Featured Post

KIKOSI 841KJ MAFINGA KIMESHEREKEA MIAKA 50 TOKA KUANZISHWA KWAKE KWA KUJENGA KIWANDA CHA NAFAKA

Mgeni rasmi katika maazimisho hayo Luteni kanali mstaafu Pius Chale alikipongeza kikosi cha 841kj mafinga kwa kutimiza miaka 50 pamoja na kuzindua jarida maalum la kikosi hicho akiwa amelishika linaitwa Uhodari.
 Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha 841kj wakionyesha ukakamavu wake kwa kushindana kuvuta kamba ikiwa na lengo la kuburudisha wakati wa sherehe za miaka 50 ya kikosi cha 841kj
Baadhi ya vijana waliopo kwenye mafunzo ya awali ya kijeshi maarufu kama operation Magufuli kujitolea katika kikosi cha 841kj mafinga nao walikuwa miongoni mwa waliosherekea miaka 50 ya kikosi hicho.
Hili ndio jengo linalojengwa kwa ajili ya kiwanda cha Kukoboa na kusaga nafaka za kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa 841KJ Mafinga.

Na Fredy Mgunda,Mafinga

Kikosi cha jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga kimeanzisha kiwanda kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao wanayozalisha lengo likiwa ni kuhakikisha jeshi hilo linajilisha na kupata mahitaji mengine kupitia uzalishaji mali.

Akizungumza kaimu kamanda wa kikosi cha 841 kj mafinga Captain Victor Nkya katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mnamo tarehe 15 / 03 / 1967 kikiwa na lengo la kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kuwa na serikali ya viwanda kwa kuanza kujenga kiwanda cha nafaka na mifugo ambacho kitatoa ajira wa watu wengi na kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla pamoja na kuimalisha ulinzi kutokana na majukumu waliyonayo.


 Nkya alisema kuwa kikosi cha 841kj kj mafinga kimeamua kujenga kiwanda hicho ambacho kitakuwa kinaendeshwa kibiashara ili kukuza ajira na pato la taifa.

“Hapa kikosini tunalima na kufuga mifugo ya aina mbalimbali kwa wingi na kwa kiwango kinachotakiwa  kukidhi soko ili kuonyesha kuwa kikosi cha jeshi la kujenga taifa 841kj mafinga kinakuwa mfano wa kuigwa na kukidhi haja ya kuanzishwa kwa kikosi hicho”.alisema Nkya

Captain Nkya alisema Sasa hivi Jeshi la kujenga taifa kikosi cha 841kj kimekuwa kikosi cha Kisasa nachenye wasomi wengi wanaweza kusaidia kubuni vitu vingi vyenye faida ya kulisaidia Jeshi katika Kufanikisha Malengo yake kama Kulinda Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kujitoa katika shughuli nyingine za kijamii.

“Tumefungua kiwanda ni lazima sasa kuongeza uzalishaji kwa lengo la kuja kuipunguzia serikali gharama za kukihudumia kikosi cha 841kj mafinga ukiangalia tunaeneo kubwa na tunanguvu kazi hivyo ni lazima tulime na kufuga kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli anataka jeshi la kujenga taifa lirudi kujitegemea”.alisema Nkya

Kwa upande wake mgeni rasmi katika maazimisho hayo Luteni kanali mstaafu Pius Chale alikipongeza kikosi cha 841kj mafinga kwa kutimiza miaka 50 kwa kuwa kudumu huko kwa kikosi hicho ni hatua kubwa sana katika ujenzi wa taifa.

Chale alikitaka kikosi cha 841kj kurudisha uzalendo kama zamani ili kuendelea kuzalisha chakula kwa wingi kama zamani kwa saizi kikosi hicho kin  alima eneo dogo sana kitu kinachochangia kuipa serikali wakati mgumu wa kikihudumia kikosi hicho.

“Nimetembea eneo kubwa sana leo lakini nimeona eneo la uzalishaji ni dogo sana hivyo mnahitaji kuongeza uzalishaji ili kuisadia serikali kuzalisha chakula kwa wingi nyie mna nguvu kazi hapa lakini bado sijaona mkiitumia ipasavyo”.alisema Chale

Aidha Chale alikipongeza kikosi hicho cha 841kj mafinga kwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kuanza ujenzi wa kiwanda ambacho kitaongeza ajira,uzalishaji wa bidhaa za chakula na kukuza uchumi wa nchi kutokana na uzalishaji wake.

“Nichukue fursa hii kuwapongeza kwa kuweza kuwa na wazo zuri kama hili la kujenga kiwanda hapo ndio mnakuwa mnatimiza malengo ya kikosi cha 841kj mafinga kwa kukuza uzalishaji kwa kutumia raslimali watu ambao mnao katika kiosi kuzalisha na sio kila siku mnakuwa mnategemea msaada kutoka serikalini”alisma Chale

Chale alikitaka kikosi kuendelea kutunza nidhamu waliyonayo na kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli katika jitihada zake za kuijenga Tanzania mpya yenye uchumi na viwanda.

Naye Bwana shamba wakikosi (farm manager) luteni Francis Breek wa kikosi cha 841kj alisema kuwa wamejipanga kuongeza uzalishaji kwa kuwa wana eneo kubwa na wana wataalamu wengi wanaoweza kukidhi mahitaji ya kukuza uzalishaji.

“Ukiangalia mwaka huu tumelima eneo kubwa na tumeongeza idadi ya mifugo hivyo tunatarajia kuongeza tena idadi ya mifugo na kupanua eneo la kilimo ili kuongeza uzalishaji kwa kuwa tumejenga kiwanda na kiwanda kinahitaji uzalishaji mkubwa wa nafaka pamoja na ufugaji mkubwa na wenye tija”alisema Breek

Lakini pia kikosi hicho cha 841kj Mafinga kilizindua jarida linaloitwa uhodari ambalo linaonesha kila kitu kinachofanywa na kilichofanywa na kikosi hichotoka kuanzishwa kwake.

“Hongera kikosi cha 841kj kwa Kutimiza Miaka 50 Tokea Kuanzishwa kwake”

Comments