- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na
Jovina Bujulu- MAELEZO
Kila
mwaka ifikapo Machi 8 kila mwaka, wanawake duniani kote huadhimisha siku yao ambapo hujitathmini
kupitia shughuli mbalimbali za maendeleo walizofanya, changamoto zilizopo na
kuweka mikakati ya utatuzi wa changamoto hizo.
Akiongea
hivi karibuni katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, Katibu
mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi
Sihaba Nkinga alisema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Tanzania ya Viwanda; Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko”
Kauli
mbiu hii inasisitiza kuwajengea wanawake uwezo wa kitaaluma, kibiashara,
upatikanaji wa mitaji, masoko na biashara ili waweze kushiriki kwa usawa, na
kunufaika na fursa zilizopo badala ya kuwa wasindikizaji.
“Ujumbe
wa kauli mbiu hii umezingatia sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia ya mwaka
2000 na ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu hususani lengo namba 5 kuhusu
usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi” alisema Bi Nkinga.
Kauli
mbiu ya mwaka huu imetotolewa kutokana na kauli mbiu ya Umoja wa Mataifa (UN) isemayo
“Uwezeshaji wa Wanawake Kiuchumi katika
Dunia ya Mabadiliko ya Kazi”.
Akizungumza
hivi karibuni, Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini (TAMWA) Mama
Edda Sanga alisema kuwa wanawake
wanapaswa kujiwezesha katika maeneo ya kiuchumi, kisiasa, na kijamii ili
wapate fursa ya kushiriki katika maamuzi mbalimbali ambayo hatimaye yatawaletea
tija na mafanikio.
Hii
ina maana kuwa, endapo wanawake watapata nafasi ya kushiriki katika maamuzi
mbalimbali ni rahisi kwao kusikilizwa na hata kuwa na sauti katika masuala ya
wao kumiliki ardhi, majumba na hata viwanda.
Aidha,
kauli mbiu hii inawahamasisha wanawake kuhakikisha kuwa kunakuwa na usawa wa
jinsia unaoondoa vikwazo na kuhakikisha wanapata fursa sawa na kuweka
ulinganifu katika ushiriki ambao unawanufaisha kiuchumi kuanzia ngazi ya
familia.
Ili
kufikia malengo ya kujikomboa kiuchumi, wanawake wanatakiwa kujitambua na pia
kutambua malengo na mipango yao. Wanatakiwa kutambua na kutumia fursa vizuri
wanayopata hasa mahali watakapopata taarifa za kuwanufaisha kiuchumi kwa mfano
benki, vikundi vya mikopo, taasisi au hata kwa watu binafsi.
Kumekuwa
na juhudi mbalimbali za kuwakwamua wanawake kiuchumi, kutoka kwenye taasisi,
mashirika na watu binafsi, hata hivyo
wao pia wanahitaji kujikomboa kwa kutumia juhudi zao binafsi kama vile kujiunga
katika vikundi waweze kukopeshwa ili waweze kujiajiri katika mkondo wa
uzalishaji mali, kama vile kuanzisha viwanda vidogo vidogo, kwa mfano viwanda
vya usindikaji vyakula, kazi za mikono na ushonaji ambavyo havihitaji mtaji
mkubwa.
Hii
itawafanya kunufaika na kuondoa hali ya utegemezi katika jamii, na hivyo
kujiondoa katika hali ya unyonge.
Ni
ndhahiri wanawake ndio wazalishaji wakubwa katika nyanja za kiuchumi, hivyo
katika kutimiza ndoto na malengo zao ni budi juhudi zitumike ili washiriki
katika kukuza pato lao na taifa kwa ujumla.
Naye
Bibi Lilian Liundi ambaye ni Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) anasema
kuwa katika kusherekea siku ya wanawake duniani, taasisi yao ilifanya kongamano
hivi karibuni pamoja na mambo mengine walizungumzia mpango wa taifa
kuhusu ushiriki wa wanawake katika kuelekea uchumi wa viwanda vya kati.
Alisema
kuwa wanawake wa mjini kwa sasa wanashiriki vizuri katika shughuli ambazo huwaongezea
kipato wakati wanawake wa vijijini
ushiriki wao katika shughuli za kuwaongezea kipato si wa kuridhisha kwani
wanatumia muda mrefu kutembea kutafuta maji na kuni kwa ajili ya matumizi ya
familia.
Bibi
Liundi alitoa wito kuwa huduma za jamii zisogezwe karibu na jamii ili wanawake
ambao ni wazalishaji mali wakubwa wapate muda wa kutosha kushiriki katika
shughuli za kujiongezea kipato badala ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma
hizo.
Naye
Bibi Magreth Dotto ambaye ni Mhandisi wa Migodi, na Mhadhiri Msaidizi kutoka
Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam aliwashauri watoto wa kike kusoma masomo ya
sayansi kwa kuzingatia kasi ya ukuaji wa teknolojia kila siku ili baadaye
wapate nafasi nzuri katika jamii na kutoa mchango wao katika kutatua changamoto
za kijamii na taifa.
“Uhandisi
unawezekana kwa wasichana na ni taaluma nzuri, hivyo wasichana waache kuyaogopa
masomo ya sayansi, ni taaluma inayobadilisha maisha kwa kuyaboresha kwa sababu
inalipa vizuri” alisema Bibi Magreth.
Kwa
upande wake Dkt. Ave Maria Samakafu ambaye ni Mhadhiri katika Chuo cha Sayansi
ya Tiba Muhimbili na Mratibu wa Taifa wa Taasisi ya Wanawake ya Ulingo alisema
kwa sasa wanawake wana mwamko mkubwa ambao umeleta mageuzi katika familia na
kuinua kipato chao.
“Kwa
sasa tunaona ushiriki mkubwa wa wanawake katika nyanja ya uchumi kwa sababu
kuna wanawake wafanyabiashara wadogowadogo, wa kati na hata wakubwa” anasema
Dkt Semakafu.
Alisema
kuwa elimu inahitajika zaidi kwa wanawake wa vijijini ambao bado wanatawaliwa
na tafsiri potofu ambapo ukandamizaji wa wanawake bado unapewa nafasi kubwa na
jamii, hivyo kuwafanya wasisonge mbele katika kujiletea maendeleo yao.
Dkt.
Semakafu aliendelea kusema kuwa wanawake wengi wa mjini wanatambua nafasi zao
katika jamii, hivyo wanatumia ufahamu huo kama fursa kwao ambazo zinawasaidia
katika kuleta mageuzi ndani ya familia zao.
“Vijana
wa kike wamekuja na nguvu mpya, kinachoendelea sasa hivi kinafungua uelewa wa
jamii, watoto na wazazi na kuwafanya watambuliwe na jamii” alisema Dkt. Semakafu.
Dkt.
Semakafu alitoa mfano unaodhihirisha nafasi ya mwanamke akimtaja Agnes Magongo
ambaye hivi karibuni ameshinda tuzo ya UN ya “women economic empowerment” ambayo
ni tuzo ya uwezeshaji wa wanawake.
“Wanawake
tushiriki katika kuboresha maisha yetu, tusiwe wasindikizaji bali watendaji,
twende pamoja katika uchumi wa viwanda ili tuweze kumiliki viwanda” alimalizia
Dkt. Semakafu.
Katika
kuhimiza fursa za uchumi kwa wanawake kauli mbiu ya mwaka huu inalenga
kuhamasisha jamii na wadau wote nchini kuongeza fursa za kiuchumi kwa wanawake
ili waweze kushiriki na kunufaika nazo hasa kipindi hiki ambapo Tanzania
inaelekea azma ya uchumi wa kati kwa misingi ya kuwa nchi ya viwanda.
Mama
Sihaba aliwakumbusha wadau wote katika ngazi zote kuweka mikakati thabiti ya
kutatua changamoto zinazokwamisha kufikiwa kwa usawa wa jinsia na kusababisha
wanawake na wasichana kushindwa kutimiza malengo na ndoto zao kimaisha.
Mwisho
Comments
Post a Comment