Featured Post

ZIARA YA NAIBU WAZIRI MASAUNI MPAKANI TUNDUMA KUKAGUA SHUGHULI ZA UINGIAJI NA UTOKAJI WA WAGENI NA RAIA

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisaini daftari la wageni baada ya kuwasili wilayani Momba Mkoani Songwe, kwa lengo la  kutembelea na kukagua uingiaji na utoakaji wa raia na wageni katika mpaka wa Tunduma unaotoa huduma kwa watu wanaoingia na kutoka katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Botswana, Afika Kusini, Namibia na DRC Congo.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Afisa Uhamiaji Mpaka wa Tunduma akimuelekeza jambo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), wakati wa ziara ya kutembelea mpaka huo unaotoa huduma kwa watu wanaoingia na kutoka katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Botswana, Afika Kusini, Namibia na DRC Congo.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, walipotembelea jiwe (linaloonekana pichani) linalotenganisha nchi ya Tanzania na Zambia.Wengine ni Wakuu wa Idara za Uhamiaji, Magereza, Zimamoto na Polisi walioambatana na Naibu Waziri katika ziara hiyo mkoani Songwe. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mpakani Tunduma huku akiwaasa kushirikiana kwa pamoja katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu wanaoingia  nchini kupitia mpaka huo. Kulia  ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali na Wakuu wa Idara za Uhamiaji, Magereza, Zimamoto, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Polisi baada ya kutembelea mpaka wa Tunduma.Ambapo aliwaasa kushirikiana kwa pamoja katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu wanaoingia  nchini kupitia mpaka huo. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Comments