Featured Post

UONGOZI WA BODABODA MKOANI MWANZA WAPONGEZA ZOEZI LA UKAGUZI WA POLISI

Binagi Media Group
Umoja wa waendesha bodaboda mkoani Mwanza umepongeza zoezi la ukaguzi wa vyombo hivyo linaloendeshwa na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani.
Jana Mwenyekiti cha umoja huo, Makoye Kayanda, amesema zoezi hilo linaangazia maeneo makuu manne ambayo yamekuwa yakihatarisha usalama wa watumiaji wa bodaboda wakiwemo abiria.

"Cha kwanza ni uvaaji wa kofia ngumu, cha pili leseni ya udereva, cha tatu kuwa na BIMA na ni ubebaji wa mishikaki. Kuna baadhi ya abiria zaidi ya 14 wametozwa faini kwa kukataa kuvaa kofia ngumu, sasa lazima tufuate sheria bila shuruti". Alisema Kayanda huku akipongeza zoezi hilo.

Kayanda aliwasihi waendesha bodaboda wote kuzingatia utii wa sheria bila shuruti ili kuondokana na mazoea yanayoweza kuhatarisha maisha yao na abiria wao pia huku akiwaonya baadhi ya abiria kuepuka tabia ya kukataa kutumia kofia ngumu kwa kisingizio cha uchafu.

"Kupanga ni kuchagua, kama hutaki kuvaa kofia nguvu ya unayopewa na bodaboda, nunua ya kwako ama mfuko wa plastiki ili ukipewa kofia uvalie maana kuna watu wanapata ajali wanapasuka vichwa na inakuwa ni tatizo kwa familia zao na taifa kwa ujumla". Alihimiza Kayanda.
Mwenyekiti wa bodaboda mkoani Mwanza, Makoye Kayanda

Comments