Featured Post

TIRDO YAIMWAGIA SIFA SIMIYU



 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,  Mhe. Anthony Mtaka


Na Dereck Murusuri
Dar Es Salaam,  21 Jan 2017
TAASISI ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) imeahidi kufanya kazi na Mkoa wa Simiyu katokana na utayari wake wa kutafsiri kivitendo dhamira ya Rais Dk Magufuli ya Tanzania ya Viwanda.
"Tumekubali kuja Simiyu kufanya 'feasibility study' ya kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za sekta ya afya zitokanazo na pamba, " alisema Prof Mtambo Madundo Mkumbukwa.

Prof Mkumbukwa, Mkurugenzi Mkuu wa TIRDO, alimwambia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,  Mh Anthony Mtaka kuwa wako tayari kuanza kazi hiyo mara moja.
"Tuna PhD 12 hapa na wengine wote ni Masters, tuko tayari kuja kufanya ukaguzi wa mwanzo wa kimazingira (preliminary environmental impact assessment) kwasababu tunaunga mkono juhudi zenu," alisema Prof Mkumbukwa.
Akiongea na wafanyakazi wa TIRDO,  mh Mtaka aliwapongeza kwa kuwa 'reference laboratory' ya Tanzania, dhamira iliyojengwa na credibility iliyowafanya wachague kufanya nao kazi.
"Nyie ndiyo mmetusaidia kufanya chaki zetu kuwa salama kabisa tofauti na chaki zingine," alisema na kuongeza kuwa TIRDO walihakikisha kuwa vumbi la chaki halina madini yanayoweza kumwathili mwalimu au mtumiaji wake.
RC Mtaka aliwaomba TIRDO, katika wakati wote wa mradi, wawapatie ushauri wa kitaalamu katika miradi yao, ombi ambalo lilipokelewa na kukubaliwa palepale.
"Unawezaje kumpa kazi ya kukupa ushauri wa kitaalamu mzungu  au mchina, kutengeneza vifaa vya sekta ya afya wakati yeye mwenyewe anavitengeneza hivyo na anataka uendelee kuwa soko lake na kama mshindani wake anaweza asikupe ushauri wa kukujenga ili ushindane nae, " alisema Mh Mtaka.
"Nitakuwa Balozi wenu popote nitakakokwenda kutokana na kazi nzuri ambayo nimeishuhudia hapa pamoja na raslimali watu walioko hapa" alisema.
Aliwashukuru kwa kukubali kupunguza gharama za utaalam wa kazi ya feasibility study na uandaaji wa mpango wa biashara kutoka milioni 700 ambayo ndiyo gharama halisi hadi milioni 150.
"Tumeamua kujenga mkoa mpya wa kiuchumi Simiyu, tunawaomba TIRDO, TFDA,  TBS,  TEMDO,  TIB, SIDO pamoja na Simiyu, tuungane kujenga viwanda kuifanya Tanzania ya viwanda iwe halisi.
Mh Mtaka na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu, walimaliza ziara yao isiyokuwa na mafanikio makubwa katika jitihada zao za ujenzi wa viwanda na kuanzisha kilimo cha umwagiliaji.

Comments