- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
ZILIKUWA ni dola mia
tatu rahisi zaidi ambazo Nelson Ryan ameweza kuzipata, lakini ghafla akagundua
kwamba alikuwa amejiingiza mtegoni. Mwito wa simu, ukionekana hauna kasoro
yoyote, ulimwongoza kwenye mauaji ya binti wa Kichina aliyepiga simu huku
akiongea sana. Simu hiyo pia ikamwongoza moja kwa moja kwenye maisha ya
kihalifu ya Hong Kong. Tangu sasa na kuendelea, Ryan hakuweza kufanya chochote mpaka
atakapompata muuaji ambaye amemwingiza kwenye majanga. ENDELEA…
Alikuwa mfupi, kijana ambaye utamu
wa maisha ulikuwa umemzingira ambao ulianza kumtupa mkono. Wakati nikisaini
kitabu chake, macho yake yaliangaza kwenye chumba changu kidogo, akaangaza
kwenye dari iliyojaa kutu, vumbi kwenye kabati la vitabu, dawati lisilo na
mvuto, kiti cha wateja kilichochakaa na kalenda iliyokuwa ukutani.
Baada ya kuondoka nikafungua
bahasha. Ilikuwa na noti thelathini za dola kumi kumi. Kwenye kadi nyeupe
kulikuwa kumeandikwa:
Kutoka kwa John Hardwick, S3
Connaught Boulevard, Pasadena City.
Kwa muda nilishangazwa aliwezaje
kuniletea fedha haraka kiasi kile, lakini nikasema huenda alikuwa na
mawasiliano na kampuni ya Express ambayo huenda aliwapigia simu mara tu baada
ya kunipigia mimi. Ofisi yao ilikuwa ng’ambo ya barabara jirani na jengo la
ofisi yangu.
Nilichukua kitabu cha simu na kuanza
kutafuta majina ya akina Hardwick. Hapakuwepo na jina la John Hardwick. Nilitoka
kwenye kiti na kuzunguka chumbani kutazama Ramani ya Mtaa. Ilionyesha kwamba Jack
S. Myers, Jnr., na siyo John Hardwick, ndiye aliyekuwa akiishi mtaa wa 33
Connaught Boulevard.
Nilikikanyaga kivuli change cha saa
kumi na mbili wakati nikitafakari tukio hilo. Nikakumbuka kwamba mtaa wa Connaught
Boulevard ulikuwa katika barabara ya nje kwenye Mlima Palma, takriban maili
tatu kutoka katikati ya jiji. Lilikuwa ni eneo ambalo watu wangeweza kukodi
nyumba wakiwa mapumzikoni: hali hii huenda ndiyo aliyokuwa nayo John Hardwick na
mkewe. Anaweza kuwa ofisa mkubwa wa kampuni ya Herron Corporation, akisubiri
nyumba yake imalizike ujenzi, na kwa wakati huu, alikuwa amepanga 33 Connaught
Boulevard kutoka kwa Jack S. Myers, Jnr.
Nimewahi kufika Connaught Boulevard mara
moja tu na hii ilikuwa kitambo sana. Eneo hilo liliendelezwa baada ya vita:
hakukuwa na kitu chochote cha kuvutia. Mengi yalikuwa mahekalu, nusu ya
matofali, nusu mbao. Jambo zuri la pekee kuhusiana na mtaa wa Connaught
Boulevard lilikuwa mazingira yake yanayokuwezesha kuuona mji na bahari, na kama
ungependa, upweke wake.
Kwa kadiri nilivyoifikiria kazi hii,
ndivyo nilivyozidi kuichukia. Sikuwa hata na maelekezo ya mwanamke ambaye
nilipaswa kumchunguza. Kama nisingekuwa nimelipwa dola mia tatu nisingeweza
kuifanya kazi hiyo bila kuonana kwanza na Hardwick, lakini kwa kuwa tayari
nilikwishalipwa, niliona nalazimika kufanya kile alichotaka nifanye.
Niliifunga ofisi yangu, halafu baada
ya kuvuka ofisi ya nje, nikafunga mlango wa nje na kuelekea kwenye lifti.
Jirani yangu, Mkemia wa Viwanda,
alikuwa akiendelea na harakati za kusaka maisha. Nilisikia sauti yake kali
ikielekeza ama kwenye rekoda ama kwa katibu muhtasi wake.
Nilipanda lifti hadi chini na baada
ya kuvuka mtaa, nikaingia kwenye baa ya Quick Snack ambako daima ndiko
nilikopata mlo wangu. Nilimuuliza Sparrow, mtu wa kaunta, kunipatia mkate na
kuku.
Sparrow, mrefu na mwembamba
aliyekuwa na nywele nyeupe, alikuwa amevutiwa na mambo yangu. Hakuwa mtu mbaya,
na mara kwa mara, nilimfurahisha kwa uongo mwingi kuhusu mambo ambayo
aliyependa yaliyonitokea.
“Uko kazini usiku huu, Bwana Ryan?” aliuliza
kwa shauku wakati alipoanza kunitengeneza vitafunwa.
“Ndiyo,” Nilisema. “Ninatumia usiku
huu na mke wa mteja wangu, kuhakikisha hafanyi upumbavu.”
Mdomo wake ukaachama huku
akinitazama kwa mshangao, “Ni kweli? Yukoje, Bwana Ryan?”
“Unamfahamu Liz Taylor?”
Akaitikia, akiinama na kupumua kwa
nguvu.
“Unamfahamu Marilyn Monroe?”
Koo lake likapanda ghafla.
“Hakika namfahamu.”
Nikampa tabasamu la huzuni.
“Hafanani na mmoja wao.”
Akapepe, baada ya kugundua kwamba
nilikuwa namtania, akatabasamu.
“Umeigonga pua yangu mahali ambapo
haistahili kugongwa, huh?” akasema.
“Pengine niliombea hilo.”
“Harakisha, Sparrow,” Nilisema. “Nahitaji
kutafuta malipo yangu ili niishi.”
Aliweka sandwich kwenye mfuko wa
karatasi.
“Usifanye chochote ambacho hukulipwa
ukifanye, Bwana Ryan,” alisema, akinipatia mfuko.
Muda huo ilikuwa yapata saa moja na
dakika ishirini. Niliingia kwenye gari yanguna kuendesha kuelekea Connaught
Boulevard. Sikufanya haraka. Wakati naendesha kwenye barabara hiyo ya mlimani,
jua la mwishoni mwa mwezi Septemba lilikuwa linazama kwenye kilele cha mlima.
Majumba kwenye mtaa wa Connaught
Boulevard yalikuwa yamekingwa upande wa barabani na uzio wa mbao au vichaka vya
maua. Niliendesha taratibu kupita nyumba Na. 33. Mageti makubwa mawili
yaliificha nyuma. Takriban yadi ishirini au zaidi kwenye barabara hiyo kulikuwa
na uwanda ambao ulikuwa mzuri kwa kutazama bahari. Nilisimama pale, nikazima
gari na kuhama kutoka kwenye kiti cha dereva na kuketi kiti cha abiria. Kutoka
upande huu nilikuwa katika nafasi nzuri ya kuyatazama mageti yale.
Sikuwa na chochote cha kufanya bali
kusubiri. Hili ni jambo ambalo nilikuwa mzoefu nalo. Kama una wazimu wa kutaka
kufanya kazi kama yangu, ustahamilivu ndicho kiungo muhimu zaidi.
Saa moja baadaye, magari mawili au
matatu yalipita hapo. Madereva, wanaume wakirejea kutoka kutafuta sembe ya
watoto, walinitazama wakati wakipita. Nadhani nilionekana kama mwanamume
anayemsubiri mpenzi wake, na siyo kama mtu aliyekuwa akimchunguza mke wa mteja
wake.
Msichana, akiwa amevaa skini taiti
na sweta, alipita pembeni ya gari langu. Mwanamume alipita akikimbia kumpita,
akaingia kwenye miti. Binti Yule alinitazama wakati macho yangu yakisawiri
umbile lake maridhawa. Aliniona sikuwa na hamu naye kuliko mimi nilivyomuona.
Nilimtazama kwa masikitiko akipotelea mbali.
Hadi kufikia saa tatu usiku giza
lilikuwa limetanda. Nilichukua mfuko wa karatasi na kula sandwich. Nilikunywa
funda la whisky kutoka kwenye chupa niliyoiweka ndani.
Kilikuwa kipindi kirefu cha
kufubiri, kilichochosha. Mageti kwenye Na. 33 yalikuwa yametulia tu. Lakini
sasa kulikuwa na giza mno kwangu kuanza harakati zangu. Nililiacha gari na
kuvuka barabara. Nilifungua mojawapo ya mageti hayo na kutazama bustani ndogo.
Kulikuwa na mwanga kidogo kuona nyasi nzuri, maua na njia iliyoelekea kwenye
hekalu ambalo mbele yake kulionekana kuwepo na baraza.
Itaendelea
kesho…
Comments
Post a Comment