Featured Post

CHADEMA WANATAFUTA KIKI, MBONA HAWAKUULIZA KWANINI NAPE ALITEULIWA?



KATIKA mazingira yanayoonyesha wazi kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekosa hoja nii kauli yake iliyotolewa leo.
Katika mkutano wao na wanahabari jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Tanzania Bara), John Mnyika, wamehoji sababu za Rais Dkt. John Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye.

Mnyika, ambaye kwa zaidi ya mwaka mmoja amekuwa kimya na kupotea kwenye majukwaa ya siasa, amemtaka Rais Magufuli kuueleza umma wa Watanzania sababu za kutengua uteuzi wa Nape.
“Tunamtaka Rais Magufuli aueleze umma wa Watanzania sababu hasa zilizomfanya atengue uteuzi wa Nape,” alikaririwa akisema.
Hata hivyo, hoja hizo zinaonekana kukosa mashiko na kama njia za kutafuta kiki katika siasa, kwani hakuna hata siku moja ambayo wao kama Chadema, ama mtu yeyote, waliowahi kuhoji kutenguliwa kwa teuzi za watendaji wengine.
Ama Chadema hawakuwahi kuhoji mara ya kwanza kabisa wakati Rais Magufuli alipoamua kumteua moja kwa moja Nape kuwa waziri kamili mara tu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mnyika anasema, taarifa za Ikulu hazikueleza sababu za kwa Nape hivyo ipo haja kwa Rais kueleza wazi sababu ya kumuondoa.
Lakini hasemi kama iliwahi kutokea hata wakati mmoja tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani ama marais waliopita, wakaeleza sababu za kuwaondoa mawaziri kwenye nafasi zao, kama ilivyokuwa vigumu pia kupata sababu za kuteuliwa kwao.
Kama ni kubadilisha gea angani nadhani wamekosea, warudi wajipange upya.

Comments