliwa wa Kijiji cha Koromije wilayani Misungwi.
Wanasema jina la sasa limetokana na cheti cha mtu anayeitwa Paul Christian Muyenge ambalo ndilo ameendelea kulitumia kabla ya kuapa na kupata jina la Makonda.
Vita hiyo imezidi hadi haya yalipotokea, kama yalivyo hapa chini:
MAKONDA AVAMIA CLOUDS KWA MITUTU YA BUNDUKI
 
Jengo la Clouds Media Group lililopo Mikocheni B jana lilishuhudia sekeseke la aina yake baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia akiwa na Walinzi wenye Bunduki.

Tukio hilo tukoea majira ya Usiku wakati kipindi SHILAWADU kikiwa hewani ambapo Makonda alivamia kwa lengo la kushinikiza Shilawadu waonyeshe mahojiano yenye lengo la kumchafua Askofu Gwajima.

Vyanzo vya uhakika vinaeleza kwamba, mwanzoni wiki 2 zilizopita, SHILAWADU walipigiwa simu na watu wasiojulikana wakieleza kwamba wana 'ubuyu' mzito wa kuhusu Askofu Gwajima na mwanamke anayedaiwa kuzaa nae. Mwanzo Shilawadu walikataa habari hiyo, lakini siku moja walikutana na Makonda akawashawishi SHILAWADU wafuatilie stori hiyo. Kama kawaida yao kupenda umbea, SHILAWADU wakiongozwa na Soudy Brown walimtafuta mwanamke anayedaiwa kuzaa na Gwajima kisha wakamhoji.

Hata hivyo, kwa kuhofia nguvu ya Gwajima katika kupambana na shutuma dhidi yake, na kwa kuzingatia maadili ya kazi, SHILAWADU waligoma kurusha habari hiyo hewani mpaka wapate kauli za upande wa pili ( upande wa Gwajima ). Baada ya kuhangaika huku na kule , SHILAWADU walishindwa kupata upande wa pili wa habari ( walishindwa kubalance story ).

Kutokana na hilo, na kujua kwamba Gwajima asingewaacha salama kwa kutoa story ya uongo dhidi yake, #SHILAWADU na wasimamizi wa vipindi wa Clouds Tv waliamua kuachana kabisa na story hiyo.

MAKONDA ANAINGIAJE? : Imefahamika kwamba watu ambao walipiga simu kwa Shilawadu kuhusu uwepo wa Mwanamke huyo ni watu wa Makonda. Makonda alitaka story hiyo itolewe kupitia #SHILAWADU ambao wana kawaida ya kuripoti matukio ya Watoto/wanawake waliokataliwa. Kwa kuwa Makonda ana marafiki wengi pale Clouds, aliamini kwamba story hiyo lazima ingetolewa na hivyo kumchafua adui yake GWAJIMA (kuzima sakata la vyeti ).

Akiwa nyumbani kwake Masaki, Makonda alikaa kwenye Tv yake Ijumaa kusubiri SHILAWADU wamvue nguo Gwajima. Cha kumsikitisha, Makonda alipata habari kwamba SHILAWADU wamegoma kupeleka habari hiyo. Hata viongozi akiwemo swahiba wake Ruge walikaataa kabisa kupeleka habari ambayo haiko 'balanced' na mbaya zaidi inawaingiza kwenye vita na mtu wa aina ya Gwajima.

Kama kawaida yake, Makonda aliamua kutumia ubabe. Kwa kuwa amezoea kuingia Clouds, Makonda alifahamu kuwa muda huo viongozi hawapo na watu waliopo anawamudu. Hivyo aliamua kwenda Clouds kuhakikisha Shilawadu wanaonyesha habari hiyo ya kumchafua Gwajima. Hivyo alibeba wanaume zaidi ya 8 wakiwa wamebeba silaha za moto.

Alipofika Clouds, walinzi wa Getini walimruhusu kupita yeye na gari iliyokuwa nyumba yake akisema ni rafiki zake wamekuja mara mara moja kwenye SOSOO FRESH kwani Adamu Mchomvu amewaalika. Lakini alipofika Reception, Mlinzi wa zamu alisitia baada ya kuona Makonda amekuja na watu wengi. NA HAPO NDIPO KASHESHE ILIANZA.

Walinzi wa Makonda walitoa Bunduki, walimtishia Mlinzi wakampiga sana na wakatumia nguvu kubwa hadi walifanikiwa kuingia ndani. Walipofika na Bunduki zao, Makonda aliamuru kila mtu kukaa alipo huku akilazimisha habari ya Gwajima iende. Kwisa kama kiongozi wa kipindi ndiye ambaye alipingwa mitama na ngumi za kutosha.

Kwa walioangalia kipindi wanajua kwamba kipindi hakikuisha, hiyo ni kutokana na kwamba Makonda na waligawa kipigo cha maana kwa Shilawadu kisha wakawabeba kwenda nao nje akisema wanaenda Cental.

Pia alitumia Bunduki kuwalazimisha Shilawadu wampe Video ya Mama anayedaiwa kuzaaa na Gwajima (alipewa). Makonda aliwaambia wapambe wake kama Shilawadu wamekataa kuonyesha habari hiyo baasi yeye atahakikisha inasambaa kupitia mitandao ya kijamii.

Hivi sasa Shilawadu hawako sawa kisaikolojia huku Suod Brown akiwa hana amani kwani alipigwa picha na Makonda alimuambia kama anaogopa kumdhalilisha Gwajima baasi yeye atadhalilishwa kwani Sura yake itawekwa hadharani kila mtu afahamu.

Baadae Makonda aliondoka baada ya kupigiwa simu ambayo haijulikani nani alipiga lakini Makonda alipoondoka Ruge alingia Clouds akiwa na watu huku na yeye amebeba bastola. Inaaminika ile simu ilipigwa kumuambia aondoke maana Ruge anakuja.


CV YA PAUL MAKONDA

1. Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.

2. Majina yake halisi ni Daudi Albert Bushite

3. Alianza darasa la kwanza mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije akitumia majina ya Daudi Albert Bushite. Mwaka 1991 alifeli darasa la 4, akarudia.

4. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition).

5. Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali.

6. Mwaka 1997 akajiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Pamba.

7. Mwaka 2000 akahitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero).
 8. Mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002.

9. Mwaka huohuo 2002 akitumia cheti cha Ndg.Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005.

10. Mwaka 2003 alikutana na Ndg.Benjamin Sitta (mtoto wa Marehemu Samwel Sitta, ambaye ni Mayor Kinondoni kwa sasa). Wakawa marafiki.

11. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yake ya uvuvi, aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada lakini akakosa nafasi.

12. Baada ya kukosa nafasi alienda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta akiwa kama rafiki wa Ben (mtoto wa Sitta). Kwakuwa alitoka familia duni, Sitta aliahidi kumsomesha elimu ya juu.

13. Mwaka 2006, alipata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa kutumia vyeti vyake vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani).

14. Alidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management & Accounting. Mwaka 2007 alimaliza first year lakini akashindwa kuendelea na 2nd year baada ya kupata Suplementary 6 kati ya Course 8 alizokua akisoma (akawa discontinued).

15. Mwaka huohuo 2007 akaomba Admission upya. Akamaliza first year akiwa na carriers 3 ambazo alienda nazo 2nd year. Mwaka 2008 akiwa 2nd year akapata supplementary 4 kati ya course 8 alizokua akisoma. Akawa na mzigo wa carry over na supplementary. Akaamua kuacha chuo.

16. Mwaka 2008 akaenda kujaribu kuomba udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine lakini akakosa.

17. Mwaka 2009 akarudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya. Akaachana na CMA akachagua Community &Economic Development (CED).

18. Mwaka 2012 akahitimu shahada ya kwanza ya Community &Economic Development kwa jina la Paul C Makonda badala ya majina yake halisi ya Daudi A Bushite.

19. Jina Makonda analitumia baada ya kula kiapo mahakamani kubadili jina. Cheti cha Form four kinasomeka Paul C Muyenge lakini vyeti vya elimu ya juu vinasomeka Paul C Makonda baada ya kuapa mahakamani.

20. Ndugu Daudi Albert Bushite ameoa (tangu mwaka 2009) lakini hajabahatika kupata mtoto. Na ndiye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa.



Comments